Tuesday, January 27, 2026

WANASIASA WANAWAKE WATAKIWA KUJIKITA KWENYE UCHUMI

WANAWAKE wanasiasa Wilayani Kibaha wametakiwa kupambana kukuza uchumi wao ili kukabiliana na changamoto ukatili wa kijinsia wanazozipata kipindi cha kuwania uongozi.

Akizungumza na waandishi wa habari Mjini Kibaha mgombea Udiwani Kata ya Kibaha kupitia Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) Hamo Machapula amesema kuwa wanawake wengi wamekuwa wakikumbana na changamoto hiyo kutokana na kuwa na uchumi duni.

Machapula amesema kuwa ili kupata uongozi kwa mwanamke ni changamoto kubwa sana kutokana na baadhi ya viongozi wanaume kuwakwamisha kutokana na kuwawekea vikwazo.

"Ili tuweze kufanikiwa kupata uongozi lazima tuwe na uchumi imara ili tuweze kufanikiwa lakini uchumi wetu ukiwa chini ni changamoto kuwa viongozi,"amesema Machapula.

Alisema kuwa wanawake wanauwezo mzuri wa kuwa viongozi lakini wanakumbana na vitendo vya ukatili wa kijinsia kutoka kwa viongozi wanaume pale wanapotaka kuwania nafasi za uongozi.

"Ninachowasihi wanawake wenye ndoto za kuwa viongozi ili kukabiliana na vitendo vya ukatili pale wanapowania nafasi za uongozi ni kuwa na uchumi imara ili kukabili vitendo hivyo,"amesema Machapula.

Aidha amesema kuwa uongozi wa vyama unapaswa kuchukua hatua kwa viongozi wanaojihusisha na vitendo hivyo ili wachukuliwe hatua za kinidhamu.

"Kwanza tunapaswa kutoa taarifa pale tunapokumbana na kadhia hizo badala ya kukaa kimya kwani ukimya wetu utatusababishia madhara makubwa na kufifisha ndoto zetu,"amesema Machapula.

Alibainisha kuwa wanawake ndani ya vyama wajishughulishe na shughuli mbalimbali ili kujiongezea kipato kwani siasa inaendana na uchumi.

Monday, January 26, 2026

MITI 6,379 KUPANDWA PWANI KUMBUKIZI KUZALIWA DK SAMIA SULUHU HASSAN

MITI 6,379 itapandwa Mkoani Pwani katika kuadhimisha siku ya kumbukizi ya kuzaliwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Mkuu Abubakar Kunenge amesema zoezi hilo litafanyika kesho huko Wilayani Rufiji.

Kunenge amesema kuwa zoezi la upandaji wa miti hiyo ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Rais katika kulinda na kutunza mazingira hapa nchini ili kukabili mabadiliko ya Tabianchi.

"Zoezi hilo litahusisha upandaji wa miti ya matunda 671 pamoja na miti 5,708 ya mbao na vivuli, ambayo itapandwa katika maeneo ya shule ili kuwajengea wanafunzi utamaduni wa kutunza mazingira,"amesema Kunenge.

Amesema kuwa zoezi hilo ni sehemu ya mpango wa Mkoa wa Pwani wa kupanda jumla ya miti milioni 13.5 wakati wa mvua za masika pamoja na ugawaji wa miche ya mikorosho milioni 1.5 kwa wakulima wa Wilaya ya Rufiji chini ya kauli mbiu “Uzalendo ni Kutunza Mazingira – Shiriki Kupanda Miti.”

HALMASHAURI YAKABIDHI MADAWATI 4,000

HALMASHAURI ya Manispaa ya Kibaha imetoa madawati viti na meza 4,000 kwa Shule za Msingi na Sekondari vikiwa na thamani ya shilingi milioni 400.

Akikabidhi madawati viti na meza Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Nickson John alisema kuwa Halmashauri imefanya jambo zuri la kukabili changamoto ya wanafunzi kukaa chini.

Kwa upande wake Meya wa Manispaa ya Kibaha Dk Nicas Mawazo alisema kuwa idadi ya wanafunzi inaongezeka kutokana na wazazi kuhamia Kibaha.

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha Dk Rogers Shemwelekwa alisema kuwa walitenga kiasi cha shilingi milioni 400 kwa ajili ya kutengeneza madawati viti na meza 4,000 ikiwa kwa Shule za Msingi madawati 2,000 na Sekondari viti na meza 2,000.

Sunday, January 25, 2026

VIJANA WATUNZE AMANI

MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) NEC Taifa kupitia Jumuiya ya Wazazi Hamoud Jumaa ameitaka Jumuiya hiyo kuwapa vijana malezi mazuri ili watunze amani.

Jumaa ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kibaha Vijijini ameyasema hayo Mjini Kibaha wakati akifungua baraza la Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Pwani.

Amesema kazi ya Jumuiya hiyo ni kuhakikisha jamii hususani vijana wanakuwa na malezi bora ili kutojiingiza kwenye makundi ambayo hayana maadili mema.

"Tuwape elimu na malezi mazuri vijana wetu na tuzungumze nao juu ya amani kwani amani pia huleta afya njema na amani ndiyo kila jambo hivyo tuhubiri amani,"amesema Jumaa.  

Aidha amesema vijana nchini wanapaswa kudumisha amani na kutokubali kurubuniwa ili wasivunje amani iliyopo kwani bila amani hatutaweza kufanya mambo ya maendeleo.

"Vijana wanapaswa kulinda amani kwani ndiyo msingi wa Taifa la Tanzania na wasukubali kushawishiwa na watu kuharibu amani iliyopo kwani ikipotea ni gharama kuirudisha,"amesema Jumaa.

Amewataka viongozi wa Jumuiya  hiyo kuanza maandalizi ya uchaguzi wa Jumuiya utakaofanyika mwakani kwani uchaguzi ndani ya chama ni mgumu kuliko uchaguzi wa vyama.

"Muanze maandalizi na kama kuna kiongozi anaona anauwezo ajiandae kugombea kwenye chama wakati ukifika kwani Jumuiya hii ndiyo inayobeba jumuiya zote za chama,"amesema Jumaa.

Aliongeza kuwa viongozi wanapaswa kuacha alama kwa kuwa na miradi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kununua ardhi pamoja na ofisi za makatibu wa jumuiya kwa kila wilaya.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Mkoa wa Pwani Josiah Jackson amesema kuwa uchaguzi umekwisha kilichobaki ni kujenga jumuiya na chama.

Jackson amesema kuwa wanachama waache makandokando kwa kuwaacha waliochaguliwa wafanye kazi zao na kuwaunga mkono ambapo kwa mkoa walipata madiwani 17 kutoka jumuiya.

Naye katibu wa CCM Mkoa wa Pwani  Kitte Mfilinge amesema kuwa anaipongeza jumuiya kwa kufanya vizuri kwenye uchaguzi mkuu kwani mkoa umeshika nafasi tatu za juu hapa nchini.

Mfilinge amesema kuwa Jumuiya hiyo iko vizuri kwani ina mshikamano na imetulia hivyo kwa sasa wajiandae na uchaguzi wa jumuiya mwakani lengo ni kujenga chama ili kiwe imara.

Saturday, January 24, 2026

VIJANA WAPEWE MALEZI BORA KULINDA AMANI

MZJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) NEC Taifa kupitia Jumuiya ya Wazazi Hamoud Jumaa ameitaka Jumuiya hiyo kuwapa vijana malezi mazuri ili watunze amani.

Jumaa ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kibaha Vijijini ameyasema hayo Mjini Kibaha wakati akifungua kikao cha Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Pwani.

Amesema kazi ya Jumuiya hiyo ni kuhakikisha jamii hususani vijana wanakuwa na malezi bora ili kutojiingiza kwenye makundi ambayo hayana maadili mema.

"Tuwape elimu na malezi mazuri vijana wetu na tuzungumze nao juu ya amani kwani amani pia huleta afya njema na amani ndiyo kila jambo hivyo tuhubiri amani,"amesema Jumaa.  

Aidha amesema vijana nchini wanapaswa kudumisha amani na kutokubali kurubuniwa ili wasivunje amani iliyopo kwani bila amani hatutaweza kufanya mambo ya maendeleo.

"Vijana wanapaswa kulinda amani kwani ndiyo msingi wa Taifa la Tanzania na wasukubali kushawishiwa na watu kuharibu amani iliyopo kwani ikipotea ni gharama kuirudisha,"amesema Jumaa.

Amewataka viongozi wa Jumuiya  hiyo kuanza maandalizi ya uchaguzi wa Jumuiya utakaofanyika mwakani kwani uchaguzi ndani ya chama ni mgumu kuliko uchaguzi wa vyama.

"Muanze maandalizi na kama kuna kiongozi anaona anauwezo ajiandae kugombea kwenye chama wakati ukifika kwani Jumuiya hii ndiyo inayobeba jumuiya zote za chama,"amesema Jumaa.

Aliongeza kuwa viongozi wanapaswa kuacha alama kwa kuwa na miradi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kununua ardhi pamoja na ofisi za makatibu wa jumuiya kwa kila wilaya.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Mkoa wa Pwani Josiah Jackson amesema kuwa uchaguzi umekwisha kilichobaki ni kujenga jumuiya na chama.

Jackson amesema kuwa wanachama waache makandokando kwa kuwaacha waliochaguliwa wafanye kazi zao na kuwaunga mkono ambapo kwa mkoa walipata madiwani 17 kutoka jumuiya.

Naye katibu wa CCM Mkoa wa Pwani  Kitte Mfilinge amesema kuwa anaipongeza jumuiya kwa kufanya vizuri kwenye uchaguzi mkuu kwani mkoa umeshika nafasi tatu za juu hapa nchini.

Mfilinge amesema kuwa Jumuiya hiyo iko vizuri kwani ina mshikamano na imetulia hivyo kwa sasa wajiandae na uchaguzi wa jumuiya mwakani lengo ni kujenga chama ili kiwe imara.

