Na John Gagarini, Kibaha
JESHI la Polisi mkoani Pwani linamshikilia John Semindu mkazi
wa Kibamba CCM kwa tuhuma za kujifanya kuwa ni mtumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu
kitengo cha usalama na kujipatia fedha kwa watu mbalimbali kwa ahadi ya
kuwatafutia kazi serikalini.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoani
humo Ulrich Matei alisema kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa akitumia kitambulisho cha
usalama wa Taifa kujipatia fedha kwa njia hiyo ya udanganyifu.
Matei alisema kuwa katika upekuzi mtuhumiwa alikutwa na vyeti
vya watu mbalimbali vya kitaaluma kwa madai ya kuwatafutia nafasi za kazi
serikalini.
“Mtuhumiwa tunamshikilia na uchunguzi bado unaendelea ambapo alikuwa
akitumia gari aina ya Suzuki Escudo rangi ya bluu yenye namba za usajili T 383
ARA,” alisema Matei.
Kamanda Matei aliongeza kuwa mtuhumiwa huyo anatarajiwa
kufikishwa mahakamani siku ya Jumatatu ijayo kujibu tuhuma hizo zinazomkabili.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment