Na John Gagarini, Bagamoyo
MBUNGE wa Jimbo la Chalinze wilayani Bagamoyo mkoani Pwani Said Bwanamdogo anatarajia kuzindua mpango wa kuweka kuweka vifaa vya huduma ya kwanza kwenye shule ambazo ziko mbali na huduma za afya katika jimbo hilo Julai mwaka huu.
Akizungumza na vikundi vya wajasiriamali vya Upendo Saccos na Uamke Saccos kwenye kata za Miono na Mkange wilayani humo,alisema kuwa uzinduzi huo anatarajia kuufanya Julai mwaka huu.
Bwanamdogo alisema kuwa gharama za kutekeleza mpango huo ni kiasi cha shilingi milioni 31 ambapo tayari ameshapata kiasi cha shilingi milioni 12 kwa ajili ya mpango huo.
“Baadhi ya shule ziko mbali na huduma za afya sasa haiwezekani mwanafunzi anaumwa ugonjwa mdogo anashindwa hata kupata panado ni jambo ambalo halipendezi ndiyo sababu ya mimi kubuni mpango huo kwa shule zote ambazo ziko mbali na huduma hizo,” alisema Bwanamdogo.
Katika hatua nyingine amewataka viongozi wakuchaguliwa katika jimbo la chalinze wilaya ya Baagamoyo Mkoani Pwani kutekeleza ahadi mbalimbali walizozitoa kwa wananchi ili kujenga imani na ili kuleta maendeleo ya eneo husika.
Aidha alisema wakati alipokuwa akigombea ubunge aliahidi kuwezesha wanawake,vijana,sekta ya afya,elimu na miradi suala ambalo amelivalia njuga na tayari ameshawezesha kiasi cha sh m 170 katika vijiji 66 kati ya 75 jimboni humo.
“Ni vijiji tisa vilivyobaki natarajia kukamilisha maombi yao mapema kabla ya mwaka huu kwisha na kuendelea na mipango mingine aliyojiwekea kwa kipindi cha miaka miwili na nusu iliyobaki.
Katika kata ya Miono ameweza kutoa sh M 32 na alikabidhi kiasi cha sh Milioni moja kwa kwa Saccos ya akinamama Upendo na UWAMKE milioni moja.
Mwisho
No comments:
Post a Comment