Monday, April 28, 2014

story pwani

 John Gagarini, Bagamoyo
KITONGOJI cha Biga kata ya Mkange wilayani Bagamoyo mkoani Pwani ambacho kilikumbwa na mafuriko hivi karibuni kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha hapa nchini kimeomba serikali kuwapatia mbegu za mahindi tani 2.5 kwa ajili ya kupanda tena zao hilo.
Ombi hilo limekuja baada ya hekari 510 za wakazi wa kitongoji hicho kusombwa na maji ya mvua ambazo zilinyesha kabla ya mvua kubwa za mafuriko kunyesha hivi karibuni ambapo kilizungukwa na maji na kuwafanya wakazi wengine kupewa hifadhi ya muda.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi diwani wa kata hiyo ya Mkange Abdala Mwendadi alisema kuwa mazao ya wakazi hao yote yalisombwa na maji hali ambayo itasababisha kitongoji hicho kuwa hatarini kukumbwa na njaa.
"Kutokana na hali hiyo wakazi wa kitongoji hicho wanaomba serikali iwapatie mbegu kwa ajili ya kupanda mahindi mara mvua hizi zitakapokwisha ambapo msimu huo mahindi yake huitwa "Mahindi ya Kitopeni" ambayo hupandwa baada ya mvua kwisha mwezi Mei kiloa mwaka," alisema Mwindadi.
Mwindadi alisema kuwa jumla ya kaya 63 zimeathiriwa na mvua hizo ambapo zaidi ya watu 200 wameathirika hivyo kuwafanya kuhama kwenye maeneo hayo na kwenda kwa ndugu jamaa kwa ajili ya hifadhi.
"Wakazi wengi waliokumbwa na mafuriko hayo ni wale waliokuwa wakiishi kwenye mkondo wa maji ambapo kutokana na mvua hizo kumechangia kukumbwa na mafuriko hayo ambayo yamesomba mazao yote yaliyopandwa msimu wa kilimo," alisema Mwindadi.
Aidha diwani huyo wa kata ya Mkange alisema kuwa kutokana na maombi hayo atayapeleka halmashauri ili hatua za kuwasaidia zianze kwani endapo hawatapata msaada huo hali ya chakula kwenye kitongoji hicho itakuwa mbaya.
mwisho.
Na John Gagarini, Bagamoyo
MWENYEKITI wa Kijiji cha Kinzagu William Makumu ameshangzwa na wawekezaji kwenye kijiji hicho kushindwa kuchangia maendeleo hasa kwenye sekta ya barabara kutokana na kuingiza magari makubwa kwa ajili ya kubeba kokoto.
Alisema kuwa kuna wawekezaji wengi ambao wamewekeza kwenye uchimbaji kokoto ambazo zinatumika kwa ajili ya ujenzi wa nyumba na barabara hasa Jijini Dar es Salaam.
Makumu alisema kuwa uwekezaji mkubwa kijijini hapo ni uchimbaji wa kokoto kutokana na kijiji hicho kuzungukwa na milima ya mawe.
"Wamekuwa wakiingiza mamilioni ya fedha kwa ajili ya uchimbaji wa kokoto ambapo magari makubwa ambayo yanafikia hadi uzito wa tani 30 hutumia barabara za kijiji lakini hawazikarabati licha ya wao kufanya uharibifu mkubwa," alisema Mukamu.
Alisema kuwa kabla ya kupewa maeneo kwa ajili ya kuendeshea shughuli zao huomba kupitia mkutano wa Kijiji ambapo hutakiwa kutoa asilimia fulani kutokana na mapato yao pia hutakiwa kutoa nguvu zao kwa ajili ya kufanya kazi za maendeleo.
"Tatizo wao wamekuwa wakiangalia upande wao mfano ni eneo la barabara ambazo zimeharibika sana kutokana na wao kuingiza magari yao ya kubebea kokoto lakini hawako tayari kuzitengeneza licha ya kuwa wao ndiyo watumiaji wakubwa kwa ajili ya kupitisha kokoto kwenda maeneo mengine," alisema Mukamu.
Alibainisha kuwa uchangiaji wa wawekezaji hao ni mdogo sana ikilinganishwa na mapato wanayoyapata na athari wanazoziacha baada ya kupasua mawe kwenye kijiji hicho.
Aliwataka wawekezaji hao kujitahidi kuheshimu mikataba waliyoingia ya kuisadia jamii inayowazunguka ambayo ndiyo iliyowapa ardhi wanayoitumia kwa uwekezaji wao.
mwisho.
Na John Gagarini, Chalinze
HUKU Tarafa ya Chalinze ikiwa kwenye maombi ya kupatiwa wilaya kata ya Bwiringu wilayani Bagamoyo inaendelea na mchakato wa kuhakikisha kuwa inapata nafasi ya kuwa makao makuu ya wilaya hiyo yanakuwa hapo.
Moja ya mambo waliyofanya ni pamoja na kugawa viwanja zaidi ya 11,000 kwa ajili ya makazi na huduma za kijamii kwa wakazi wa kata hiyo iliyopo katikati ya mji huo wa Chalinze.
Hivi karibuni kupitia baraza la Madiwani lilipitisha mpango wa tarafa hiyo kuwa wilaya ambapo suala hilo bado liko kwenye mchakato kwa kupeleka maombi hayo kwenye ngazi husika.
Akizungumza mjini Chalinze diwani wa kata hiyo Nasa Karama alisema kuwa wao wako tayari kufanya hivyo na kuwa makao makuu ya wilaya mpya mara maombi hayo yakapopitishwa na wizara husika.
Karama alisema kuwa moja ya mambo waliyoyafanya kuhakikisha wanapata nafasi hiyo ya kuwa makao makuu ya wilaya ni pamoja na kugawa viwanja hivyo.
"Tumegawa viwanja hivyo kwa kushirikiana na halmashauri ili kuupanga mji wetu uwe kwenye mandhari nzuri na kuepukana na ujenzi holela usiozingatia ramani za mipangomiji," alisema Karama.
Alisema kuwa viwanja hivyo vimetolewa kwa wananchi na wadau mbalimbali wa maendeleo kwenye vijiji vya Mbala, Kibiki na Koo lengo kubwa ikiwa ni kuondokana na ujenzi holela.
"Baadhi ya wadau waliopewa viwanja hivyo tayari wameanza ujenzi huku wengine wakiendelea na michakato ya kuendeleza maeneo yao baadhi yao ni NSSF, wanaotaka kujenga soko la kisasa wakiwa kwenye hatua ya tathmini, ujenzi wa nyumba za watumishi, tume ya utumishi wa umma, ofisi ya Mbunge, TAKUKURU,  benki na kituo cha polisi," alisema Nasa.
Aidha alisema kuwa wametoa fidia ya shilingi milioni 98 kwa wananchi kutokana na kuchukua maeneo yao kwa ajili ya matumizi mbalimbali ya maendeleo.
mwisho.
Na John Gagarini, Kibaha
HOSPITALI Teule ya Rufaa ya mkoa wa Pwani Tumbi imesisitiza kuwa haiuzi damu kama baadhi ya watu wanavyodai kwani hilo ni kosa kisheria.
Akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea hospitali hiyo wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari wa mkoa wa Pwani juu ya hali tete na migogoro iliyoandaliwa na Baraza la habari Tanzania (MCT), mkuu wa kitengo cha maabara Boaz Motto alisema kuwa sera ya afya hairuhusu uuzaji wa damu.
Motto alisema kuwa utaratibu unaonyesha kuwa mgonjwa akipewa damu anapaswa kurejesha ili wagonjwa wengine nao waweze kupata damu wanapokuwa wanahitaji.
"Tatizo huwa linakuwa ni kwa wanafamilia ambapo wanapoambiwa wachangie damu baadhi yao huwa wanashindwa hali ambayo inasababisha kutafuta watu na kuwaomba damu lakini kwa makubaliano ya kuwalipa fedha," alisema Motto.
Alisema kuwa mapatano ya kuuziana damu hayafanyiki hospitalini bali ni makubaliano ya watoa damu na wenye mgonjwa lakini hospitali hutoa damu bure bila ya malipo lakini sharti ni kwamba wenye mgonjwa nao watoe damu ili itumike kwa wengine.
"Hii dhana ya damu kuuzwa imeenea sana lakini sera ya afya hairuhusu hospitali kuuza damu kwa mgonjwa bali ni kwa wanandugu kumtolea damu ambapo watu huwanunua watoa damu na wakifika hospitali hudai kuwa ni ndugu," alisema Motto.
Alisema kuwa kwa sasa hospitali ina damu ya kutosha na haina upungufu ambapo kuna uniti 150 ambazo watu hujitolea kama vile taasisi za jeshi, watu binafsi, wanafunzi na makundi mbalimbali ndani ya jamii.
"Changamoto tuliyonayo ni vipimo vya damu ambapo hutubidi kupeleka kwenye hospitali ya Muhimbili kwa ajili ya kupimwa kujua ubora wake ili iweze kutumika kwa wagonjwa wanaohitaji damu," alisema Motto.
Aidha alisema kuwa magonjwa yanayoongoza ni pamoja na yale ya msimu wa mvua kama vile kichocho, malaria na minyoo ambapo mazalia yake ni kwenye maji huku wakati wa kiangazi magonjwa ni yale ya kifua kikuu, kukohoa na malaria.
mwisho.    
 
