Sunday, September 8, 2013

MWANAFUNZI ABAKWA NA WENZAKE

Na John Gagarini, Kibaha
MATUKIO ya uvunjifu wa maadili kwenye shule mbalimbali hap nchini yameendelea kuharibika baada ya wanafunzi wanne wa shule ya Msingi Lulanzi wilayani Kibaha mkoani Pwani kutuhumiwa kubaka mwanafunzi wa darasa la pili (9) na kumsababishia maumivu yalipelekea kulazwa hospitali ya Tumbi kwa matibabu.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi jana babu wa mtoto huyo (jina tunalo), Jacob Mrope alisema tukio hilo lilitokea Septemba 2 majira ya saa 6 mchana,  ambapo mjukuu wake ambaye ni yatima, alikuwa akitoka shuleni huku akiwa na wenzake wawili wakike walikimbizwa na watuhumiwa hao ambapo yeye alishindwa kukimbia kutokana na kuuumia mguu na kujikuta akikumbana na dhahma hiyo.
Mrope alisema kuwa wanafunzi wenzake aliokuwa nao walisema kuwa baada ya watuhumiwa hao kumkamata walimziba mdomo kisha wakaanza kumuingilia kwa zamu ambapo mwanafunzi huyo hakuweza kupata msaada wowote hadi watuhumiwa hao kutimiza haja zao.
“Wenzake waliokuwa nao walitoa taarifa nyumbani kwa mlezi wake ambaye ni dada yake ambapo alikwenda na kumkuta akitokwa na damu nyingi na alipomuuliza alisema kuwa wenzake wamembaka na kumchukua na kumpeleka shuleni na kutoa taarifa,” alisema Mrope.
Kwa upande wake dada yake Lwiza alisema kuwa yeye alipata taarifa kupitia kwa wanafunzi hao ambao walikuwa nao wakati wanatoka shule na kukimbizwa na watuhumiwa hao, ambapo walisema kuwa ilibidi warudi na kumkuta mwenzao akitokwa damu na kumkokota mwenzao hadi nyumba iliyojirani na kumjulisha.
“Alikuwa kwenye hali mbaya kwani alikuwa akitokwa na damu nyingi na nilipomuuliza alisema kuwa amebakwa na mtuhumiwa ambaye alimtambua na kumtaja jina mwenye umri wa miaka 10 akiwa na wenzake watatu,” alisema Lwiza.
Lwiza alisema kuwa baada ya kuona hali ile walimpeleka shule na uongozi wa shule ukamwelekeza kufuata taratibu za kisheria ambapo walikwenda serikali ya mtaa kasha kwenda polisi na baadaye hospitali ya Tumbi kwa matibabu zaidi ambapo hadi juzi mwanafunzi huyo alikuwa bado kalazwa na hali yake inasemekena kuwa ni mbaya.
Naye mwalimu mkuu wa shule hiyo ya Lulanzi Anna Bilali alisema kuwa wao kama uongozi wa shule hawawezi kusema lolote kwani sula hilo liko kwenye vyombo vya sheria pamoja na kitabibu na watakuwa tayari kusema mara taarifa zitakapokamilika.
“Ni kweli tukio hili limetokea lakini bado haijathibitishwa kama ni kweli au la na pia lilitokea nje ya shule na muda wa shule kwa wanafunzi wa madarasa ya chini walisharuhusiwa kurudi nyumbani mara baada ya masomo kwisha,” alisema Bilali.
Akizungumzia tukio hilo mjumbe wa mtaa wa Lulanzi Rasul Shaban alisema kuwa walipata taarifa hiyo na kushnagazwa na kitendo hicho ambapo tukio hilo ni la mara ya kwanza kutokea katika shule hiyo ambayo iko kwenye mtaa huo na pia walitoa barua za kuwadhamini wanafunzi wanaotuhumiwa kufanya tukio hilo.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoani Pwani Ulrich Matei alisema kuwa hadi sasa wanawashikilia wanafunzi wanne wenye umri kati ya miaka 10 na 13 kuhusiana na tukio hilo.
“Wanafunzi hao wanatuhumiwa kumbaka mwenzao wakati akitoka shule ambapo walimkamata na kumkimbiza kwenye kichaka na kumziba mdomo ili asiweze kupiga kelele kisha walimshika miguu na mikono na kumbaka kwa zamu  na kumsababishia maumivu makali ambapo amelazwa hospitali ya Tumbi kwa matibabu zaidi na hali yake bado haijawa nzuri,” alisema Matei.
Matei alisema kuwa watuhumiwa hao wanne wanahojiwa juu ya tukio hilo ambapo watafikishwa mahakamani mara upelelezi utakapokamilika ikiwa ni pamoja na uchunguzi wa daktari kuhusina na tukio hilo lakusikitisha.
Mwisho.

VIZIWI NA MAJI

Na John Gagarini, Kibaha
VIZIWI mkoani Pwani wamependekeza kwenye katiba ijayo iwe na kipengele cha matumizi ya lugha ya alama kwenye maeneo ya umma ili kurahisisha utoaji huduma kwa watu wote.
Hayo yalisemwa na katibu wa klabu ya Michezo ya Viziwi mkoani Pwani (PDSC), Daud Kulangwa wakati akitoa ripoti ya utekelezaji wa mradi wa kuwawezesha watu wenye ulemavu kujadili rasimu ya katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, baada ya baraza la katiba lililofanyika Mlandizi wilayani Kibaha.
Kulangwa alisema kuwa kwa katiba iliyopo inasema tu kuweka mazingira ya matumizi ya lugha ya alama ambayo utekelezaji wake kwani sehemu za umma na sekta binafsi  matumizi ya lugha hiyo hayapo kwa sasa.
“Tunataka kwanza kuwe na mafunzo ya lugha ya alama na nukta nundu kama ilivyo masomo mengine mashuleni na kwenye vyuo kwa watumishi wa umma na kila raia wa Tanzania awe anaijua lugha hiyo ambapo wafanyakazi wa umma wataweza kuwasiliana na watu wenye ulemavu kama wafanyavyo ndani ya ndege,” alisema Kulangwa.
Alisema kuwa kwa sasa watu wenye ulemavu wakiwemo viziwi wasioona wanapata tabu sana wanapokwenda kwenye sehemu za kupata huduma kama vile mahakamani, polisi, hospitali, maofisini, mahali pa kuabudia na sehemu nyingine hivyo kushindw akupata huduma stahili.
“Kama unavyojua ukienda sehemu za huduma unashindwa kuhudumiwa kwani wahusika hawajui kumwelekeza mteja kwa usahihi kutokana na mawasailiano kuwa magumu hivyo kushindwa kupata kile kinachostahili,” alisema Kulangwa.
Aidha alisema kuwa kwenye kipengele cha lugha ya Taifa ni Kiswahili pia kuwe na nyongeza ya lugha ya alama ili iwe kisheria na endapo mtu atashindwa kutekeleza iwe ni kosa kisheria.
“Uwepo wa lugha ya alama na nukta nundu utasaidia mawasiliano kwa watu wote hasa kwenye shughuli za serikali na watu watu wenye ulemavu watapata taarifa kwani kwa sasa upatajia wa taarifa ni mdogo sana kutokana na matumizi ya lugha ya alama kutopewa kipaumbele,” alisema Kulangwa.
Aliongeza kuwa juu ya haki za watu wenye ulemavu zitajwe na aina, kuwezeshwa na serikali vifaa maalumu vya kujipatia elimu, vyombo vya usafiri, kupata hifadhi ya jamii kwa watu wenye ulemavu na kuw ana chombo cha kuwaunganisha na kuwatetea kuanzia ngazi ya kata hadi Taifa. Mabaraza hayo yaliwashirikisha wajumbe zaidi ya 100 na yalifadhiliwa na The Foundation for Civil Society (FCS).
Mwisho.
Na John Gagarini, Kibaha
WAKAZI 5,720 wa mtaa wa Mwanalugali wilayani Kibaha mkoani Pwani watanufaika na mradi wa maji safi na salama ya bomba wenye thamani ya shilingi milioni 210,768,135 baada ya mradi wa maji kwenye mtaa huo kukamilika na kuanza kutoa maji.
Mradi huo ambao ulizinduliwa na kiongozi wa mbio za mwenge hivi karibuni Juma Simai ulianza rasmi mwaka 2009 kwa kufanywa utafiti wa upatikanaji wa huduma ya maji ya ardhini na kukamilika Januari mwaka huu.
Mwenyekiti wa kamati ya maji wa mtaa huo Godfrey Mwandenga alisema kuwa mradi huo uliibuliwa na wakazi wa mtaa huo kupitia mpango shirikishi na kuwa kipaumbele cha kwanza cha jamii.
“Tumepata kisima kirefu cha mita 110 chenye kutoa maji ujazo wa lita 15,00 kwa saa na mradi huu utawawezesha wananchi wa mtaa wetu wa Mwanalugali sawa na asilimia 64 watapata maji safi na salama karibu na maeneo wanayoishi kama ilivyoainishwa kwenye sera ya maji ya Taifa ya mwaka 2002,” alisema Mwandenga.
Alisema kuwa kati ya fedha zilizofanikisha mradi huo kiasi cha shilingi milioni 207,168,135 ni fedha kutoka serikali kuu na shilingi milioni 3,600,000 ni michango ya jamii.
“Mradi huu umepunguza adha kwa akinamama kufuata maji mbali na makazi yao hivyo kutumia muda huo katika shughuli mbalimbali za kiuchumi na mradi huu unasimamiwa na uongozi wa jumuiya ya watumiaji maji wa mtaa wa Mwanalugali.
Aidha alisema kuwa wanajumuiya hao huwajibika kukusanya mauzo ya maji, kulipia matumizi ya umeme, kufanya usafi wa mazingira, kukarabati pamoja na kupanua huduma kwa maeneo yasiyofikiwa na huduma hii.
Mwisho.

Monday, August 26, 2013

MWANALUGALI WATWAA UBINGWA



Na John Gagarini, Kibaha
TIMU ya soka ya Mwanalugali imenyakua ubingwa wa Micho Cup baada ya kuifunga timu ya Bamba zote za wilayani Kibaha mkoani Pwani kwa magoli 2-1.
Mchezo huo ilipigwa kwenye uwanja wa Kwa Mbonde wilayani Kibaha ulikuwa mkali na wa kusisimua muda wote na kuwafanya mashabiki waliojazana uwanjani hapo kushindwa kukaa kwenye viti vyao.
Washindi walianza kupata bao la kuongoza dakika ya nane ya mchezo kupitia kwa Makida Makida baada ya gonga za hapa na pale na kuwainua mashabiki wake.
Huku Bamba wakiwa hawajajiweka sawa walishtukia wakipachikwa bao la pili kupitia kwa Laurence Mugia dakika ya 13, hata hivyo Bamba walifanikiwa kupata bao la kufuta machozi dakika ya 44 ya mchezo.
Naye wandaaji wa mashindano hayo Athuman Shija alisema kuwa jumla ya timu 14 zilishiriki mashindano hayo ambayo yalikuwa na lengo la kuhamasisha michezo kwenye wilaya hiyo.
Kwa upande wake meneja wa kampuni ya 3 J’s ambao ndiyo wadhamini wa mashindano hayo Samwel Mwegoha alisema kuwa wataendelea kudhamini michezo ili vijana waweze kupata ajira kupitia michezo.   
Kufuatia ushindi huo wa Mwanalugali washindi walipata zawadi za jezi seti mbili, mipira miwili na mipira miwili, Bamba walipata mipira miwili  na fedha taslimu kiasi cha shilingi 150,000.
Mwisho.

Tuesday, August 20, 2013

MAJAMBAZI YAVAMIA KWA DAVIS MOSHA YAPORA




Na John Gagarini, Kibaha

WATU 10 wanaozaniwa kuwa ni majambazi wakiwa na silaha za jadi kama marungu na mapanga wamevamia kituo cha mafuta cha Delina mali ya Davis Mosha na kufanikiwa kupora vitu  mbalimbali ambavyo thamani yake bado haijaweza kufahamika mara moja.

Akithibitisha kutokea tukio hilo kamanda wa Polisi mkoa Pwani  Ulrich Matei alisema tukio hilo lilitokea usiku saa saba Agosti 19 eneo la Picha ya Ndege wilayani Kibaha mkoani humo.

Matei alisema kuwa watu hao walifika kituoni hapo wakiwa na gari mbili moja  aina ya Prado na nyingine aina ya Saloon rangi nyeupe walizoegesha karibu na pampu za kuwekea mafuta.

“Baada ya hapo walimkamata mfanyakazi wa zamu  aitwaye Samsoni Rufunga na mlinzi wa kituo hicho Mohamed Shaban na kuwafunga  kamba  za miguu na mikono na kuwafungia ndani ya chumba kimoja kilichopo katika kituo hicho na kupora fedha hizo ambazo bado hazijafahamika,” alisema Matei.

Aidha alisema kuwa majambazi hao yalimkamata Frank Nyamahaga ambaye ni dereva mkazi wa Tabata nakumpora laki moja ,simu mbili za laki mbili na funguo za gari lake aina ya scania lililokuwa limeegeshwa kituoni hapo.

“Watu hao walimkamata Isack Silinu  ambaye alikuwa utingo wa scania hiyo ambaye naye aliporwa simu aina ya Itel yeny thamani ya sh.38,000, wakati Shabani Ramadhani aliporwa simu aina ya nokia yenye thamani ya sh. 45,000, Issa Mohamed aliyeporwa
simu aina ya nokia yenye thamani ya sh.75,000 na pesa taslimu sh.68,000  na wote walikuwa  wakisafiri katika lori aina ya scania
likitokea Iringa kuelekea Dar,” alisema Matei.

Aliongeza kuwa kama haitoshi watu hao walimpora Juma Seleman wa Mwanalugali, pikipiki aina ya Sanlg na fedha kiasi cha shilingi 46,000 alipokwenda kituoni hapo kwa ajili ya kununua mafuta.

Alibainisha kuwa katika tukio hilo hakuna mtu aliyejeruhiwa katika tukio hilo na jeshi hilo linaendelea na jitihada za kuwasaka majambazi hao ili waweze kutiwa nguvuni.
Mwisho.

Thursday, August 15, 2013

KIFAA KIPYA KUDHIBITI MADEREVA WAENDAO MWENDO KASI CHAINGIA NCHINI

Na John Gagarini, Kibaha

JESHI la polisi nchini limeanza mradi wa majaribio wa matumizi ya kifaa cha kisasa cha kuangalia mwenendo wa magari yanayokwenda mwendo kasi ili kupunguza ajali.

Akizungumza na waandishi wa habari jana wakati wakifanya majaribio ya vifaa hivyo kwenye barabara ya morogoro, kamanda wa kikosi cha usalama barabarani mkoani Pwani Nasoro Sisiwaya   alisema kuwa vifaa hivyo vimeanza kufanya majario mkoani humo kwa majaribio.

Sisiwaya alisema kuwa vifaa hivyo ni vya kisasa kwani vitafungwa sehemu ya juu na kuyaona magari tofauti na vile vya awali ambavyo hushikwa mkononi na vilikuwa havina taarifa za kutosha hasa wakati wa kuthibitisha kosa .

“Kifaa hichi kina uwezo wa kutoa taarifa za gari ambalo limeonekana kwenda kwa mwendo kasi  kwani kinauwezo wa kuonyesha kasi ya gari, muda na namba za gari husika, tofauti na kile cha zamani ambacho kinaonyesha mwendo kasi pekee ambapo dereva ana uwezo wa kukana kwani hakuna ushahidi wa kutosha,” alisema Sisiwaya.   

Naye mwakilishi wa kikosi cha usalama barabarani nchini Notker Kilewa, alisema kuwa kifaa hichi cha kisasa na kinauwezo wa kufungwa sehemu ambayo kitaona magari na mienendo yao na kulitambua gari lenye mwendo kasi kinyume cha sheria.

Kwa upande wake mwakilishi wa kampuni ya TMT ya Afrika Kusini, hapa nchini Twaha Ngambi ambayo inasambaza vifaa hivyo alisema kuwa kifaa hicho kitasaidia kukabiliana na madereva wanaokwenda mwendo wa kasi pamoja na makosa mengine ya barabarani.

Ngambi alisema kuwa kifaa hicho kitakuwa na uwezo wa kuona umbali wa mita 200 toka kilipofungwa hivyo itaondoa usumbufu wa kulisimamisha ghafla gari ambalo linabainika kuwa kwenye mwendo wa kasi.

Mwisho.



 Moja ya wataalamu toka Afrika Kusini kupitia kampuni ya TMT akiunganisha mitambo wakati wa wakifanya majaribio ya namna ya kutumia kifaa hicho ambacho kitakuwa na uwezo wa kuona magari ambayo yanakwenda kwa mwendo kasi kinyume na sheria za usalama barabarani, huko Mlandizi wilayani Kibaha mkoani Pwani.
 

YATIMA WTENGEWE ENEO

Na John Gagarini, Bagamoyo

KATA ya Miono wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani imetakiwa kutenga eneo kwa ajili ya kufanya shughuli za watoto yatima na wale waishio kwenye mazingira magumu.

Akizungumza jana kwenye kata hiyo wakati wa kuzindua mfuko wa kusaidia watoto yatima na wale wanaoishi kwenye mazingira magumu Meya wa mji mdogo wa Bagamoyo Abdul Sharifu alisema lazima viongozi wa vijiji wanapaswa kutenga maeneo kwa ajili ya kundi hilo.

Sharifu alisema kuwa kundi hilo limekuwa halitendewi haki hasa zinapotokea fursa mbalimbali kutokana na baadhi ya viongozi kutoona umuhimu wa watoto hao na kuwaona kama hawastahili kwenye jamii.

“Watoto yatima na wale waishio kwenye mazingira magumu ni sawa na watoto wengine na wanastahili kuwekewa mazingira mazuri ili waweze kuishi na kupata huduma muhimu za kijami hivyo ni vema mkawatengea eneo lao kwa ajili ya kufanyia shughuli zao,” alisema Sharifu.

Alisema kuwa katika eneo hilo watakuwa wakilitumia kwa ajili ya mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kusoma, michezo, kujifunza ufundi na masuala mengine kwa ajili ya watoto.

“Mimi mwenyewe nilikuwa yatima baada ya kufiwa na wazazi wangu ndiyo sababu nimeguswa na jambo hili la kuanzisha mfuko kwa ajili ya kuwasaidia kwani najua taabu wanazozipata na sisi ndiyo wa kuwasemea na kuwasaidia,” alisema Sharifu.

Kwa upande wake moja ya watoto yatima Yusuph Ally alisema kuwa jambo alilolifanya meya ni la kuigwa na viongozi wengine pamoja na jamii inayowazunguka.

Katika uzinduzi huo Meya huyo alichangia kiasi cha shilingi 500,000 kwa ajili ya mfuko huo na kuahidi kutoa shilingi milioni 2 mara ufunguaji wa akaunti utakapokamilika, jumla ya watoto zaidi 200 walihudhuria.    

Mwisho.

 
Meya wa mji wa Bagamoyo mkoani Pwani Abdul Sharifu katikati akiangalia watoto walipokuwa wakicheza wakati wa uzinduzi wa mfuko wa watoto yatima kata ya Miono wilayani humo.

WAKURUGENZI WA HALMASHAURI WASHUKIWA

Na John Gagarini, Bagamoyo

WAKURUGENZI wa Halmashauri za wilaya na Miji mkoani Pwani wametakiwa kuwashirikisha maofisa tarafa kwenye vikao mbalimbali vya maendeleo kwani wao ni wasimamizi wa mambo yote kwenye tarafa zao.

Hayo yalisemwa mjini Bagamoyo na katibu tawala wa mkoa wa Pwani Beatha Swai, wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo maofisa tarafa wa mkoa huo.

Swai alisema kuwa anawashangaa wakurugenzi wa halmashauri kutowatenga maofisa hao ambao ni kiungo muhimu baina ya serikali na wananchi lakini wamekuwa wakiwekwa pembeni na kuonekana kama hawastahili kushiriki kwenye masuala mbalimbali ya maendeleo.

“Inashangaza hata kwenye vikao vya uongozi juu ya maendeleo hawashirikishwi kama ilivyo kwa wataalamu wengine kwenye halmashauri hawa nao wanapaswa kupewa kipaumbele katika michakato mbalimbali ya maendeleo,” alisema Swai.

Alisema kuwa tayari serikali ilishawapa waraka wakurugenzi hao kuwashirikisha kwenye masuala yote yanayohusu utendaji kazi ili wafanye kazi kwa pamoja lakini bado wanakaidi maagizo hayo.

“Tumeona kuwa kwenye vikao vya uongozi juu ya maendeleo hawashirikishwi jambo ambalo ni kinyume cha taratibu hivyo tutawachukulia hatua kali za kisheria wakurugenzi wote ambao wanakiuka taratibu za kazi,” alisema Swai.

Aidha alisema kuwa wakurugenzi hao wamekuwa na dhana kuwa maofisa tarafa hao wanakwenda kwa ajili ya kupata posho jambo ambalo halina ukweli kwani kushiriki kwenye vikao kama hivyo ni haki yao.
Awali akifungua mafunzo hayo mkuu wa mkoa wa Pwani Mwantumu Mahiza alisema kuwa baadhi ya maofisa tarafa wengine hawajui wajibu wao.

Mahiza alisema kuwa maofisa tarafa hao wanapaswa kujua wajibu wao kwa kutimiza malengo ambayo yanawekwa na halmashauri na wanapaswa kuwa na taarifa zote za shughuli za maendeleo na changamoto ndani ya tarafa zao.

Mwisho.

 
mkuu wa mkoa wa Pwani Mwantumu Mahiza akizungumza na maofisa tarafa wa mkoa huo alipokuwa akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo kwenye ukumbi wa chuo cha uongozi cha ADEM Bgamaoyo mkoani Pwani

baadhi ya maofisa tarafa wa mkoa wa Pwani wakimsikiliza mkuu wa mkoa wa Pwani Mwantumu Mahiza hayupo pichani wakati akifungua mafunzo kwa maofisa hao kwenye ukumbi wa chuo cha uongozi cha ADEM Bagamoyo mkoani Pwani.