TIMU za Umoja wa Michezo na Sanaa kwa Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA) na Umoja wa Michezo na Taaluma Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA) za Mkoa wa Pwani zimekabidhi makombe ilivyoshinda kwenye mashindano ambayo yaliyomalizika Mkoani Tabora hivi karibuni.
Monday, August 5, 2024
TIMU ZA UMISSETA NA UMITASHUMTA MKOA WA PWANI ZAKABIDHI VIKOMBE
TIMU za Umoja wa Michezo na Sanaa kwa Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA) na Umoja wa Michezo na Taaluma Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA) za Mkoa wa Pwani zimekabidhi makombe ilivyoshinda kwenye mashindano ambayo yaliyomalizika Mkoani Tabora hivi karibuni.
Sunday, August 4, 2024
YPC YAWATAKA VIJANA KUJITOKEZA KUWANIA NAFASI ZA UONGOZI
Thursday, August 1, 2024
DK BITEKO AMWAKILISHA RAIS MKUTANO MKUU (TLS)
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko leo Agosti 1, 2024 amemwakilisha Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Miaka 70 wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) unaofanyika Ukumbi wa Jakaya Kikwete, Jijini Dodoma.
Maadhimisho hayo yamehudhuriwa na Waziri wa Katiba na Sheria, Pindi Chana, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dkt. Eliezer Feleshi, pamoja na Wanachama wa Chama cha Wanasheria Tanganyika.
Itakumbukwa kuwa TLS ilianzishwa mnamo mwaka 1954 ikiwa na mawakili takribani 141 wakiwa ni wakoloni hadi ilipofika mnamo Oktoba 31,1961 ilipopata wakili wa kwanza Mtanganyika.
Hadi sasa TLS ina jumla ya mawakili takribani 12,471 wanaofanya kazi za usaidizi wa kisheria katika taasisi mbalimbali za kisheria nchini.
MH.RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AZINDUA TRENI YA KISASA (SGR)
Mhe.Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan azindua Rasmi Huduma za Usafiri wa Treni ya Kisasa (SGR) kutoka Dar es Salaam – Morogoro hadi Dodoma, katika eneo la Stesheni Jijini Dar es Salaam, leo 1 Agosti, 2024.
WAZIRI MKUU AFUNGUA MAONESHO YA WAKULIMA NANE NANE
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Agosti 01, 2024 afungua maonesho ya Kimataifa ya Wakulima ya Nanenane ambayo kitaifa yanafanyika kwenye viwanja vya Nanenane Nzuguni Jijini Dodoma,
Kauli mbiu ya Maonesho hayo ni Chagua Viongozi Bora wa Serikali za Mitaa kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi.
Saturday, July 27, 2024
RIZIWANI KIKWETE NDANI YA BARAZA LA MADIWANI UCHAGUZI MAKAMU MWENYEKITI HALMASHAURI YA CHALINZE
Nimeshiriki kikao cha Baraza la Madiwani Cha Chama Cha Mapinduzi kuchagua diwani atakayegombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze kilichofanyika Chalinze ,mapema leo.#KaziInaendelea
TAKUKURU DODOMA YATOA ELIMU KUELEKEA UCHAGUZI WA MITAA MWAKA HUU
Na Wellu Mtaki, Dodoma
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoani Dodoma imeendelea kutoa elimu kwa Umma kupitia makundi mbalimbali kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa nchini unaotarajia kufanyika mwaka huu.
Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoani Dodoma Euginius Hazinamwisho amesema kuwa viongozi wa Kisiasa nchini Tanzania hupatikana kupitia uchaguzi unaofanyika kila baada ya miaka mitano kwa namna mbili uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani na uchaguzi wa viongozi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa.
"Mwaka 2024 utafanyika uchaguzi wa Serikali za Mitaa na mwaka 2025 utafanyika uchaguzi wa Serikali kuu,"amesema.
Aidha amesema kuwa kuwepo kwa vitendo vya Rushwa wakati wa kuchagua viongozi huwanyima haki wagombea na kuwakosesha maendeleo wananchi
"Jitihada za Serikali kuhakikisha uchaguzi unakuwa huru na wa haki kwa wananchi wameweza kutunga Sheria mbalimbali zinazodhibiti vitendo vya Rushwa,"amesema
"TAKUKURU kwa kuzingatia kifungu cha 4 kifungu kidogo cha 2 na kifungu cha 7(d) vya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa vina wajibu wa kuwahakikishia wadau kuweka mikakati dhidi ya Rushwa wakati wa uchaguzi.
Hata hivyo amesema kuwa katika utekelezaji wa majukumu yake TAKUKURU mwaka 2014 na mwaka 2019 ilifanya uchambuzi wa ufuatiliaji wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa na mwaka 2020 ilifanya uchambuzi wa mfumo kwa uendeshaji wa uchaguzii mkuu wa Serikali wa Rais, Wabunge na Madiwani katika majimbo yote ya Uchaguzi Tanzania bara.
"Katika chaguzi zote yalikuwepo malalamiko ya vitendo vya Rushwa,katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa Mwaka 2014/2019 vitendo vya Rushwa vilijitokeza kama ifuatavyo kulikuwa na ugawaji wa fedha, ugawaji wa vitu, kama kanga,fulana,vinywaji na vyakula na ahadi za ajira,"amesema
Kwa upande wake Kamishna Msaidizi wa Mamlaka ya kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Mzee Kasuwi amesema kuwa athari za biashara ya Dawa za Kulevya kwenye uchaguzi wa Kisiasa zinaweza kuwa na madhara makubwa na kuathiri mchakato wa Kidemokrasia na utulivu wa jamii.
Aidha biashara na matumizi ya Dawa za Kulevya ni tatizo linaloathiri nchi nyingi dunia.
"Dawa za Kulevya zina athari Kiuchumi,kiafya, kijamii, Kisiasa, kidiplomasia, Kimazingira na usalama,"amesema