Wednesday, April 23, 2014

HABARI MCHANGANYIKO

Monday, January 27, 2014

WAANDISHI WAPIGWA MSASA JUU YA PETS

Na John Gagarini, Kibaha
IMEELEZWA kuwa ili nchi iweze kuendelea watendaji na mamalaka zikiwemo halmashauri hapa nchini zimetakiwa kuwa na uwazi na uwajibikaji ili kuwaletea wananchi maendeleo.
Hayo yalisemwa jana mjini Kibaha na mkuu wa shule kuu ya uandishi wa habari ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Dkt Herbert Makoye  wakati akifungua mafunzo ya ufuatiliaji wa rasilimali za Umma (PETS) kwa waandishi wa habari kutoka vyombo vya habari vya Business Times na Mlimani.
Dkt Makoye alisema kuwa kumekuwa na malalamiko mengi toka kwa wananchi juu ya matumizi mabaya ya fedha za Umma zinazotolewa na serikali hivyo kusababisha huduma muhimu za kijamii.
“Tumeona tufanya mafunzo haya kwa lengo la kuwajengea uwezo waandishi wa habari juu ya kuweza kuandika taarifa juu ya matumizi ya fedha hizo ambazo madhumuni yake ni kuwapunguzia kero wananchi hivyo watapata taarisa sahihi,” alisema Dkt Makoye.
Alisema bila ya uwazi kutakuwa hakuna uwajibikaji hali ambayo itasababisha kutokuwa na maendeleo ya haraka ya mwananchi kujikwamu na hali ngumu ya kimaisha.
“Kupitia mafunzo haya waandishi wanapaswa kuyatumia kwa lengo la kuwapatia wananchi taarifa sahihi juu ya michakato mbalimbali ya matumizi ya fedha hizo na zitasaidia watendaji kuwajibika kwani watakuwa na hofu ya kufuja fedha kwani kuna vyombo vinavyowafuatilia,” alisema Dkt Makoye.
Kwa upande wake Mhariri Mtendaji wa gazeti la Majira Bw Imma Mbuguni alisema kuwa mafunzo hayo ni muhimu kwa waandishi katika ufuatiliaji wa rasilimali za umma zikiwemo fedha zinazotolewa na serikali kwa maendeleo ya wananchi.
Bw Mbuguni alisema pia mafunzo hayo yatasaidia kuibua mijadala mbalimbali juu ya matumizi sahihi ya fedha za Umma ambapo baadhi ya watendaji wanaonekana kutozitumia kwa malengo yaliyowekwa au mahitaji ya wananchi.
Mafunzo hayo yameandaliwa kwa pamoja na Shule Kuu ya Uandishi wa Habari ya Chuo kikuu cha Dar es Salaam kwa kushirikiana na kampuni ya Business Times kutokana na ufadhili wa Mfuko wa Ufadhili wa Vyombo vya Habari (TMF).
Mwisho.

Sunday, January 26, 2014

SACCOS WATAKIWA KULIPA MADENI YA MIKOPO YAO

Na John Gagarini, Kibaha
CHAMA cha Kuweka na Kukopa cha KIWAO SACCOS cha wilayani Kibaha mkoani Pwani kimewapa muda wa miezi mitatu kulipa madeni ya mikopo yao baadhi ya wanachama wake wenye madeni sugu na endapo watashindwa kurejesha ndani ya muda huo watawachukulia hatua kali ikiwa ni pamoja na kuwapeleka mahakamani.
Akiongea na wanachama kwenye mkutano mkuu uliofanyika Shirika la Elimu Kibaha, mwenyekiti wa chama hicho Bi. Magdalena Kabukire alisema kuwa wanachama hao wapatao tisa wana madeni ya mikopo ya muda mrefu.
Bi. Kabukire alisema kuwa tayari wamewaandikia barua wanachama hao kuwakumbushia madeni yao ili waweze kurejesha kufanikisha wanachama wengine waweze kukopa.
“Chama chetu kinakabiliwa na changamoto hiyo ya baadhi yao kuchelewesha kurejesha mikopo hali inayosababisha wengine washindwe kukopa kutokana na fedha nyingi kuwa mikononi mwa watu,” alisema Bi Kabukire.
Naye mwenyekiti wa mtaa wa Mwanalugali kilipo chama hicho Deodatus Rwekaza alisema kuwa watashirikiana na chama hicho kuhakikisha wanarejesha mikopo hiyo.
“Wakiona wanachama hao wanashindwa kulipa kwa kipindi hicho walete majina kwenye ofisi yangu ili waangalie sheria iweze kuchukua mkoando wake, kwani mabenki na asasi za kifedha zimefanya hivyo na wadeni wamelipa,” alisema Bw Rwekaza.
Kwa upande wake ofisa ushirika wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha Bw Kulwa Masambu alisema kuwa ili vyama hivyo viweze kupiga hatua lazima wanachama warejeshe mikopo kwa wakati.
Bw Masambu alisema kuwa vyama hivyo vimekuwa mkombozi kwa wananchi hususani wanawake ambao ndiyo wenye changamoto kubwa ya kuziletea maendeleo familia zao na jamii inayowazunguka.
Kwa mwaka jana chama hicho kiliweza kukopesha wanachama wake 19 kiasi cha shilingi milioni 16.4 na kupata mapato ya shilingi milioni 1.9 hisa zikiwa shilingi 638,000 akiba zikiwa ni m 4.2 na kina jumla ya wanachama 76.

Mwisho.   

Thursday, January 23, 2014

MWINJILISTI AU AJINYONGA

Na John Gagarini, Kibaha
MWINJILISTI wa Kanisa Anglikana Eliakia Daniel (35) amekufa kwa kujinyonga baada ya kumuua mkewe Bi Mboni Patrick (28) kutokana na wivu wa kimapenzi.
Kwa mujibu wa kamanda wa Polisi mkoani Pwani kamishna Msaidizi Mwandamizi Ulrich Matei alisema kuwa marehemu walikuwa ni wakulima wa Kijiji cha Gama - Makaani wilayani Bagamoyo.
Kamanda Matei alisema kuwa tukio hilo lilitokea Januari 20 mwaka huu majira ya saa 10 jioni kijijini hapo ambako walikuwa wakifanya shughuli ya kuchoma mkaa.
“Mwinjilisti huyo alimwua mkewe baada ya kutokea wivu wa kimapenzi ndipo alipochukua panga na kumkata kichwani upande wa kulia na kumsababishia majeraha makubwa yaliyosababisha kifo chake,” alisema Kamanda Matei.
Alisema baada ya kumwua mkewe alimfunika kwa magogo sehemu waliyokuwa wakifanyia shughuli zao hizo za kuchoma mkaa kwa ajili ya biashara.
“Baada ya kumwua mkewe alijinyonga umbali wa mita 300 kutoka eneo la tukio,” alisema Kamanda Matei.
Alibainisha kuwa chanzo cha mauaji hayo ni kutokana na wivu wa kimapenzi na kupelekea tukio hilo kutokea ambalo limewasikitisha wananchi wa kijiji hicho.
Mwisho.

MBUNGE KUZIKWA MIONO

Na John Gagarini, Pwani
MBUNGE wa Jimbo la Chalinze Wilayani Bagamoyo mkoani Pwani Bw Said Bwanamdogo ambaye alifariki dunia asubuhi Januari 22 mwaka huu katika hospitali ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu ya tatizo la ugonjwa wa tumbo kwa miaka mitatu anatarjiwa kuzikwa Januari 24 Kijijini kwao Miono wilayani humo.
Akitoa tarifa juu ya msiba huo huko Makondeko msemaji wa familia ambaye ni baba mdogo wa marehemu Bw Omary Nguya alisema kuwa msiba huo utahudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Kikwete ambaye yuko ziarani nchini Uholanzi.
Bw Nguya alisema mazishi hayo yalikuwa yafanyike Januari 23 lakini yalisogezwa mbele ili kumsubiri Rais ambaye baada ya kupata taarifa aliomba mazishi yahairishwe hadi siku ya Ijumaa ambapo mwili wa marehemu utasafirishwa Ijumaa asubuhi kwenda Kijijini kwake Miono.
 “Marehemu alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa tumbo kwa muda mrefu hali iliyosababisha kuanzishiwa matibabu nchini India ambapo mbali ya jitihada zilizofanywa na madaktari hazikuweza kufanikiwa ambapo marehemu alfariki dunia asubuhi Januari 22 akiwa hospitali ya Muhimbili kwa matibabu na marehemu ameacha watoto sita,” alisema Bw Nguya.
Kwa upande wake Katibu wa CCM Mkoani Pwani Bi Sauda Mpambalioto alisema wamepokea msiba huo kwa mshtuko mkubwa na kukiri kubadilishwa kwa siku ya mazishi.
“Mbali ya msiba huo pia jana Januari 21 tumemzika mjumbe wa halmashauri kuu CCM Taifa (MNEC) kupitia wilaya ya Mkuranga Bi Rukia Msumi ambaye alipata ajali ya pikipiki ambayo ilisababisha kifo chake,” alisema Mpambalioto.
Naye mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Bw Silvestry Koka alisema msiba huo ni pigo kwake kwani walikuwa karibu na marehemu kwa kushirikiana kikazi na kupeana mawazo ya kiutendaji.
Alisema Bwanamdogo alikuwa ni mtu mcheshi ,msikivu ,asiye na majivuno ,alipenda kuzungumza na kila rika pasipo kuwa na majivuno hali inayomfanya awe na kitu cha kuiga kwake.
Kwa upande wake mbunge wa zamani wa Jimbo la Kibaha ambaye kwasasa ni katibu mwenezi mkoani Pwani Dkt Zainab Gama alisema sifa za mbunge wa Chalinze ni nyingi, lakini cha kujivunia kwake ni uadilifu na ucheshi aliokuwa nao.
Dkt Gama alisema enzi za uhai wake atakumbukwa kwa utendaji kazi na kutokuwa mbaguzi kwa wengine.
Mwisho
 
MAENEO YANAUZWA

Maeneo yanauzwa hekari  2,000 liko Mikese kilomita 2 barabara kuu lina hati linauzwa m 400, hekari 1,000 liko Chalinze, liko barabarani  lina hati bei m 500, hekari 900 liko Soga Kibaha lina hati b 3.15, hekari 200 zinauzwa ziko Zogowale km 8 toka barabara kuu ya Moro halina hati linauzwa m 60, hekari 11 na hosteli liko Miembe Saba umbali wa km 1 kutoka barabara kuu ya Moro lina hati m 400, hekari 4 na nyumba zinauzwa liko Kibamba barabarani hati zipo m 400, hekari 100 liko Kwala km 25 kutoka barabara kuu halina hati m 40, hekari 100 liko Mbwawa km 10 toka barabara kuu,  hekari 38 liko Mpiji  lina hati m 133, hekari tano liko Misugusugu barabarani lina hati m 600, hekari 30 liko Misugusugu km 8 toka barabara kuu lina hati m 375, hekari 6 liko Miembe Saba km 2.5 toka barabara kuu halina hati m 100, hekari 6 liko Miembe Saba liko barabarani lina hati m 400, hekari 40 liko Mlandizi km 8 toka barabara kuu lina hati m 400, hekari 9 liko Chalinze liko barabarani lina hati m 400, hekari 11 liko Miembe Saba  km 4 toka barabara kuu lina hati m 35, hekari 20 liko Viziwaziwa/ Kibaha Kwa Mfipa halina hati m 40, hekari 30 liko Kumba Kwa Mfipa km 7 toka barabara kuu halina hati lianuzwa m 60. Kwa mawasiliano piga simu namba 0783 989168, 0754 393118 au 0656 046424.