Na John Gagarini, Kibaha
BONDIA Zumba Kukwe wa Maili Moja wilayani Kibaha mkoani Pwani leo
anatarajiwa kushuka ulingoni kupambana na Baraka Nuhu wa Chalinze
wilayani Bagamoyo kwenye ukumbi wa Ndelema Inn uliopo Chalinze.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi jana mjini Kibaha Kukwe
maarufu kama Lazima Ukae au Mzee wa Uganda alisema kuwa amejiandaa
vema na pambano hilo na anatarajia kuibuka na ushindi kwenye pigano
hilo ambalo ni la kirafiki la uzito wa kati la raundi nane.
Mzee wa Uganda alisema kuwa tangu alivyotoka nchini Uganda Oktoba
kupambana na bondia Badru Lusambya ambapo alitoka sare, amekuwa kwenye
mazoezi makali chini ya mwalimu wake Gaudence Oyaga.
“Nimejiandaa vizuri na ninatarajia kufanya vema kwenye pambano hili
licha ya kwamba mpinzani wangu sijamfahamu vizuri lakini mashabiki
wangu wasiwe na wasiwasi kwani lazima niwakilishe vizuri na naamini
kuwa lazima akae,” alisema Mzee wa Uganda.
Aidha alisema kuwa mchezo alilocheza nchini Uganda umempa uzoefu
mkubwa kwani ameweza kupata mbinu mpya za kupigana na bondia huyo wa
Uganda ambaye anaishi nchini Uingereza, hivyo anaamini kuwa ushindi ni
lazima.
Mbali ya pambano hilo lililoandaliwa na Mama Ndelema Intertainmet na
Shumbili Promotion kutakuwa na mapambano mengine kati ya Mwaite Juma
na Adam Mustapha, Shani Jaribu na Dula Kiroba, Singa Angokile na Juma
Shumbili.
Mapambano mengine ni ati ya Osama Kaongwa na Mustapha Tozo, Alex Kado
na Juma Soja, Issa Mawe na Khalid Hongo, Ismail Tembo na Bodi
Kitongoji, Salehe Mkalekwa na Jumanne Mvuteni, mgeni wa pambano hilo
anatarajiwa kuwa diwani wa Bwiringu Nasir Karama.
Mwisho.
Monday, November 25, 2013
Tuesday, November 5, 2013
WAFA KWA MATUKIO TOFAUTI
Na John Gagarini, Kibaha
Jeshi la Polisi Mkoani Pwani linamshikilia Zaina Selemani umri miaka 14 mkazi wa Kitongoji cha Janga tarafa ya Mlandizi Wilaya ya Kibaha kwa tuhuma za mauaji ya mtoto wake aitwaye Mariam Stamili mwenye miezi tisa.
Jeshi la Polisi Mkoani Pwani linamshikilia Zaina Selemani umri miaka 14 mkazi wa Kitongoji cha Janga tarafa ya Mlandizi Wilaya ya Kibaha kwa tuhuma za mauaji ya mtoto wake aitwaye Mariam Stamili mwenye miezi tisa.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Pwani Kamishina Msaidizi Ulrich Matei amethibitisha kutokea
kwa tukio hilo na ameeleza kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo mnamo tarehe
21/10/2013 majira ya saa 00:00 usiku kwa kumnywesha vitu vinavyosadikiwa kuwa
ni sumu ya panya huko Kata ya Janga mtoto wake huyo.
Kamanda
Matei ameongeza kuwa kifo cha mtoto huyo hapo awali ilidaiwa kuwa kilitokana na
kusumbuliwa na maradhi ya degedege hali iliyopelekea familia yake na majirani
kuamini hivyo na kupelekea taratibu zingine za mazishi kufanyika.
Kamanda
Matei ameongeza kuwa siku ya tukio, baada ya mzazi wa mtoto huyo kununua sumu
hiyo alimnyeshwa mtoto wake na baada ya kuona hali yake imebadilika na kuwa
mbaya alimpigia simu mume wake Stamili Shabani umri miaka 21 na kumweleza kuwa mtoto
wao anasumbuliwa na ugonjwa wa degedege hivyo wampeleke kwa mganga wa kienyeji.
Ameongeza
kuwa baada ya mume wake kurejea nyumbani walimchukua motto huyo na kumpeleka
kwa mganga huko Kijiji cha Disunyara ambapo marehemu alianza kupatiwa matibabu
lakini hata hivyo kutokana na hali yake kuzidi kuwa mbaya walimchukua mtoto
huyo na kwenda nae kituo cha afya Mlandizi ambapo alipoteza maisha siku ya
tarehe 21/102013 majira ya saa 00:00 usiku.
Baada
ya kutokea kwa kifo hicho mwili wa marehemu ulichukuliwa na ndugu zake na
kuzikwa majira ya saa 17:00 jioni huko Kijiji cha Kilangalanga, lakini hata
hivyo baada ya kumalizika kwa mazishi hayo mtuhumiwa wa mauaji hayo usiku wa
kuamkia tarehe 23/10/2013 alianza kulia
na kumwambia mume wake huyo kuwa mtoto wao hakufa kwa ugonjwa wa degedege ila
alikuwa amemnywesha sumu hivyo kumuomba amsamehe.
Mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma dhidi
yake mara baada ya upelelezi kukamilika.
