Na John Gagarini,
Kibaha
MKUU wa mkoa wa Pwani
Mhandisi Evarist Ndikilo amewataka wakuu wa wilaya mkoani humo kuhakikisha
wanakamilisha ujenzi wa maabara za sayansi kwenye kata ifikapo Machi mwaka huu.
Ndikilo alitoa agizo
hilo jana mjini Kibaha wakati wa kuwakaribisha wakuu hao wa wilaya ambao waliteuliwa na Rais
hivi karibuni na kusema kuwa wanapaswa kufanya jitihada madhubuti ili kufikia
malengo hayo.
Alisema kuwa mkoa huo
unatakiwa kujenga maabara 327 lakini zilizokamilika ni maabara 144 hivyo kuna
upungufu wa maabara 183 ili kukamilisha idadi hiyo inayotakiwa.
“Hizi maabara 183 ziko
kwenye hatua mbalimbali ili kukamilika kwake kwa hiyo kila mkuu wa wilaya
ahakikishe kuwa ujenzi wa maabara unakamilika ifikapo Machi ambapo anapaswa
kuwa amekamilisha,” alisema Ndikilo.
Aidha alisema kuwa ikifika
kipindi hicho kila mkuu wa wilaya ahakikishe anamkabidhi maabara hizo kufuatia
agizo la Rais la ujenzi huo ukamilike ifikapo Juni mwaka huu.
“Agizo la Rais hali jail
kuwa muda muda mfupi katika uongozi wenu kinachotakiwa ni maabara hizo
kukamilika kwa wakati uliopangwa hivyo hakutakuwa na kisingizio chochote cha
kushindwa kukamilisha ujenzi,” alisema Ndikilo.
Katika hatua nyingine
mkuu huyo wa mkoa wa Pwani alisema kuwa wakuu hao wanapaswa kuondoa urasimu
katika kuwapatia maeneo wawekezaji kwani fursa za uwekezaji ni nyingi sana.
Alisema wakuu hao
watenge maeneo kwa ajili ya uwekezaji baada ya Jiji la Dar es Salaam kujaa
hivyo fursa iliyopo ni kwa mkoa wa Pwani hivyo wanapaswa kuweka mazingira
mazuri ya uwekezaji.
Mwisho.
Moja ya kiongozi wa dini ambaye alihudhuria sherehe za kukaribishwa na kutambulishwa kwa wakuu wa wilaya wapya leo mjini Kibaha. |
No comments:
Post a Comment