Na John Gagarini, Kibaha
MJUMBE wa Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya ya Wazazi ya Chama
Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Pwani David Mramba ametoa mipira sita kwa timu za
mpira wa pete za kata ya Kibaha.
Mramba alikabidhi mipira hiyo kwa manahodha wa timu za Umoja
wa Wanawake Tanzania (UWT) kwa matawi ya kata hiyo kwa lengo la kucheza ligi ili
kupta timu ya kata.
Alisema kuwa aliona
changamoto kubwa ya ukosefu wa vifaa vya michezo ikiwemo mipira ndiyo sababu ya
yeye kutoa mipira hiyo ili iweze kusaidia kukabiliana na changamoto hiyo.
“Mipira hii iwe changamoto kwenu katika kukabiliana na
ukosefu wa vifaa kwani kwa sasa michezo mbali ya kuimarisha afya zenu pia ni
ajira hasa kwa vijana ambao wengi hawana ajira,” alisema Mramba.
Aidha alisema kuwa mipira hiyo itasaidia kufanikisha kufanya
mashindano ya ngazi ya matawi ambayo inatarajiwa kuanza kufanyika mwezi wa
Julai.
“Mashindano hayo yataleta mahusiano mazuri baina ya wanachama
wa CCCM na hata jamii kwa ujumla hivyo mipira hiyo itumike na si kuiweka ndani
kama mapambambo,” alisema Mramba.
Naye Diwani wa Viti Maalumu Selina Wilson alizitaka timu hizo
kuanza maandalizi mapema kwani tayari wameshapata mipira ambayo ilikuwa
ikiwafanya washindwe kufanya mazoezi na kukutana kwenya mashindano tu.
Akishukuru kukabidhiwa mipira hiyo katibu wa UWT kata ya
Kibaha Sada Duda alisema kuwa kwao hiyo ni changamoto ambayo itawafanya
wahamasike na kushiriki michezo ipasavyo. Matawi yaliyopewa mipira hiyo kila
tawi likipata mpira mmoja ni Mwendapole A, Kwa Mfipa, Changombe, Kitende,
Simbani na Mwendapole B.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment