Monday, September 4, 2023

WAHAMIAJI HARAMU WAKAMATWA

 

JESHI la Polisi Mkoa wa Pwani limewakamata wahamiaji haramu watatu toka nchi mbalimbali kwa kuingia nchini bila ya kibali.
 
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na kaimu kamanda wa polisi mkoani Pwani ACP Muhudhwari Msuya imesema kuwa watuhumiwa hao wamekabidhiwa Uhamiaji kwa hatua za kisheria.

Msuya amesema kuwa watuhumiwa hao ni kutoka nchi za Ethiopia mmoja, Kenya mmoja na Uganda mmoja.

Amesema kwenye matukio mengine jeshi hilo limekamata jumla ya Pikipiki 111 za aina mbalimbali Haoujue 23, Boxer 30, Fekon 10, SanLg 16, Sinray 1, Kinglion, Senke 01, bajaji 4 na Tvs 23 mali zidhaniwazo kuwa za wizi na watuhumiwa 97 walikamatwa.

Pia kwenye matukio mengine jeshi limefanikiwa kukamata Bhangi viroba 7, Puli 60, Kete 791 na Mbegu za Bangi kilogramu 5, Mirungi Kilogramu 5, Bunda 3 za mirungi ambapo umla ya watuhumiwa 114 wamekamatwa katika makosa hayo.


POLISI PWANI WAKAMATA WATUHUMIWA NYAMA YA SWALA NA MAGAMBA 11 YA KAKAKUONA

JESHI la Polisi Mkoa wa Pwani kwa kushirikiana na askari wa wanyama pori limefanikiwa kukamata watubuhumiwa 14 wakiwa na nyama ya swala na magamba 11 ya mnyama Kakakuona.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoani humo ACP Muhudhwari Msuya amesema kuwa baadhi ya watuhumiwa walifikishwa mahakamani.

Msuya amesema kuwa kukamatwa watuhumiwa hao 14 ni mafanikio ya jeshi hilo ambapo kati ya hao watuhumiwa watatu wamefikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.

Amesema kuwa watu watatu wamehukumiwa vifungo tofuati kutokana na kukutwa na makosa ya ubakaji na ulawiti.

Amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Salim Issa ambaye amehukumiwa kifungo cha maisha baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kulawiti mwingine ni Albino Anthony amehukumiwa kifungo cha miaka 30 baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kubaka.

"Mazoea Salum amehukumiwa kifungo cha miaka 30 baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kubaka huku Hamisi Idd amehukumiwa kifungo cha miaka 20 baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kupatikana na nyara za Serikali,"amesema Msuya.

Aidha amesema kuwa Yusuph Athuman naye  amehukumiwa kifungo cha maisha baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kupatikana na nyara za Serikali.

"Katika kipindi cha mwezi Agosti jumla ya kesi zilizoshinda mahakamani zilikuwa 75 zikiwemo hizo za watuhumiwa ambao walihukumiwa jela maisha na wengine jela miaka 30 kwa kosa la kulawiti na kubaka watuhumiwa waliotiwa hatiani katika mahakama za Mkoa wa Pwani na kwenda jela kwa baadhi ya kesi,"amesema Msuya.

JUMUIYA YA WAFANYABIASHARA TANZANIA WATEMBELEA VIONGOZI NJOMBE

Picha ikiwaonesha Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania Abdalla Salim wakisalimiana na Katibu  wa Wafanyabiashara Makambako  Mkoani Njombe Edison Gadau Leo September 4,2023.

UONGOZI JUMUIYA YA WAFANYABIASHARA WAINGIA MKOANI NJOMBE

Picha ikimuonesha Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania Abdalla Salim akiwa anasaini Kitabu Cha  wageni Katika Ofisi ya Jumuiya ya Wafanyabiashara Makambako mkoani Njombe Leo September 4,2023.

MWENYEKITI JUMUIYA YA WAFANYABIASHARA TANZANIA AKUTANA NA UONGOZI MKOA WA NJOMBE

Picha ikimuonesha Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania Hamis Livembe akizungumza na Uongozi wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Makambako Mkoani Njombe kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Jumuiya Leo September 4, 2023.

MWENYEKITI (JWT) TAIFA MKOANI NJOMBE

Mwenyekiti wa Jumuiya ya wafanyabiashara Tanzania Hamis Livembe akiwa anasaini Kitabu Cha Wageni Katika Ofisi ya Jumuiya ya Wafanyabiashara Makambako Mkoani Njombe Leo September 4,2023.

MWENYEKITI JUMUIYA YA WAFANYABIASHARA TANZANIA ATUA MKOANI NJOMBE

Mwenyekiti wa Jumuiya Wafanyabiashara Tanzania  Hamis Livembe akiwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya wafanyabiashara Makambako Mkoani Njombe Sifaeli Msigala Leo September 4, 2023.