Tuesday, January 17, 2023

UJENZI TAASISI ZA SERIKALI UZINGATIE BAJETI

Na Wellu Mtaki Dodoma

SERIKALI kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu) imetoka wito kwa taasisi zote zinazoendelea na ujenzi Dodoma zihakikishe ujenzi huo unakamilika kwa kizingatia taratibu zote za ujenzi ikiwemo ubora, muda , bajeti iliyotengwa na thamani ya fedha Ili kuleta tija.

Wito huo umetolewa Jijini Dodoma na Mhe. George Simbachawene Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera , Bunge na Uratibu wakati wa hafla ya kukabidhi vibali vya ujenzi wa ofisi za taasisi Dodoma huku akiagiza taasisi nyingine ambazo bado hazijaaza maandalizi ya ujenzi Dodoma ziwasilishwe Ofisi ya Waziri Mkuu mahitaji ya viwanja vya ujenzi wa ofisi za taasisi Dodoma kwa ajili ya uratibu wa pamoja.

Simbachawene amesema kuwa serikali ya awamu ya sita imeendelea kutekeleza kikamilifu Mpango wa kuhamia Dodoma ambapo wananchi wanapata huduma zote katika makao makuu ya nchi na kwamba watumishi wote wa serikali ikiwemo wizara zote, vyombo vya ulizi na usalama, muhimili wa bunge na baadhi ya taasisi zimeamia Dodoma na wanaendelea kutekeleza majukumu yao.

Aidha amesema kuwa ifikapo march 2023 muhimili wa mahakama unatarajiwa kuhamia Jijini Dodoma kwani ujenzi wa jengo hilo umefika zaidi ya asilimia 90.

Pia ametoa rai kwa viongozi wa mkoa wa Dodoma, Wizara, Halmashauri, taasisi za serikali, sekta binafsi, wananchi na wadau wengine kuendelea kutoa ushirikiano katika utekelezaji wa Mpango wa serikali wa kuahamia Dodoma pamoja na ujenzi wa makao makuu Ili kufikia malengo ya kuwa na Jiji Bora la kuvutia litakalokidhi mahitaji ya kijamii na kiuchumi kwa miaka mingi ijayo.

Lengo la hafla hiyo ni kukabidhi vibali vya ujenzi kwa taasisi zilizopewa idhini ya ujenzi wa ofisi Jijini Dodoma kama sehemu ya kutambua mchango wa taasisi hizo katika kuunga mkono utekelezaji wa Mpango wa serikali kuhamisha shughuli zake Jijini Dodoma.

No comments:

Post a Comment