Friday, January 23, 2026

AJIPATIA KIPATO KUPITIA PANYA WEUPE

VIJANA Mkoani Pwani wameshauriwa kuchangamkia mradi wa ufugaji panya weupe ambao ni chanzo cha mapato ambapo mmoja huuzwa kati ya shilingi 3,000 hadi 5,000 kwa panya mmoja.

Akizungumza na waandishi wa habari Mjini Kibaha Mtaalamu wa Mifugo na Kilimo Rodney Mwasha amesema kuwa ufugaji wa panya hao hauna gharama kubwa.

Mwasha amesema kuwa panya hao ambao asili yao ni kutoka Japan wanatumika mashuleni kwa ajili ya mafunzo kwa wanafunzi mashuleni kwa somo la Bailojia.

"Panya hawa ni rahisi kuwafuga na hawana usumbufu na hata kuwahudumia ni rahisi kwani ni rafiki na siyo wakorofi na hawakufanyi kushindwa kufanya shughuli nyingine,"amesema Mwasha.

Amesema kuwa mradi huo ni mzuri na hautumii gharama kubwa za uzalishaji ambapo panya mmoja anauwezo wa kuzaa watoto nane hadi 10 kwa wakati mmoja na huzaa kila mwezi.

"Mimi nafuga kuku wa kienyeji, bata bukini, bata mzinga, nyuki na upande wa kilimo nalima mbogamboga na kuzalisha uyoga hivyo ufugaji wa panya nao ni sehemu ya kuongeza kipato,"amesema Mwasha.

Aidha amesema kuwa mahitaji ya panya kwa mashule ni kubwa sana hivyo vijana watumie fursa hiyo ili waweze kuongeza kipato chao na familia zao.

"Changamoto ya hawa panya ni nyoka ambao hupenda sana kula panya hivyo endapo hujaimarisha banda wanaweza kuliwa na changamoto nyingine ni maradhi,"amesema Mwasha.

Aliongeza kuwa panya hao chakula chao ni pumba, nafaka kama vile mahindi mtama na dagaa ambapo panya 300 gharama za kuwalisha ni kama 100,000 na faida ni kama milioni 1.5.

"Panya hawa wana uwezo wa kuishi miaka miwili na yeye alianza kwa kufuga panya wanne na sasa ana panya 300 hadi 400 ambapo soko lake huwa kipindi cha katikati ya mwaka,"amesema Mwasha.

Wednesday, January 21, 2026

FIDIA LAMI MAILI MOJA SHELI-MUHEZA ZAIVA

WANANCHI 65 wanaopitiwa na mradi wa ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kutoka Barabara kuu ya Morogoro Bp Sheli hadi Muheza Kata ya Maili Moja Wilaya ya Kibaha wamefanyiwa tathmini kwa ajili ya kulipwa fidia.

Diwani wa Kata ya Maili Moja Ramadhan Lutambi amesema kuwa zoezi hilo ni muhimu kabla ya kuanza kutekelezwa kwa mradi huo Uboreshaji Miundombinu ya Miji Tanzania (TACTIC) kwa Manispaa ya Kibaha.

Lutambi amesema kuwa barabara hiyo ni muhimu sana kwani itaufungua Mji wa Maili Moja pia itafungua uchumi wa wakazi wa Kata hiyo kuondoa changamoto ya ubovu wa barabara.

"Ninachowaomba wananchi kutoa ushirikiano ili ujenzi usiwe na changamoto kwani kwa sasa hichi ndiyo kipaumbele cha Kata yetu kwa mwaka huu lazima lami ijengwe ikiwa ni awamu ya kwanza,"amesema Lutambi.

Amesema ni mradi muhimu sana kwani utafungua fursa nyingi za kiuchumi na kurahisisha usafiri kuwa wa haraka na usafirishaji na Mji utajengeka na kuleta maendeleo kwenye Mitaa ya Uyaoni, Maili Moja Shule na Muheza.

Naye Salum Mizoka Mthamini wa mradi kutoka Kampuni ya Botek ambaye ni Mkandarasi mshauri kwa kushirikiana na Kampuni ya Uress amesema zoezi hilo linakwenda vizuri.

Mizoka amesema kuwa uthamini unaofanyika ni kujua kila mlengwa anadai na atalipwa nini na baada ya hapo malipo yatafanyika kwa wahusika ambao wameshatambuliwa kwenye barabara hiyo kwa awamu ya kwanza ikianza na kilometa 4.

Amesema kuwa lengo la kufanya tathmini ni kuhakikisha kila mtu anayepitiwa na mradi huo ambapo sehemu za nyumba au baraza zinataguswa watalipwa fidia.

"Tunataka kusiwe na migogoro wakati wa utekelezaji wa mradi ili ujenzi ufanyike bila ya manunguniko kwani walengwa watalipwa stahiki zao bila ya tatizo lolote,"amesema Mizoka.

Aidha amesema kuwa malipo hayo yanafanywa kulingana na hali ya soko kwa sasa na hadi wakati huu hakuna changamoto na zilizopo ni ndogo ndogo.