Sunday, January 5, 2025

COREFA KUANDAA VIJANA KWENYE VITUO KILA WILAYA

CHAMA Cha Soka Mkoa wa Pwani (COREFA) kimesema kitahakikisha kila Wilaya inakuwa na kituo cha kuandaa vijana ili kuzalisha wachezaji watakaokuja kulitumikia Taifa.

Aidha amesema kwa sasa kuna vituo vinne lakini lengo ni kuwa na vituo saba na baadaye kuwe na vituo kila Halmashauri za mkoa huo ambazo ziko 9.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Mjini Kibaha Mwenyekiti wa Corefa Robert Munis amesema kuwa kwa sasa changamoto za viwanja hazipo kwani viwanja vipo vingi.

Munis amesema kuwa kwa sasa wanahamasisha wazazi kuhakikisha wanawawezesha watoto wao ili washiriki kwenye soka ili vijana wa Mkoa huo waweze kutumia vipaji vyao kujiletea maendeleo

"Tunawapongeza wenzetu Chalinze wameanza ligi ya vijana chini ya miaka 15 haya ndiyo tunayoyataka kwani Pwani lazima Mpira Uchezwe ndiyo kauli mbiu yetu,"amesema Munis.

Amesema kuwa mpira ni ajira lakini ili kufikia lengo hilo lazima ushiriki wa wazazi nao uwepo kwa kuwawekea mazingira ili waweze kucheza na wasiwazuie watoto kucheza.

"Tumeanza mpango wa kusajili shule za soka Academy na kuzitambua ili tushirikiane nao ili malengo yetu yatimie kama viwanja vipo kwa nini vijana wasicheze tuhakikishe vijana wetu wanacheza mpira kwani wataliwakilisha vyema Taifa,"amesema Munis.

Ametaja baadhi ya viwanja vilivyopo ndani ya Mkoa wa Pwani kuwa ni Mwanambaya, Bungu, Mabatini, Tumbi, Mwanakalenge, Kiromo, Msoga, Maili Moja Mwendapole, Kwambonde na vingine vingi ambavyo baadhi vinatumika na vingine viko kwenye ujenzi.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa chama hicho ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya mipango na fedha Mohamed Lacha amesema wanawashukuru wadau mbalimbali ambao wamefanikisha kupata ofisi ya kisasa.

Lacha amesema kuwa jambo kubwa ni kuhakikisha Corefa inasonga mbele kwa kushirikiana na kuepukana na migogoro ambayo huwa inarudisha nyuma masuala ya soka.

Naye Mwenyekiti wa Chama Cha Soka la Wanawake Mkoa wa Pwani Asha Mbata amesema kuwa wanafarijika kwani kwa mwaka jana Wilaya zote zikichezesha ligi ya wanawake isipokuwa Mafia pekee ambapo ni mafanikio makubwa sana.

Mbata amesema kuwa wanaandaa ziara ya kutembelea Wilaya ili kuhamasisha wanawake na kucheza soka na Wilaya kuandaa ligi  kwa wanawake.

COREFA KUANDAA VIJANA KUPITIA VITUO KILA WILAYA

VIONGOZI WA DINI NCHINI JAMHURI YA AFRIKA YA KATI WAISHUKURU JWTZ

Umoja wa Viongozi wa madhehebu ya dini nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati wameonesha imani kubwa ya ulinzi wa amani unaotolewa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania nchini humu.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti mara baada ya kutembelewa na Kamanda wa Kikosi cha Nane cha Ulinzi wa Amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati Luteni Kanali Theofili Nguruwe wamesema uwepo wa JWTZ umekuwa na tija sana nchini humo kwani wamekuwa wakifanya kazi zao kwa weledi wa hali ya juu.

Akizungumza kwa niaba ya Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Berberati Mhashamu Koffi Denis, Karibu Mkuu wa Jimbo hilo Padre Jean Ancelimo amesema mbali na Ulinzi wa Amani pia limekuwa likitoa misaada mbalimbali ya hali na mali huku akitolea mfano wa ujenzi wa shule ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ambayo imepewa jina la Serengeti.

Naye Askofu Mkuu wa Kanisa la Evenjeliko (AEC) Mhashamu Lucian Nday amesema uwepo wa JWTZ nchini hapo umewafanya waishi kwa amani na zaidi ya yote limewezesha ukuaji wa lugha adhimu ya kiswahili.

Sheikh Rashid Mohamoud Arouna ni Imam wa Masjid Nuur amesema JWTZ limekuwa mstari wa mbele kwenye kila jambo ambalo wanaombwa kutoa msaada kwa ajili ya kuhakikisha nchi yao inakuwa na amani.

Kwa upande wa Kamanda wa Kikosi cha Nane cha Ulinzi wa Amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati Luteni Kanali Theofili Nguruwe amewashukuru viongozi hao na kuahidi kutekeleza majukumu yake kwa weledi wa hali ya juu.

Saturday, January 4, 2025

JESHI LA POLISI MKOANI PWANI LIMEKAMATA WATU 173 KWA TUHUMA ZA MAKOSA MBALIMBALI

WATUHUMIWA 173 wamekamatwa Mkoani Pwani kutokana na makosa mbalimbali ikiwa ni pamoja na nyaya za Shaba kilogramu 3,687.

Aidha kati yao watu wanne wamekamatwa kwa tuhuma ya kukutwa na meno ya Tembo nane yanayokadiriwa kuwa uzito wa kilogramu 67.

Hayo yamesemwa na Kamanda wa Polisi (ACP) Salim Morcase alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Mjini Kibaha kuelezea mafanikio ya misako na operesheni. 

Morcase amesema kuwa watuhumiwa hao walikamatwa katika kipindi cha mwezi Desemba mwaka jana 2024.

"Pia watuhumiwa hao walikamatwa na mafuta ya mafuta ya transfoma lita 80, mafuta ya dizeli lita 3,547, mitungi ya gesi 10, madawati 15 ya Shule ya Msingi Kibadagwe, mafuta ya kula dumu 45 sawa na lita 900,"amesema Morcase.

Amesema kuwa watuhumiwa 54 wamekamatwa kwa tuhuma za kukutwa na bhangi kilogramu 3 na gramu 120.5, mirungi kilogramu 7 na gramu 40, pia watuhumiwa 44 wakikamatwa na pombe ya moshi lita 86 na mtambo wa kupikia pombe hiyo.

"Watuhumiwa wengine walikamatwa na vitu mbalimbali vikiwemo injini ya gari aina ya Corolla, pikipiki 35, simu za mkononi 13, nondo 35 na vipande 12, kompyuta mpakato 1, redio 1, spika 2, vitanda 2 na magodoro yake na mabomba ya chuma 5,"amesema Morcase.

Akizungumzia kuhusu nyara za Serikali amesema watu wanne walikamatwa na nyama ya Swala vipande nane vyenye uzito wa kilogramu 32, vichwa vitano na miguu ya Tohe.

"Pia watu saba wamekamatwa kwa tuhuma za kuiba ngombe sita wenye thamani ya shilingi milioni 8.1 ambapo ngombe hao tumewaokoa,"amesema Morcase.

Amewataka wananchi kuendelea kutoa taarifa zinazohusu uhalifu na wahalifu kwa viongozi wa serikali za mitaa watendaji wa kata au kwa wakaguzi kata waliopo kwenye kata zao.

Monday, December 30, 2024

NYIKA MABINGWA MKOA WA PWANI

TIMU ya soka ya Nyika imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Mkoa wa Pwani kwa kuifunga timu ya Kiduli kwa goli 1-0 kwenye mchezo wa fainali wa ligi daraja la tatu ngazi ya Mkoa.

Mchezo huo ambao ulichezwa kwenye uwanja wa Mwendapole Mjini Kibaha ulihudhuriwa na viongozi wa Chama  Cha Soka Mkoa wa Pwani (COREFA), viongozi wa Chama Cha Soka Wilaya ya Kibaha KIBAFA na vyama vya Wilaya zingine na vyama shiriki na mashabiki wengi wa Kibaha.

Mwenyekiti wa COREFA Robert Munis akizungumza mara baada ya mchezo huo amesema kuwa lengo lao ni kuhakikisha mpira unachezwa ili kukuza vipaji vya soka Pwani.

Munis amesema kuwa fainali hiyo ambayo ilionyesha kiwango kikubwa cha wachezaji wa timu hizo zimeonyesha jinsi gani zilivyojiandaa na vijana kuonyesha uwezo mkubwa.

"Lengo letu ni kuhakikisha tunapambania timu zetu angalau zifike kucheza ligi kuu ya NBC angalau timu moja na hilo linawezekana kama tutaunganisha nguvu na kuziunga mkono timu zetu,"amesema Munis.

Kufuatia ushindi huo timu ya Nyika ilipewa kombe na itawakilisha mkoa wa Pwani kwenye mashindano ya Ligi ya mabingwa wa Mikoa (RCL) mwakani.

Saturday, December 28, 2024

JAMII YAWEZESHWA PEMBEJEO KILIMO CHA BUSTANI WILAYA YA KIBAHA

TAASISI ya Anjita Child Development Foundation ya Kibaha imetoa pembejeo za kilimo cha bustani ya mbogamboga zenye thamani ya shilingi milioni 10.8 kwa vikundi vya wakulima wa bustani kwenye Vitongoji vya Mwanabwito na Kidai Kata ya Kikongo kwa ajili ya kuongeza uzalishaji.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi kuwezesha jamii kupitia kilimo cha bustani na kukabidhi pembejeo  kwa vikundi hivyo Mkuu wa Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Evelyn Ngwira kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha amesema kuwa mradi huo utakwenda kubadilisha maisha ya jamii kwenye Kata hiyo.  

Ngwira amesema kuwa mradi huo wa uwezeshaji jamii ili kujikwamua kiuchumi na kuboresha afya na utasimamiwa na wanajamii wenyewe na watapaswa kufuata ushauri wa wataalamu wa kilimo.

"Mnapaswa kulima kwa kuzingatia kalenda ili kupata mazao mazuri ambayo yatakuwa na soko zuri na mradi huu utakuwa endelevu na mtasimamia wenyewe hivyo muwe mfano kwa awamu hii ya kwanza,"amesema Ngwira.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Anjita Janeth Malela amesema kuwa mradi huo umeibuliwa na wananchi wenyewe na wataundesha kwa kusimamiwa na taasisi na wataalamu wa kilimo.

Malela amesema kuwa pembejeo hizo ni ufadhili kutoka Ubalozi wa Marekani ukiwa na lengo la kuongaza kipato kwa familia na kuboresha afya kwa wananchi.

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kidai Samson Dotto kwa niaba ya diwani wa Kata ya Kikongo amesema kuwa kilimo ni uti wa mgongo kwani wao wanafanya shughuli hizo kando ya Mto Ruvu na utawasaidia kiwasogeza mbele kutoka hatua moja kwenda hatua nyingine.

Naye ofisa kilimo kata ya Kikongo Fortunatus Ng'itu amesema kuwa hiyo ni fursa muhimu kwa wananchi na wanapaswa kuitumia ili kubadili maisha yao.

Moja ya wanufaika wa mradi huo Eliwaza Kingu amesema kuwa wanaishukuru taasisi hiyo kwa kuwapatia mradi huo kwani utawasaidia kuwapunguzia gharama za kununulia pembejeo ambazo ni kubwa.

Kitongoji cha Mwanabwito ni vikundi  3 ambavyo vina watu 9 na kimoja kina watu 10 kwa Kitongoji cha Kidai kuna vikundi 6 kasoro vikundi 2 wapo  watu 5  wa tano.

TAASISI ya Anjita Child Development Foundation ya Kibaha imetoa pembejeo za kilimo zenye thamani ya shilingi milioni 10.7 kwa vikundi vya wakulima wa bustani kwenye Vitongoji vya Mwanabwito na Kidai Kata ya Kikongo kwa ajili ya kuongeza uzalishaji.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi kuwezesha jamii kupitia kilimo cha bustani na kukabidhi pembejeo  kwa vikundi hivyo Mkuu wa Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Evelyn Ngwira kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha amesema kuwa mradi huo utakwenda kubadilisha maisha ya jamii kwenye Kata hiyo.  

Ngwira amesema kuwa mradi huo wa uwezeshaji jamii ili kujikwamua kiuchumi na kuboresha afya na utasimamiwa na wanajamii wenyewe na watapaswa kufuata ushauri wa wataalamu wa kilimo.

"Mnapaswa kulima kwa kuzingatia kalenda ili kupata mazao mazuri ambayo yatakuwa na soko zuri na mradi huu utakuwa endelevu na mtasimamia wenyewe hivyo muwe mfano kwa awamu hii ya kwanza,"amesema Ngwira.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Anjita Janeth Malela amesema kuwa mradi huo umeibuliwa na wananchi wenyewe na wataundesha kwa kusimamiwa na taasisi na wataalamu wa kilimo.

Malela amesema kuwa pembejeo hizo ni ufadhili kutoka Ubalozi wa Marekani ukiwa na lengo la kuongaza kipato kwa familia na kuboresha afya kwa wananchi.

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kidai Samson Dotto kwa niaba ya diwani wa Kata ya Kikongo amesema kuwa kilimo ni uti wa mgongo kwani wao wanafanya shughuli hizo kando ya Mto Ruvu na utawasaidia kiwasogeza mbele kutoka hatua moja kwenda hatua nyingine.

Naye ofisa kilimo kata ya Kikongo Fortunatus Ng'itu amesema kuwa hiyo ni fursa muhimu kwa wananchi na wanapaswa kuitumia ili kubadili maisha yao.

Moja ya wanufaika wa mradi huo Eliwaza Kingu amesema kuwa wanaishukuru taasisi hiyo kwa kuwapatia mradi huo kwani utawasaidia kuwapunguzia gharama za kununulia pembejeo ambazo ni kubwa.

Kitongoji cha Mwanabwito ni vikundi  3 ambavyo vina watu 9 na kimoja kina watu 10 kwa Kitongoji cha Kidai kuna vikundi 6 kina watu 6 kasoro vikundi 2 wapo  watu 5  wa tano.

Thursday, December 19, 2024

KAMPUNI YA PPM GROUP YAHAMASISHA NISHATI SAFI NA UTUNZAJI MAZINGIRA

KAMPUNI ya PPM Group inahamasisha wananchi kuwa na matumizi ya nishati safi na kuachana na matumizi ya mkaa na kuni ili kunusuru misitu ambayo inaathiriwa na matumizi kama hayo.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya wiki ya Uwekezaji na Biashara Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya PMM Group Dk Judith Spendi amesema matumizi yanayopaswa kutumika kwa kupikia ni ya nishati safi.

Dk Spendi amesema kuwa Dar es Salaam na Pwani inatumia mkaa tani milioni 2.4 kwa mwaka hali ambayo ni hatari kwa misitu.

"Tunahamasisha matumizi ya majiko sanifu ambapo tutaanza uzalishaji wa majiko sanifu na upandaji miti ili kuepuka mabadiliko ya tabianchi,"amesema Dk Spendi.

Waziri wa Viwanda na Biashara Suleiman Jaffo aliipongeza kampuni ya PPM Group kwa jitihada zake za kukabiliana na uharibifu wa mazingira na kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia.