Na John
Gagarini, Kibaha
WANACHAMA
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Kibaha Mjini wametakiwa kuacha tabia ya
kukumbatia makundi mara baada ya uchaguzi wa ndani kumalizika kwani
yanasababisha chama kushinda kwa tochi.
Hayo
yalisemwa juzi na mwenyekiti wa CCM Kibaha Mjini Maulid Bundala wakati
akiwanadi watia nia waliojitokeza kuwania kuchaguliwa na chama hicho
kupeperusha bendera kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba
mwaka huu.
Bundala
alisema kuwa makundi hayo yanachangia kwa kiasi kikubwa chama kushindwa kutokana
na mshikamano na ushirikiano kutokuwepo kwenye chaguzi mbalimbali ambazo
zinahusisha vyama vingi vya siasa.
“Kipindi
hichi ni kigumu sana kuwa na kundi siyo tatizo lakini mara atakapopatikana
mgombea mmoja wa ubunge makundi yanatakiwa kwisha na kubakia kundi moja tu la
CCM ambalo linatakiwa lipambane na wapinzani,” alisema Bundala.
Alisema
kuwa kwanini chama kishindwe kwa mbinde kwa ushindi wa tochi wakati kina wanachama
wengi ukilinganisha na vyama vya upinzani lakini inaonekana kushindwa
kunatokana na kukumbatiwa kwa makundi hayo.
“Makundi
yanatakiwa yaishe mara uteuzi wa mwanachama mmoja ambaye atawakilisha chama
kwenye uchaguzi tatizo linguine ni wanachama kumpenda mtu badala ya kukipenda
chama na kuachana na tabia ya kuwasema vibaya wagombea kwani wote ni Wanaccm,”
alisema Bundala.
Aliwataka
wanaccm ambao wanasifa ya kupiga kura za maoni za kuchagua mbunge kwenye kura
za maoni wanapaswa kuwa hai kwa kulipia kadi za chama, wawe wameorodheshwa
kwenye daftari la tawi na wawe na kadi ya kupigia kura.
Mwisho.
Na John Gagarini, Kibaha
WATIANIA
wanne wa Jimbo la Kibaha Mjini wilayani Kibaha mkoani Pwani kupitia Chama Cha
Mapinduzi (CCM) wameendelea kumwaga sera zao kwa wanachama ili waweze kupata
fursa ya kuchaguliwa na chama hicho kwa kupigiwa kura za maoni kupata mgombea
mmoja zinazotarajiwa kufanyika Agosti Mosi mwaka huu.
Wagombea
hao ambao ni Silvestry Koka ambaye anatetea kiti chake Rugemalila Rutatina, Idd
Majuto, Abdala Bagdela na Abdulaziz Jab
wakiwa kwenye kata ya Kibaha na Kongowe wote kila mmoja alijinadi kwa staili ya
aina yake ikiwa ni njia ya kuomba kuchaguliwa kwenye kura za maoni ili
kukiwakilisha chama hicho kwenye nafasi ya Ubunge wa Jimbo hilo.
Kwa
upande wake Mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa NEC CCM, Rugemalila Rutatina
alisema kuwa ilani ya chama ni nzuri sana lakini tatizo ni kwamba wasimamiaji
ndiyo chanzo cha kushindwa kufikiwa kwa maendeleo.
Rutatina
alisema kuwa endapo atachaguliwa athakikisha anaisimamia ilani ya chama ambayo
ina majibu ya changamoto zote zinazowakabili wananchi na atakuwa kiongozi na si
mtawala na kuwa ubunge ni ajira huku wananchi wakiwa ndiyo waajiri wa wabunge.
Silvestry
Koka alisema kuwa katika uongozi wake amefanya mambo makubwa ikiwa ni pamoja na
kukabiliana na changamoto ya maji ambapo ameweza kuhakikisha maji yanapatikana
mitaa 14 ambapo kwa sasa kuna mradi mkubwa ambao utafanya Jimbo hilo kutokuwa
na tatizo la maji.
Alisema
anaomba achaguliwe tena ili aweze kukamilisha mipango iliyobaki kwani anauwezo
wa kuongoza na kufanikisha maendeleo ya Jimbo hilo ambalo kwa sasa liko kwenye
mchakato wa kuwa manispaa.
Abdulaziz
Jaab alisema kuwa endapo atachaguliwa kwenye nafasi hiyo ya Ubunge kupitia CCM
yeye atasimamia maendeleo endelevu na si uongozi wa nadharia ya kuongoza kwa
msimu kama baadhi ya viongozi wanavyofanya.
Jab
alisema kuwa kwa kushirikiana na wananchi atahakikisha anawashirikisha wananchi
kwenye suala zima la maendeleo na si kujikita zaidi kwa vipindi huku muda
mwingi wanachi wakiwa hawafikiwi hadi msimu wa uchaguzi.
Idd
majuto yeye alisema kuwa wanCCM wanatakiwa kuacha kuchagua viongozi ambao
wanatumia rushwa kupata uongozi kwani wanachangia kuzorotesha maendeleo ya
wananchi kwani wanawanunua wananchi kama nyanya.
Alisema
kama mgombea anatoa rushwa wao wale lakini wakati wa kuchagua waangalie nani
anayefaa kuwa kiongozi na kuacha kuchagua viongozi wanaofanya rushwa kama
kigezo cha kuwa kiongozi kwani hawafai.
Abdala
Bagdela alisema kuwa endapo atachaguliwa atahakikisha kila mwananchi anamiliki
nyumba ili aweze kuishi kwenye makazi bora huku fedha za ujenzi zikitokana na
vyama vya kuweka na kukopa VICOBA.
Alisema
kuwa atahakikisha anaweka mazingira mazuri kwa wajasiriamali wadogo kwa
kuwaondolea kero za sheria zinazowabana ili waweze kufanya kazi zao bila ya
usumbufu wanaoupata lengo wafanikiwe kujikwamua na hali ngumu.
Mwisho.
Na
John Gagarini, Mufindi
WATIA
nia watatu wamejitokeza kupambana na Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kaskazini
ambaye ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mahmoud Mgimwa ambaye anattetea
kiti chake kwenye Jimbo hilo ambalo limeganywa na kutoka Jimbo lingine la
Mafinga Mjini .
Katibu
wa CCM Jimson Mhagama alisema kuwa kwa sasa watia nia wote wanapitishwa kwa
wanachama ili waeleze sera zao kwa wanachama ambao watawapigia kura za maoni
zinazotarajiwa kufanyika Agosti Mosi mwaka huu ili kupata Mbunge atakayepambana
na vyama vya upinzani.
Mhagama
aliwataja wagombea wengine kuwa ni Dk Godfrey Kalinga, Godfrey Ngupula na Exaud
Kigahe ambao kwa sasa wako kwenye zoezi la kunadi sera zao kwa wanachama ili
wawachague mmoja aweze kupeperusha bendera
ya chama.
Kwa upande
wa Jimbo la Mafinga Mjini ambalo limemegwa kutoka Jimbo la Mufindi Kaskazini
jumla ya wagombea watano watachuana kwenye kinyanganyiro hicho ambao ni Zuber
Ngullo, Cosato Chumi, Paul Myinga, Benjamin Balali, James Mgimwa.
Aidha
alisema kuwa Jimbo la Mufindi Kusini jumla ya watia nia 15 wamejitokeza kuwania
nafasi hiyo ambao ni Dickson Lutevele, Mary Miho, Golden Ally, Dionis Myinga,
Frank Mng’olage, Dk Prosper Mfilinge, Anton Mpiluka, Charles Sanga, Menrad
Kigola, Wende Ngahala, Faustin Mhapa, Marcelin Mkini, Dk Alex Sanga, Albert
Chalamila na Robert Malangalila.
Mhagama
alisema kuwa wagombea wote ni wa CCM na wana sifa za kuwa wabunge kinachotakiwa
ni wanachama kuchagua mmoja ambaye wataona anafa
Na John
Gagarini, Bagamoyo
WAJUMBE wa
mkutano mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania kupitia Chama Cha
Mapinduzi (UWT) Wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani wamechagua madiwani wake wa
viti maalumu baada ya kufanyika kwa uchaguzi wa nafasi hiyo.
Kwenye uchaguzi huo ulihudhuriwa na wajumbe
wapiga kura 958 kutoka Tarafa saba zilizomo katika wilaya hiyo,uchaguzi ambao
ulisimamiwa na Pilli Augostino ,aliyesaidiwa na Husna Ally huku mwenyekiti wa
Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya Almasi Masukuzi na katibu wake Kamote Kombo
wakifuatilia mchakato mzima.
Katika kinyang’anyiro hicho kilikuwa na jumla ya wagombea 22 waliojitokeza kuwania nafasi hiyo kutokea kwenye Tarafa saba zilizomo wilayani humo ambazo ni Msoga, Chalinze, Msata, Miono, Kwaruhombo, Mwambao na Yombo.
Pilli alisema
kutoka Tarafa ya Chalinze kura za washindi katika mabano ni Mwanakesi Madega
(555) dhidi ya Nuru Mhami (78), Tarafa ya Kwaruhombo Asha Mtunye (35), Tatu Mpongo
(443) na Tunu Mpwimbwi (476). Tarafa ya Msoga Zaituni Kawogo (57), Matha Patel
(400) na Maria Moreto (426).
Tarafa ya
Msata Sophia Issa (89), Anzeni Rajabu (294), Rehema Mno (484). Tarafa ya Miono
Tukae Kilo (321), Sijali Mpwimbwi (612). Tarafa ya Mwambao Nuru Abdallah (5),
Leonia Fransic (11), Shumina Sharifu (172) Sinasud Onelo (199) Hapsa Kilingo
(563). Tarafa ya Yombo Togo Omary (205), Nuru Mohamed (260)na Elizabeth Shija
(458).
Katika mchakato huo ngazi ya kapu Togola alipata (81), Sinasud (175), Sophia (118), Zaituni (31), Tukae (103), Leonia (140), Magazin (210), Shumina (308), Tatu (274), Nuru Mohamed (18), Asha (5), Nuru (4), Mhami (49), Matha (289), Anzeni (45). Hivyo Shumina Sharifu na Martha Patel.
Baada ya
kutangaza matokeo hayo,Pilli aliwataka madiwani hao kwenda kufanyakazi ili
kuhakikisha wagombea wote wanaotokea ndani ya CCM wanashinda kwa kishindo kwani
kinyume chake ushindi huo ni kazi bure.
Mwisho.
Na John Gagarini, Kibaha
WANACHAMA
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Kibaha Mjini wametakiwa kuacha tabia ya
kukumbatia makundi mara baada ya uchaguzi wa ndani kumalizika kwani
yanasababisha chama kushinda kwa tochi.
Hayo
yalisemwa juzi na mwenyekiti wa CCM Kibaha Mjini Maulid Bundala wakati
akiwanadi watia nia waliojitokeza kuwania kuchaguliwa na chama hicho
kupeperusha bendera kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba
mwaka huu.
Bundala
alisema kuwa makundi hayo yanachangia kwa kiasi kikubwa chama kushindwa kutokana
na mshikamano na ushirikiano kutokuwepo kwenye chaguzi mbalimbali ambazo
zinahusisha vyama vingi vya siasa.
“Kipindi
hichi ni kigumu sana kuwa na kundi siyo tatizo lakini mara atakapopatikana
mgombea mmoja wa ubunge makundi yanatakiwa kwisha na kubakia kundi moja tu la
CCM ambalo linatakiwa lipambane na wapinzani,” alisema Bundala.
Alisema
kuwa kwanini chama kishinde kwa mbinde kwa ushindi wa tochi wakati kina wanachama
wengi ukilinganisha na vyama vya upinzani lakini inaonekana kushindwa
kunatokana na kukumbatiwa kwa makundi hayo.
“Makundi
yanatakiwa yaishe mara uteuzi wa mwanachama mmoja ambaye atawakilisha chama
kwenye uchaguzi tatizo linguine ni wanachama kumpenda mtu badala ya kukipenda
chama na kuachana na tabia ya kuwasema vibaya wagombea kwani wote ni Wanaccm,”
alisema Bundala.
Aliwataka
wanaccm ambao wanasifa ya kupiga kura za maoni za kuchagua mbunge kwenye kura
za maoni wanapaswa kuwa hai kwa kulipia kadi za chama, wawe wameorodheshwa
kwenye daftari la tawi na wawe na kadi ya kupigia kura.
Mwisho.