Na John Gagarini, Bagamoyo
MBUNGE wa Chalinze wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani Said
Bwanamdogo amevitaka vikundi vya sanaa na michezo kwenye kata ya Miono
kumpelekea mahitaji yao ili aweze kuwasaidia.
Alitoa ahadi hiyo wakati akikabidhi fedha kwa kikundi cha
akinamama cha upendo cha Upendo Saccos cha Miono na kusema kuwa vikundi hivyo
vinahitaji misaada ili viweze kukua.
Bwanamdogo alisema kuwa vipaji vingi vijijini huwa vinapotea
kutokana na kushindwa kuendelezwa kutokana na kukosa vifaa na mahitaji
mbalimbali.
“Lengo ni kutaka kusaidia vikundi mbalimbali ili viweze
kujiendeleza hasa tukizingatia kuwa sanaa na michezo ni sehemu ya ajira na si
kujairiwa maofisini pekee,” alisema Bwanamdogo.
Aidha alisema kuwa vikundi vya sanaa na michezo viko vingi
lakini havina sehemu ya kusaidiwa ili viweze kuwa na ustawi kama vilivyokuwa
vya mijini.
“Nimeona vikundi vingi vya sanaa na michezo vinauwezo mkubwa
lakini havijaendelezwa hivyo nitahkikisha kuwa navisaidia ili viweze kusonga
mbele,” alisema Bwanamdogo.
Aliongeza kuwa kwa sasa anajipanga vema ili aweze kuandaa
mashindano mbalimbali ya michezo kwa vijana waweze kuonyesha vipaji vyao.
Mwisho.