JESHI la Polisi
mkoani Pwani linamshikilia aitwaye Francis Siza miaka (26) kwa tuhuma za
kumuuwa mama yake mzazi Naomi Isaka (55) kwa kumpiga na mchi kichwani.
Akizungumza
na waandishi wa habari mjini Kibaha kamanda wa polisi mkoani humo Ulrich Matei alisema
kuwa tukio hilo lilitokea leo majira ya saa 1:30 asubuhi eneo la Kiluvya
A wilaya ya Kisarawe.
Kamanda Matei
alisema kuwa kijana huyo alifanya tukio hilo baada ya kubaki yeye na mama yake
baada ya wadogo zake wawili wa kike ambao ni wanafunzi kwenda shule.
“Alimpiga na
mchi kichwani mara mbili uapande wa kushoto na kulia chanzo kikiwa ni kutaka
kuuza kiwanja cha mama yake ambapo ni siku moja tangu arudi baada ya kusafiri
kusikojulikana,” alisema Kamanda Matei.
Baadhi ya majirani
ambao walishuhudia tukio hil Nolasko Zenobisi alisema wakati alipokuwa
akiendelea na shughuli zake za kulima alisikia kelele zikipigwa ndipo
alipokwenda katika nyumba hiyo na aliweza kukuta tayari mama huyo ameshafariki.
Zenobisi
alisema alipowajulisha majirani na kuanza kumtafuta mtuhumiwa na kwa bahati
nzuri walimpata akiwa amijificha kichakani ndipo walipomfunga kamba na kumpeleka
eneo alilofanyia tukio.
Aidha
alisema kwamba kijana huyo ambaye ndiye wa kwanza kuzaliwa katika familia yao
alifanya tukio hilo la mauaji baada ya mdogo wake wa kike
anaiyeitwa Neema Siza kuondoka nyumbani na kuelekea shule ya sekondari
Makulenge ambapo ndipo anaposoma kidato cha tatu.
Naye
shuhuda mwingine ambaye akutaka jina lake litajwe gazeti alisema kwamba pia nay
eye asubuhi hiyo alikuwa shambani anaalia ndipo aliposikia sauti na mtu anapika
makelele na kufa na alipokwenda alimwona huyo kijana anakimbia mbio ndipo
wananchi wengine walipoamua kumkimbiza na kumkamata.
Hata hivyo
baadhi ya majirani wengine walisema kwamba kijana huyo alifika mnamo April 14
majira ya saa 4:30 usiku na kumgongea mama yake mzazi na alifunguliwa na
kuingia ndani kulala lakini asubuhi akaamua kufanya tukio hilo.
Naye mtoto wa
Marehemu Neema Siza ambaye anasoma shule ya Makurunge alisema kwamba asubuhi
aliondoka na kumwaga mama yake vizuri na kwenda shule na kwamba nyumbani
alimwacha kaka yake huyo wa kwanza pamoja na mama yake.
Kwa upande wake
mtuhumiwa huyo alisema kuwa kwa upande wake yeye hakugombana wala hawakuwa na
ugomvi wowote na mama yake mzazi isipokuwa alifanya hivyo baada ya kumwona mama
yake mzazi anateseka hivyo akaona bora ampige na kumuuwa ili aweze kupumzika.
“Lakini
kutokana na kosa ambalo nimelifanya kwa sasa najuta, lakini ninafahamu kuwa
sheria itachukua mkondo wake, ingawa mimi nimefanya hivyo kwa sabbau tangu siku
nyingi niliona mama yangu anateseka sana, na ukizingatia baba yetu naye
alishafariki dunia kwa hiyo hali halisi ndiyo iliyofanya nifanye hivyo na
hakuna kitu kingine,” alisema Siza.
No comments:
Post a Comment