Na John
Gagarini, Kibaha
SHIRIKISHO
la Soka Nchini (TFF) limeombwa kuhamasisha uanzishwaji wa mashindano ya soka
kwa wanawake kwa ukanda wa Afrika Mashariki ili kuendeleza vipaji vya wanawake
kimataifa.
Hayo
yalisemwa mjini Kibaha na mratibu wa timu ya Mlandizi Queens Florence Ambonisye
wakati wa sherehe za kuipongeza timu hiyo kwa kutwaa ubingwa huo na kuwa
mabingwa wa kihistoria wa kwanza kwa soka la Wanawake Tanzania.
Ambonisye
alisema kuwa kwa kuwa kuna mashindano ya soka la wanawake ngazi ya nchi na nchi
kuna haja ya kuwa na mashindano ya vilabu kama ilivyo kwa wanaume.
“Imefika
wakati TFF kuhamasisha kuanzishwa mashindano ya vilabu vya soka la wanawake ili
kuinua soka la wanawake hapa nchini kwani itasaidia kuwa na timu bora kutokana
na kushindana na wenzao wa nchi zingine,” alisema Ambonisye.
Ambonisye
ambaye pia ni katibu wa chama cha soka la wanawake mkoa wa Pwani alisema kuwa
mashindano hayo pia yatasaidia kuimarisha timu ya soka ya Taifa ya wanawake
Twiga Stars.
“Tukianzisha
mashindano ya nchi za Afrika Mashariki tutakuwa na timu ya Taifa ya wanawake
imara kwani watapata uzoefu mkubwa hivyo nchi itaweza kufika mbali kwenye
mashindano ya Kimataifa,” alisema Ambonisye.
Aidha
alisema kuwa washindi wa mashindano hayo watakuwa hawana mashindano yoyote hadi
mwakani lakini wangekuwa na mashindano ya vilabu vya nchi nyingine ingewasaidia
sana kuendeleza vipaji vyao ambapo kwa sasa watakaa muda mrefu bila ya kucheza.
Naye
mgeni rasmi kwenye sherehe hizo Ivan Chenga ambaye ni katibu msaidizi wa chama
cha soka wilayani Kibaha Ivan Chenga alisema kuwa timu hiyo haitakiwi kubweteka
kwa kutwaa ubingwa huo.
Chenga
alisema kuwa katika kipindi hichi wanapaswa kuendelea na mazoezi na kuachana na
vitendo ambavyo vitasababisha kushusha viwango vyao.
Kwa
upande wake mwakilishi wa chama cha soka mkoa wa Pwani COREFA Simon Mbelwa
alisema kuwa timu hiyo imeleta mafanikio makubwa kwa kuweka historia kwa kuitoa
Pwani kimasomaso kwa kutwaa ubingwa huo.
Mbelwa
alisema kuwa timu za soka za wanaume za mkoa wa Pwani zimekuwa zikifanya vizuri
kwenye ligi Kuu lakini hazijawahi kutwaa ubingwa lakini hii ya wanawake imeweza
kuleta kombe na kuonyesha mfano mzuri.
Mwisho.
Baadhi ya wachezaji wa timu ya Mlandizi Queens wakiwa wamepozi wakati wa sherehe za kuwapongeza baada ya kufanikiwa kuwa mabingwa wa soka la wananwake nchini. |
Baadhi ya viongozi wa timu ya Mlandizi Queens wakiwa wametulia wakifuatilia wakati wa sherehe za kuipongeza timu hiyo kwa kutwaa ubingwa wa soka la wanawake nchini hivi karibuni. |
Wachezaji wa timu ya Mlandizi Queens wakicheza wakati wa sherehe ya kuwapongeza kwa kuwa mabingwa wa soka la wanawake nchini. |
Wachezaji wa Mlandizi Queens wakicheza. |
Wachezaji wa Mlandizi Queens wakicheza pamoja na viongozi wao wakati wa sherehe ya kuwapongeza iliyofanyika Mlandizi hivi karibuni. |
Katibu Msaidizi wa Chama cha soka wilaya ya Kibaha Ivan Chenga akipokea kombe toka kwa kepteni wa Mlandizi Queens Mwanahamis Gaucho katikati ni diwani wa kata ya Mlandizi Ephrasia Kadala akishuhudia. |
Katibu Msaidizi wa Chama cha soka wilaya ya Kibaha KIBAFA Ivan Chenga akiongea wakati wa sherehe ya kuipongeza timu ya Mlandizi Queens kwa kuwa mabingwa wa soka la wanawake nchini |