Na John Gagarini,
Kibaha
BONDIA wa Maili Moja Kibaha mkoani Pwani Nzumba Nkukwe leo
Jumamosi anatarajia kupanda ulingoni kupambana na bondia Yusuph Yusuph wa
Chalinze wilayani Bagamoyo.
Kwa mujibu wa katibu wa katibu wa chama cha ngumi mkoa wa
Pwani Halfan Mrisho “Swagala” alisema kuwa pambano hilo litachezwa kwenye
ukumbi wa Ndelema uliopo Chalinze.
Swagala alisema kuwa pambano hilo litakuwa ni la kirafiki kwa
kuwapima uwezo wao mabondia hao pamoja na kuhamasisha watu kucheza mchezo huo
mkoa Pwani.
“Lengo kuu ni kumwandaa Nkukwe ambaye anatakiwa kucheza
mapambano 12 ili aweze kushiriki kwenye mashindano ya ubingwa hapa nchini,”
alisema Swagala.
Aidha alisema kuwa pambano hilo lililodhaminiwa na Big Right
litakuwa la raundi 12 na linatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa mabondia hao
wa mkoa huu.
“Nawaomba mashabiki waje kwa wingi ili kuwahamasisha mabondia
wa nyumbani na kutakuw ana usafiri kutokea Maili Moja hadi Chalinze hivyo
itakuwa ni nafasi kwa wadau wa ngumi kujionea vipaji vya vijana wao,” alisema
Swagala.
Alitoa shukrani kwa mdhamini wa mapambano Omary Kimbau kwa
jitihada zake za kuhamasisha mchezo huo kwa vijana wa mkoa wa Pwani kwani
amekuwa akiwaandalia mapambano mbalimbali mabondia.
Mwisho.
Na John Gagarini, Kibaha
MCHEZO wa nusu fainali kati ya Fire na Lisborn ulishindwa
kutoa mshindi baada ya mwamuzi wa pambano hilo Hamad Mbegu kutimua mbio kuhofia
usalama wake baada ya kumaliza mpira zikiwa zimesalia dakika chache zikiwa
hazijatiamia dakika 90 na kuamuru yapigwe matuta timu hizo zikiwa sare ya 1-1.
Mchezo huo wa nusu fainali ya pili kuwania kombe la Kibaha
Super Cup ulipigwa kwenye uwanja wa Bwawani Maili Moja wilayani Kibaha
ulizikutanisha timu hizo ili kupata mshindi ambaye angeungana na Mwanalugali
kucheza hatua ya fainali.
Chanzo cha mwamuzi huyo kukimbia ni pale alipoashiria mpira
kwisha huku zikiwa bado dakika 5 kutimia dakikia 90 alimaliza pambano na
kuashiria matuta lakini washabaiki wa timu ya Lisborn walimfuata na kumzonga
huku wakimtishia kumpiga.
Kutokana na mzozo huo mwamuzi aliwaita wachezaji wa Lsborn
kwa ajili ya kupiga matuta lakini walionekana kusuasua hali iliyofanya muda
mwingi upotee karibu dakika 10 hivi huku washabiki wakiwa wamezingira eneo la
goli zilipotakiwa kupigwa penati hali iliyomtia hufo mwamuzi huyo na kukimbia.
Mbali ya hali hiyo pambano hilo lilikuwa na mvutano mkubwa
huku timu hizo zikionyesha kandanda safi na walikuwa Lisborn walioandaika bao
la kuongoza kupitia kwa Kulwa Mwanda dakika ya 72 na Fundikira Fundikira wa
Fire alisawazisha kwenye dakika ya 80 ya mchezo, mchezo huu utarudiwa leo
Jumamosi kwenye uwanja huo huo.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment