Tuesday, April 18, 2023

TANZANIA KUBORESHA MAWASILIANO

 


SERIKALI ya awamu ya sita inayoongozwa na Dkt Samia Suluhu Hassan imedhamiria kuhakikisha Tanzania inakuwa na miundombinu bora ya mawasiliano yenye kutumia Teknolojia ya kisasa ambayo italeta tija na ufanisi katika kuongeza uzalishaji na ujenzi wa uchumi na kuimarisha usalama na ulinzi wa Taifa.

Hayo yamesemwa Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Moses Nnauye katika hafla ya utiaji saini kati ya TTCL na HUAWEI kuhusu upanuzi wa mkongo wa Taifa wa mawasiliano katika Wilaya 23  uliyofanyika Jijini Dodoma.

Nape amesema zaidi ya  shilingi  bilion 37 zitangharimu ujenzi wa kilometa 1,520 ambazo zitaunganisha Wilaya 23 katika upanuzi wa mkongo wa Taifa wa mawasiliano kati ya shirika la mawasiliano Tanzania na kampuni ya HUAWEI International.

Amesema kuwa mradi huu unaenda kuleta mageuzi makubwa yakiwemo kukuza matumizi ya tehama Wilaya kuongeza kasi ya ukusanyaji mapato pamoja na kuleta fursa kwa wananchi kiuchumi.



Awali kwa upande wake Mkurugezi mkuu wa TCCL  mhandisi Peter Ulanga 

Amesema mradi huu utatoa fursa nzuri kwa wizara , Taasisi za umma na Taasisi binafsi kufikisha huduma Zao kwa wateja na watumiaji wao kwa haraka na wakati kwa kuwa mkongo wa Taifa utakuwa na uwezo mkubwa wa kubeba taarifa za kutuma kwa haraka.

Monday, April 17, 2023

RIDHIWANI AGAWA ZAWADI UHIFADHI QURAAN

Nimeshiriki kugawa zawadi katika mashindano ya Kimataifa ya uhifadhi wa Quraan yaliayofanyika Ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam. Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa fursa hii.

Saturday, April 15, 2023

RIDHIWANI KIKWETE AWASHUKURU WANACHALINZE KWENYE FUTARI


Nimeshiriki futari na Wananchi wenzangu wa Halmashauri ya Chalinze pamoja na viongozi wa Chama na Serikali wa wilaya yetu. Nawashukuru sana Wananchi wenzangu kwa muitikio wenu. Asanteni sana. #RamadhanKareem #Chalinze.

Wednesday, April 12, 2023

BAJETI OFISI YA WAZIRI MKUU


Nimeshiriki kikao cha Bunge kinachojadili Bajeti ya ofisi ya Waziri Mkuu 2023/24. #KaziInaendelea #Bajeti2023

Friday, April 7, 2023

SERIKALI YABORESHA HUDUMA ZA MAJI.


Na Wellu Mtaki, Dodoma

SERIKALI ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dk Samia Suluhu Hassan imefanya jitihada kubwa katika kufanya mabadiliko na maboresho makubwa katika Sekta ya Maji  ikiwa pamoja na kuongeza uwekezaji katika sekta hiyo ili kukabiliana na changamoto zilizoko. 

Hayo yamesemwa na mkuu wa mkoa wa Dodoma Rosemary Sinyamule wakati wa ufunguzi wa tafiti juu ya maombi ya kurekebisha bei za huduma ya maji safi iliyoletwa na mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Dodoma ( DUWASA)

Sinyamule amesema  kuwa lengo kubwa la Serikali katika kufanya mabadiliko na kuongeza uwekezaji katika sekta ya Maji ni kuongeza ubora na upatikanaji wa huduma ili kuboresha maisha ya Wananchi wake na hatimaye kufikia lengo la asilimia 95 (kwa mijini) lililowekwa katika Ilani ya Chama cha Mapinduzi ifikapo mwaka 2025.

Awali mwakilishi wa  Mkurugezi mkuu wa Ewura  George Kabelwa katika maombi hayo Mamlaka ya Maji Dodoma imeomba kufanya marekebisho ya bei zitakazotumika kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia mwaka 2023/24 hadi 2025/26  kwa mujibu wa maombi yaliyowasilishwa EWURA, Mamlaka ya Maji Dodoma imebainisha kuwa marekebisho ya bei ya maji yanalenga kupata fedha za kutosha kukidhi gharama halisi za uendeshaji na matengenezo kwa lengo la kuboresha huduma zitolewazo.

Aidha Mamlaka ya Maji Dodoma imeeleza kuwa bei zinazopendekezwa zitaiwezesha mamlaka kumudu gharama zote za utoaji huduma   pamoja na mambo mengine, kuendelea kuongeza ubora wa maji, kuiwezesha mamlaka kuwa endelevu na kukidhi matarajio ya wana Dodoma.  

