Saturday, March 4, 2017

MAPAMBANO DHIDI YA DAWA ZA KULEVYA WATANZANIA WATAKIWA KUUNGA MKONO MAPMBANO



Na John Gagarini
WATANZANIA wametkiwa kuunga na serikali ya awamu ya tano katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya na matumizi ya pombe za viroba kwa kutowajengea chuki wale wanaokabili suala hilo.
Hayo yalisemwa na Kuhani mkuu wa Kituo cha Maombi na Maombezi cha Gombo Gambusi Alista Albano kilichopo Kibamba Jijini Dar es Salaam na kusema kuwa vita hiyo ni ya wananchi wote ili kuwanusuru Watanzania.
Albano alisema kuwa dawa hizo na pombe hiyo imewafanya watumiaji kudhurika na kushindwa kufanya kazi zao kikamilifu ambapo baadhi wamejikuta wakiwa wagonjwa na wengine kufikia hatua ya kupoteza maisha.
“Tumuunge mkono Rais wetu Dk John Magufuli katika vita hii ambayo imepewa nguvu na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda lakini kuna abaadhi ya watu wameonekana kupingana na mapambano hayo jambo ambalo linashangaza,” alisema Albano.
Alisema kuwa athari ya matumizi ya dawa na pombe hizo ni makubwa tofauti na watu wanavyofikiria ambapo nguvu kazi kubwa imeathirika na kushindwa kuzalisha kutokana na matumizi hayo.
“Sisi kama kaanisa tunapaswa kuliombea Taifa ikiwa ni pamoja na viongozi wetu ambao wanajaribu kuhakikisha wanatuletea maendeleo lakini kwanza wanaondoa vikwazo vilivyokuwa vinazuia nchi ishindwe kupiga hatua ikiwemo dawa na pombe hizo,” alisema Albano.
Aidha alisema Magufuli ni moja ya viongozi ambao ni bora na wataleta mabadiliko makubwa ya nchi na kuifanya Tanzania kuwa nchi ambayo itazalisha na kutoa misaada tofauti na ilivyo sasa imekuwa nchi ya kuomba wahisani.
“Hamasa yake ya kuifanya Tanzinia kuwa nchi ya viwanda itafanya nchi kuwa na uzalishaji wa bidhaa mbalimbali hivyo itasababisha uchumi kukua na kuwa moja ya nchi zitakazokuwa zinatoa misaada kwa nchi nyingine,” alisema Albano.
Alibainisha kuwa nchi kwa sasa inapita kwenye kipindi cha mpito lakini baadaye kila mwananchi atafurahia maisha kwani anarejesha vile ambavyo viliporwa na watu wachache ili viweze kutumiwa na watu wengi.
“Ninachowaomb Watanzania wenzangu tuache kulalamika kwani tumebakia kulalamika badala ya kufanya kazi kwani malamiko hayataweza kutusaidia badala yake yatatufanya tusiwajibike,” alisema Albano.
Alisisitiza kuwa Rais Magufuli ni mkombozi wa Taifa hili hivyo watu wamwombee katika kuirekebisha nchi na kuiweka katika mazingira mazuri ya kutoa huduma nzuri kwa wananchi wake.
Mwisho.

   

Friday, February 24, 2017

MWIJAGE AWEKA JIWE LA MSINGI KIWANDA CHA VIGAE PWANI










Na John Gagarini,Chalinze

WIZARA ya Biashara Viwanda na Uwekezaji imesema kuwa imeweka mazingira mazuri ya uwekezaji na kuzitaka taasisi zinazohusika na uwekezaji kutokuwa na ukiritimba.
Hayo yalisemwa na Waziri wa Biashara Viwanda na Uwekezaji Charles Mwijage kwenye Kitongoji cha Pingo Chalinze wakati akiweka jiwe la Msingi kwenye kiwanda cha Vigae cha Twyford Ceramics Ltd.
Mwijage alisema kuwa uwekezaji kama huu unaendana na dhana ya Rais Dk John Magufuli wa kuifanya nchi kuwa ya Viwanda ambapo itaongeza pato la nchi na itazalisha ajira kwa wingi.
“Baadhi ya idara ambazo zinafanikisha uwekezaji ikiwa ni pamoja na brela, idara ya uhamiaji, idara ya kazi, mamlaka ya mapato TRA, wizara ya ardhi, shirika la viwango TBS, Baraza la Mazingira NEMC na nyinginezo zinapaswa kufanya kazi kwa wepesi ili kufanikisha uwekezaji,” alisema Mwijage.
Alisema kuwa kati ya idara hizo baadhi zimekuwa zikifanya vizuri lakini nyingine zimekuwa zikiwapa usumbufu mkubwa wawekezaji hali ambayo inawakatisha tamaa.
“Kwa upande wa wizara yangu hakuna tatizo lolote lakini kuna baadhi ya idara zimekuwa kero kubwa kwa wawekezaji kwa kuwa na ukiritimba usio na sababu naomba kama kuna idara zinakuwa kikwazo niambieni ili tuwachukulie hatua,” alisema Mwijage.
“Viwanda vikiwa vingi nchi itapata mapato makubwa kupitia kodi ambazo zitalipwa kutokana na uuzwaji wa bidhaa zitakazokuwa zinazalishwa viwandani,” alisema Mwijage.
Alisema kuwa nchi zilizofanikiwa kukuza uchumi wake kupitia viwanda zimeweza kutoa ajira nyingi hasa kwa vijana kupitia sekta rasmi na isiyo rasmi.
Kwa upande wake mkurugenzi mkuu wa kiwanda hicho Jack Feng alisema kuwa kiwanda hicho asilimia 95 ya malighafi itakuwa inatoka hapa nchini ambapo kigae kinatumia maligahafi zaidi ya 10.
Feng alisema kuwa mara kiwanda hicho kitakapokamilika Agosti mwaka huu kitaweza kupunguza asilimia 30 ya uagizaji wa vigae toka nje ya nchi.
“Tunatarajia kuajiri wafanyakazi 2,000 moja kwa moja na 4,000 kazi za muda na gharama ya mradi huu ni dola milioni 56 sawa na bilioni 120 ambapo tunatarajia kuuza hadi nje ya nchi kama vile Zambia, Uganda, Rwanda na Burundi,” alisema Feng.
Alisema kuwa wanaunga mkono nchi ya Tanzania kuwa na mpango wa kuwa nchi ya viwanda na wao wanapenda kuwa mfano kwa wawekezaji.
Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa kituo cha uwekezaji Cliford Tandari alisema kuwa uwekezaji wa kiwanda hicho ni wa mfano kwani utavutia makampuni mengi.
Tandari alisema kuwa hadi sasa kituo chake kimeweza kutoa wigo mkubwa katika kuandikisha miradi mbalimbali toka china na kufikia miradi 667 ambayo itazalisha ajira 83,141 kwa watanzania ambapo miradi 452 ni miradi inayohusiana na sekta ya uzalishaji viwandani.
Naye mkuu wa mkoa wa Pwani Injinia Evarist Ndikilo alisema kuwa kwa sasa mkoa huo umeweza kuwa na viwanda 264 huku vikubwa vikiwa ni viwili.
Ndikilo alisema kuwa uwekezaji huo ni mkubwa na unatarajia kukuza ajira kwa vijana wa mkoa wa Pwani na Tanzania kwa ujumla.
Alisema kuwa mkoa wa Pwani bado una maeneo makubwa ya uwekezaji na tayari kuna eneo lenye bukubwa wa hekari 5,000 linahitaji mwekezaji na wameamua mkoa huo kuwa kituo cha uwekezaji.
Naye Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete aliwapongeza wawekezaji hao kutoka nchi ya China na kusema kuwa Chalinze nayo imejipanga kuwa sehemu ya uwekezaji ambapo kuna ujenzi wa viwanda mbalimbali.
Ridhiwani alisema kuwa changamoto kubwa inayokabiliwa wananchi na wawekezaji ni ukosefu wa maji ambapo wamekuwa wakijitahidi kuikabili lakini bado hawajafanikiwa kuidhibiti aliomba wawekezaji hao kutoa ajira bila ya kuwabagua wenyeji.
Mwisho.









Ramani ya kiwanda cha vigae cha Twyford kilichopo Pingo Chalinze wilayani Bagamoyo mkoani Pwani 


Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage akiongea wakati wa uwekeji jiwe la msingi kiwanda cha vigae cha Twyford kilichopo Pingo Chalinze wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.




Mkuu wa mkoa wa Pwani Injinia Evarist Ndikilo wa pili kulia akiwa na Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete kulia wakifuatilia jambo wakati wa uwekaji jiwe la msingi kwenye kiwanda cha vigae cha Twyford kilichopo Pingo Chalinze wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.




Katikati Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage akifunua kitambaa kuashiria uwekeji jiwe la msingi kwenye kiwanda cha vigae cha Twyford kilichopo Pingo Chalinze wilayani Bagamoyo mkoani Pwani kushoto mkuu wa mkoa wa Pwani Injinia Evarist Ndikilo kulia kwa waziri ni Jack Feng mkurugenzi wa kiwanda hicho na Mbunge wa Jimbo la Chalinze Riziwani Kikwete.


  


Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo kushoto Magid Mwanga akifuatiwa na mkuu wa mkoa wa Pwani Injinia Evarist Ndikilo, mkurugenzi wa kiwanda cha vigae cha Twyford Jack Feng na mbunge wa Jimbo la Chalinze Riziwani Kikwete wakiweka udongo kwenye jiwe la msingi.



Friday, February 3, 2017

VIJANA JKT WALIOJITOLEA UJENZI MABWENI WAPONGEZWA

 Mkuu wa mkoa wa Pwani mwenye shati jeupe Injinia Evarist Ndikilo akionyeshwa ramani ya majengo ya mabweni ya shule ya sekondari ya Nasibugani na moja ya wasimamizi wa ujenzi huo yanayaojengwa na vijana toka Jeshi la Kujenga Taifa JKT Ruvu Mlandizi wilayani Kibaha, kushoto ni katibu tawala wa mkoa Zuber Samataba  
Na John Gagarini, Mkuranga
MKUU wa mkoa wa Pwani Injinia Evarist Ndikilo emelipongeza Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kambi ya Ruvu Mlandizi wilayani Kibaha kwa kujitolea kujenga mabweni ya shule ya Sekondari ya Nasibugani iliyopo kata ya Msonga Tarafa ya Kisiju wilayani Mkuranga.
Alitoa pongezi hizo alipotembelea shule hiyo ili kujionea maenedeleo ya ujenzi huo wa mabweni matano na nyumba tano za walimu za shule hiyo ambapo wanafunzi wanalala kwenye baadhi ya vyumba vya madarasa.
Ndikilo alisema kuwa kambi hiyo ilitoa vijana zaidi ya 100 ambao wanaenedelea na ujenzi huo ambao umefikia hatua ya linta na kwa sasa wana miezi mitatu.
“Jeshi limeonyesha uzalendo wa hali ya juu kwa kujitolea kujenga bure mabweni hayo lengo ni kuhakikisha wanafunzi wa shule hiyo wanaishi kwenye mazingira mazuri kuliko ilivyo sasa,” alisema Ndikilo.
Alisema kuwa jeshi hilo limeunga mkono serikali kwa kujitolea kujenga mabweni hayo hivyo kuokoa fedha nyingi endapo wamengepewa wakandarasi.
“Hadi sasa wametumia fedha kidogo sana kiasi cha zaidi ya milioni 120 lakini endapo wangewapa wakandarasi fedha ambazo zingetumika zingekuwa ni nyingi zaidi,” alisema Ndikilo.
Alisema kuwa watu wanaojitolea wanaisadia serikali kwa kuiunga mkono kwa mambo mambo ya kimaendeleo inayoyafanya hali ambayo inapunguza gharama na fedha hizo zinazookolewa zinatumika kwenye mipango mingine.
“Kwa kuwa ujenzi unaendelea tunawaomba wadau mbalimbali waendelee kujitokeza kusaidia ujenzi huo ili ukamilike mapema na wanafunzi waweze kuishi kwenye mazingira mazuri na mnachotakiwa kukifanya kwa sasa ni kufanya upembuzi kujua mahitaji ya vitu vinavyotakiwa ili kukamilisha zoezi hili,” alisema Ndikilo.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Mkuranga Gilbert Sanga alisema kuwa anawashukuru wadau mbalimbali ambao wamejitolea kujenga mabweni hayo na kufikia hatua hiyo.
Sanga alisema kuwa Waziri wa elimu Profesa Joyce Ndalichako alitoa kiasi cha shilingi milioni 250 ambazo zianaendelea kutumika katika ujenzi wa mabweni hayo hadi sasa   
Alisema kuwa kazi ya kupanua ilianza kwa wananchi kuchangia zaidi ya milioni nne na kuwataka wanaochangisha wawasilishe fedha walizochangisha ili zifanye kazi husika
“Halmashauri walisema wametenga fedha kiasi cha shilingi milioni 32 kwa bweni moja wanafunzi 48 tu tuliungana na kamati ya ulinzi na usalama nao walikubali kuongeza mabweni zaidi na mkoa nao ukakubali na kambi ya wazalendo ambao walipiga kambi na walifyetua tofali 45,000 na ni kazi ambayo haina bajeti,” alisema Sanga.
Kwa upande wake msimamizi wa ujenzi toka kikosi cha Ruvu JKT Mohamed Boko alimwomba mkuu wa mkoa wa Pwani kufanya jitihada ili ujenzi huo uweze kukamilika ambapo kazi hiyo ilipangwa kufanyika kwa miezi miwili lakini imekuwa kubwa na muda kuongezeka.
Mwis

Wednesday, January 25, 2017

WAFANYABIASHARA MAILIMOJA WAHUKUMIWA KIFUNGO CHA NJE.

Na John Gagarini, Kibaha
WAFANYABIASHARA 62 wa lililokuwa soko la Maili Moja wilayani Kibaha mkoani Pwani waliofanya mkusanyiko usio halali na kutaka kumwona Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Seleman Jaffo wamehukumiwa kifungo cha nje cha miezi sita.
Hukumu hiyo ilitolewa kwenye mahakama ya hakimu mkazi wa mahakama ya wilaya ya Kibaha Aziza Mbadjo chini ya mwendesha mashtaka mwanasheria wa serikali Auleria Makundi na mkaguzi wa Polisi Rashid Chamwi.
Mahakama ilielezwa kuwa wafanyabiashara hao bila ya kibali walifanya mkusanyiko huo huku wakiwa na mabango yenye jumbe mbalimbali na kutaka kumwona Waziri Jaffo.
Na walifanya mkusanyiko huo wakitaka kutoa malalamiko yao juu zoezi zima la uhamishwaji wao kutoka soko la Maili Moja ambalo limebomolewa hivi karibuni kwenda soko jipya la Mnarani au Sagulasagula maarufu kama Loliondo.
Ikaelezwa kuwa washtakiwa kwa pamoja walitenda kosa hilo Januari 6 mwaka huu majira ya saa 4 asubuhi eneo la Shirika la Elimu Kibaha (KEC) Tumbi walifanya mkusanyiko bila ya kibali toka Polisi wilaya.
Pia walikuwa na mabango hayo jambo ambalo ni kinyume cha sheria jambo ambalo lilionyesha kuleta usumbufu kutokana na kukosa uhalali wa kufanya hivyo.
Baada ya kusomewa shitaka hilo ambalo ni kinyume cha sheria namba 74 (1-2) na 75 kifungu kidogo cha kanuni ya adhabu kilichofanyiwa mapitio mwaka 2002 walikiri kutenda kosa hilo na walijitetea kwa kusema kuwa walifanya kosa hilo bila ya kujua na wanamajukumu mengi ya kifamilia hivyo kuiomba mahakama iwapunguzie adhabu.
Kutokana na utetezi huo hakimu Mbadjo alisema kuwa kutojua sheria siyo sababu ya kuvunja sheria hivyo mahakama imewakuta na hatia hivyo wanahukumiwa kifungo cha nje ambapo wataitumikia jamii na hawapaswi kufanya kosa katika muda huo.
Mwisho.  


Monday, January 23, 2017

johngagariniblog: BOMOA YATIKISA MAILI MOJA KIBAHA

johngagariniblog: BOMOA YATIKISA MAILI MOJA KIBAHA: Na John Gagarini, Kibaha ZOEZI la kubomoa soko la Maili Moja wilayani Kibaha pamoja na nyumba za biashara na za makazi amba...

BOMOA YATIKISA MAILI MOJA KIBAHA





Na John Gagarini, Kibaha
ZOEZI la kubomoa soko la Maili Moja wilayani Kibaha pamoja na nyumba za biashara na za makazi ambavyo vilijengwa kwenye hifadhi ya barabara limefanyika na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) mkoa wa Pwani chini ya ulinzi mkali wa polisi.
Zoezi hilo ambalo lilianza jana majira ya asubuhi limefanyika baada ya kushindikana kufanyika kwa muda mrefu ambapo mara ya mwisho wameliki wa maeneo hayo walipewa barua na TANROADS miezi sita iliyopita.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake meneja wa wakala hao mkoa wa Pwani Injinia Yudas Msangi alisema kuwa lengo kuu la kubomoa ni kuhakikisha kuwa eneo hilo la hifadhi ya barabara inakuwa wazi.
Msangi alisema kuwa zoezi hilo limefanikiwa kutokana na kuwajulisha mapema wahusika kuwa wabomoe wenyewe kabla ya siku ya kubomoa kufanyika jana Januari 23.
“Tunashukuru kwani hakuna mtu anayelalamika kwa sababu tuliwapa taarifa mapema na wengi wametii kwa kuvunja wao wenyewe na kutoa vitu vyote vya thamani licha ya wachache ambao walishindwa kubomoa wao wenyewe,” alisema Msangi.
Alisema kuwa zoezi hilo kwa Maili Moja ndiyo limehitimisha ubomoaji kwa watu waliojenga kwenye hifadhi ya barabara katika mkoa huo ambapo mwaka jana walibomoa maeneo mengine ya wilaya zote za mkoa huo.
“Baada ya zoezi la kubomoa wananchi hawpaswi kujenga tena kwenye eneo hilo la hifadhi ya barabara ambalo lina matumizi mbalimbali kwa ajili ya magari na shughuli nyingine zinazohusu barabara,” alisema Msangi
Aidha alisema kuwa jana walivunja eneo la umbali wa mita 60 kutoka barabara kuu ya Morogoro ambazo ziko ndani ya hifadhi ya barabara ambayo ilitengwa kwa ajili ya matumizi mengine.
Naye mkaguzi wa barabara Injinia Livingstone Urio alisema kuwa zoezi hilo ni mwendelezo wa usafishaji wa maeneo ambayo ni hifadhi ya barabara ambapo pia ni usalama kwa wananchi kwani ni hatari kujenga au kufanya biashara karibu na barabara.
Urio alisema kuwa eneo hilo lilitengwa kisheria na watu hawakutakiwa kujenga makazi au vibanda vya biashara na wananchi wengi wao wanajua mmiliki wa eneo hilo.
Kwa upande wake mfanyabiashara wa soko la Maili Moja Ally Gonzi alisema kuwa wao wamepokea zoezi hilo kama lilivyo kwani tayari wlaikuwa na taarifa juu ya matumizi ya eneo hilo.
Gonzi alisema kuwa kwa kuwa wametengewa eneo la kufanyia biashara hivyo wataenda huko kwa ajili ya kuendelea na biashara zao licha ya kuwa maandalizi ya soko jipya wamechelewa.

Mwisho.

Friday, January 13, 2017

MATUKIO YA UHALIFU YALIYOTIKISA PWANI 2016


Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani Bonaventura Mushongi akiwaonyesha waandishi wa habari hawapo pichani silaha aina ya SMG no 01304 ikiwa na risasi 30 ya Askari Jackson Shirima  wa Saadani National Park ambaye aliporwa na mtuhumiwa Swalehe Mangupili na kufichwa kichakani huko Kijiji cha Gama wilaya ya Bagamoyo

Na John Gagarini, Kibaha

JUMLA ya makosa makubwa ya uhalifu 4,208 yameripotiwa kwenye vituo vya polisi mkoani Pwani kwa mwaka 2016 ambapo kumekuwa na ongezeko la makosa 419 ikilinganishwa na mwaka 2015 ambao ulikuwa na makosa 3,784.
Aidha makosa madogo 16,332 yaliripotiwa katika kipindi hicho cha mwaka 2016 ambapo kuna ongezeko la makosa 2,396 ikilinganishwa na mwaka 2015 ambapo kulikuwa na makosa 13,936.
Hayo yalisemwa mjini Kibaha na kamanda wa polisi mkoani Pwani Bonaventura Mushongi wakati akitoa taarifa ya mwaka mmoja uliopita na kusema kuwa watu waliohusika na matukio hayo walifikishwa mahakamani.
Mushongi alisema kuwa ongezeko la makosa hayo kumetokana na misako iliyofanywa, doria na oparesheni kwenye maeneo mbalimbali sambamba na ushirikishwaji wa jamii kwenye kufichua uhalifu.
“Tunawashukuru wananachi kwa kuendelea kutupa taarifa mbalimbali ambazo zimesaidia kukabiliana na uhalifu na tunaomba ubia uendelee kwani uwiano wa askari na raia bado hautoshi kwani askari mmoja anahudumia raia zaidi 1,000 hivyo ulinzi shirikishi ni muhimu,” alisema Mushongi.
Alisema kuwa katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita walifikisha mahakamani makosa 1,439 na makosa 159 watuhumiwa walikutwa na hatia na kuhukumiwa kifungo wakati makosa 29 watuhumiwa walishindwa kutiwa hatiani na kuachiwa huru  na makosa mengine kesi bado zinaendelea kwenye mahakama mbalimbali.
“Tumejiwekea mikakati mbalimbali ya kukabiliana na uhalifu kwa kuimarisha vikosi mbalimbali vilivyopo ndani ya mkoa, kuzuia na kutanzua matukio hayo kabla hayajatokea au baada ya kutokea, kuimarisha doria za miguu katika maeneo tete kila wilaya kwa ushirikiano na wananchi,” alisema Mushongi.
Aidha alisema kuwa wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni upungufu wa vitendea kazi ikiwa ni pamoja na uchache wa magari,Jografia ya mkoa kwwenye mipango miji ni ngumu katika kumpata mhalifu kwa haraka pindi uhalifu unapotokea.
“Mwaingiliano na mkoa wa Dar es Salaam unafanya wahalifu kuweza kuingia kirahisi na kufanya makosa,kutokuwa na mpango bora wa matumizi ya ardhi hivyo kusababisha migogoro ya ardhi katika jamii, uwepo wa ukanda wa mkubwa katika bahari unaosababisha kuwepo kwa bandari bubu nyingi za kupitisha wahamiaji haramu na biashara za magendo,” alisema Mushongi.
Alibainisha kuwa mwaka uliopita kulikuwa na matukio makubwa ambayo yaliyovuta hisia za watu ikiwa ni pamoja na kupatikana maiti saba wilaya ya Bagamoyo na mauaji ya viongozi wa serikali za vijiji kwa wilaya za Mkuranga, Rufiji na Kibiti ambapo katika matukio hayo watu 11 walikamatwa  na kufikishwa mahakamani.
Mwisho.