MJUMBE wa Halmashauri Kuu Chama Cha Mapinduzi Taifa (MNEC) Wazazi Hamoud Jumaa amewataka viongozi wa CCM kutumia mikutano ya hadhara iliyoruhusiwa na Rais Dk Samia Suluhu Hassan kueleza miradi ya maendeleo inayofanywa na kutekelezwa na Serikali ya awamu ya sita.
Akizungumza na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Kibaha Vijijini pamoja na baadhi ya viongozi na wanaCCM kusiwe na kigugumizi kukisemea Chama na kusimamia miradi mbalimbali inayotekelezwa.
Jumaa alisema kuwa Rais ametoa fursa nzuri kuruhusu mikutano ya hadhara kwa vyama vya siasa hivyo ni wakati sasa kwa viongozi na wanaccm kuelezea yale yaliyofanywa katika kuleta maendeleo ya wananchi.
"Viongozi wenzangu, madiwani,wabunge na wanaCCM tutoke kusemea Chama na kupanda majukwaani kuitendea haki ilani ambayo utekelezaji wake unafanya vizuri,"alisema Jumaa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Kibaha Vijijini Mkali Kanusu alisema kuwa watahakikisha wanasimamia utekelezaji wa miradi na watashirikiana na watendaji wa serikali ili kufanikisha miradi ya maendeleo kwa wananchi.
Naye Katibu wa CCM Safina Nchimbi alisema kuwa anamshukuru MNEC Taifa kuahidi kujenga ofisi ili ziendane na umri wa Chama na kinaendelea na mipango yake mbalimbali ya kimaendeleo na kuhakikisha chama kinakubalika kwa wananchi.
No comments:
Post a Comment