Kwa upande wa wakilishi wa wananchi Revina Petro Lamiula  ametoa maoni kwa kusema kuwa pamoja na bei kupandishwa ila wanaitaka mamlaka ya maji safi (Duwasa) kuhakikisha wanaboresha huduma zao.

Wednesday, April 5, 2023

WATAKIWA KUTUMIA VANILLA MARA KWA MARA

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

MKURUGENZI Mkuu wa Vanilla International Limited Simon Mnkondya ameitaka jamii kutumia zao la Vanilla katika matumizi ya kila siku kwani zao hilo huchochea kuwa na akili zaidi.

Mnkondya amebainisha hayo Jijini Dodoma kwenye kikao Cha wadau wa zao la Vanilla.

Amebainisha kuwa ili kuweza kuwa na akili nyingi,hata wanasayansi Duniani wamekuwa wakitumia malighafi inayopatika katika zao la Vanilla hali inayopelekea kuwa wabunifu na kubuni vitu mbalimbali.

Aidha Mnkondya amebainisha kuwa vyama vya ushirika vimekuwa vikiwaibia wakulima bila kuwatengenezea masoko ya uhakika na badala yake vimekuwa vikitengeneza wezi.

Pia amebainisha kuwa kilimo Cha Vanilla soko lake linapatikana Kwa wingi katika nchi za uarabuni na Vanilla inayonuniliwa sana ni Vanilla ya gradi la kwanza.

Katika kuuza zao la Vanilla Kwa Duniani ya sasa Mnkondya amebainisha kuwa haina haja ya kubeba mzigo kupeleka katika nchi unaweza kuuza kupitia mtandao Kwa kuandika vigezo vya zao lako la Vanilla na wateja wakakufata wenyewe.

Ameongeza kuwa zao la Vanilla halitakiwi kulimwa kiholela na badala yake amewashauri wakulima kulima,kulima Kwa pamoja kilimo Cha Block Farming.

WATAKIWA KUPINGA UKATILI

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

MKUU wa Mkoa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amewaasa wananchi wa Kata ya Chang'ombe kukubali kubadilika kupinga Ukatili kwa kushirikiana pamoja ili Mkoa wa Dodoma kuwa wa Mfano kwa maendeleo ya Taifa. 

Ameyasema hayo aliposhiriki katika Kongamano la Kupinga Ukatili Mkoa wa Dodoma lililoandaliwa na kamati ya kutokomeza Ukatili wa Kijinsia na Msaada wa Kisheria, kupitia kikundi cha Wanawake na Samia na kusikiliza kero za wananchi wake katika Mtaa wa Mazengo Chang'ombe. 

Senyamule amesema kuwa Chang'ombe bila vitendo vya kikatili inawezekana na kutoa rai kwa wazazi na walezi wa Kata ya Chang'ombe kutoficha vitendo viovu vya watoto na vijana katika jamii inayowazunguka ili jitihada za pamoja za kutokomeza vitendo vya kikatili ziweze kufanikiwa.

Aidha, Mhe. Senyamule ameendelea kumshukuru Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuimarisha Mkoa wa Dodoma kwa miradi mikubwa ya kimkati ambayo ni fursa kwa vijana ambayo ni fursa kwao kujishughulisha na shughuli za uzalishaji mali kwani wana sehemu ya kupeka nguvu kazi zao ili kujiepusha na tabia zisizo na Maadili.

"Mimi kama Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ningetamani kila Kata, Mtaa, Kaya na kila nyumbani isiwe na mhalifu wala mtu yeyote anaefanya ukatii na unyanyasaji wa kijinsia, lakini itawezekana kama sisi wananchi tutaamua kuungana na juhudi na dhamira nzurii za Serikali 

"Vijana mjipange kubadilika sisi kama Mkoa tunadhamira njema na kizazi cha nchi hii, ni wakati sahihi wakujiwekea sheria ambazo tutasimamia wenyewe zinazohusu Ukatili wa Kijinsia kwani inawezekana kubadilika kusiwe na vijana vibaka, wezi ili kupongeza wale wenye Maadili mazuri na kuwa mfano wa kuigwa "Amesema Senyamule. 

Naye Mwanakamati ya kupinga Ukatili Fatuma Madidi ametoa elimu juu ya Ukatili wa nafsi, watoto, vijana, wazee na Wanawake ili kuweza kutambua Madhara ya Ukatili kwa Ujumla na kuendelea kujihadhalisha .

Kwa Upande wake Diwani wa Chang'ombe Bw. Bakari Fundikira amemshukuru Mkuu wa Mkoa kwa ujio wake katika kata yake na kuahidi kuendelea kutekeleza maelekezo yake.