Katika
tukio jingine mnamo tarehe 03/11/2013, majira ya saa za 6.30 usiku huko Kijiji
cha Mindutulieni Kata ya Talawanda Tarafa ya Chalinze (W) Bagamoyo (M) Pwani. Said Mbena miaka 30, mbena, mkulima
mkazi wa Kijiji cha Mindutulieni aliuawa kwa kupigwa na fimbo sehemu mbalimbali
za mwili na Machocho Matei miaka 35, mmasai, mfugaji, mkazi wa Kijiji cha
Mindutulieni baada ya kutokea ugomvi kati yao wakiwa kwenye sherehe za ngoma za
kienyeji nyumbani kwa Asha Rashid. Mtuhumiwa baada ya kukamatwa akiwa njiani
kupelekwa katika ofisi ya Kijiji cha Mindutulieni kabla ya kufikishwa katika
ofisi hiyo aliuawa na wananchi waliojichukulia sheria mkononi. Miili ya
marehemu ya marehemu imehifadhiwa katika ofisi ya Kijiji hicho ikisubiri
kufanyiwa uchunguzi na Daktari.
Aidha
mnamo tarehe 02/11/2013, majira ya saa za 9.00 usiku huko Kitongoji cha
Mlandizi Kati Kata ya Mlandizi Tarafa ya Mlandizi Wilaya ya Kibaha (M) Pwani. Mtu mmoja aliyefahamika kwa
jina moja la Kingstone umri kati ya miaka 30-35, mkulima mkazi wa Mlandizi
aliuawa na mtu / watu wasiofahamika kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali
sehemu ya mguu wa kushoto kwenye maungio ya goti, hali iliyosababisha damu
nyingi kuvuja na kusababisha kifo chake. Mwili wa marehemu umehifadhiwa chumba
cha maiti Hospitali ya Tumbi Kibaha ukisubiri kufanyiwa uchunguzi na Daktari /
kutambuliwa na ndugu.
Kadhalika
Kamanda Matei ameeleza kuwa mnamo tarehe
02/11/2013, majira ya saa za 4.00 asubuhi huko Kijiji cha Kazimzumbwi Kata ya
Kisarawe Tarafa ya Sungwi barabara ya Dar es Salaam - Kisarawe (W) Kisarawe (M) Pwani. Gari Na. T.762 BSB
aina ya Noah likiendeshwa na Dereva asiyefahamika akitokea Dar es Salaam kwenda
Msanga aligongana uso kwa uso na pikipiki Na. T.219 BUM aina Fekon iliyokuwa
ikiendeshwa na Sixbert Ngatunga miaka 36, mkazi wa Kazimzumbwi akitokea Kisanga
kwenda Kazimzumbwi. Katika ajali hiyo dereva wa pikipiki alifariki dunia papo
hapo. Mwili wa marehemu umefanyiwa uchunguzi na Daktari na kukabidhiwa ndugu
kwa mazishi. Chanzo cha ajali ni mwendo kasi wa dereva wa Gari Na. T.762 BSB
aina ya Noah.
Monday, October 28, 2013
KIPOZI NA ELIMU
Na John Gagarini, Bagamoyo
WILAYA ya Bagamoyo mkoa Pwani imeweka mkakati wa kuhakikisha
wanafunzi wote waliopata nafasi ya kwenda sekondari wilayani humo wanakwenda
shule na kuondokana na dhana kuwa mkoa huo hauna mwamko wa elimu.
Hayo yalisemwa na mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Bw Ahmed Kipozi wakati
wa mahafali ya 22 ya shule ya sekondari ya Lugoba na kusema kuwa tayari
wameshakutana na wadau mbalimbali yakiwemo mashirika yasiyo ya kiserikali na
wazazi ili kufanikisha suala hilo.
Kipozi alibainisha kuwa moja ya mkakati huo ni ule wa ujenzi
wa hosteli kwenye baadhi ya maeneo ili kuwapunguzia umbali wanafunzi ambapo
moja ya changamoto imeonyesha kuwa umbali nao umekuwa chanzo cha wanafunzi
kutopenda shule.
“Kwa sasa tumeunganisha nguvu ya pamoja na wadau wa elimu
ndani ya wilaya ili kuhakikisha malengo ya watoto kwenda shule kwa kiwango
kikubwa yanafikiwa ambapo washikadau wametuunga mkono na tunaamini mabadiliko
yanaonekana kama leo unavyoona watoto wengi wamemaliza elimu yao ya sekondari,”
alisema Bw Kipozi.
Awali mwalimu mkuu wa wa shule hiyo Bw Alhaj Abdalla Sakasa
alisema kuwa anaomba wadau wa elimu kujitokeza kuwasaidia kupata fedha kwa
ajili ya kugharamia vifaa vya maabara na kemikali kwa ajili ya wanafunzi wa
kidato cha nne na cha sita kwani gharama ni kubwa sana.
Alhaj Sakasa alisema kuwa shule yake ina wanafunzi wengi wa
masomo ya Sayansi hivyo kufanya maandalizi ya na kuendesha mitihani hiyo ya
kitaifa kutumia gharama kubwa ambazo kwa sasa hawana.
“Gharama kwa wanafunzi wa kidato cha nne ni shilingi milioni
5.8 na kidato cha sita ni shilingi milioni 7 ambazo hadi sasa hatuna licha ya
kuwa serikali inatoa ruzuku lakini ni kidogo sana ukilinganisha na gharama halisi,” alisema
Alhaj Sakasa.
Aidha alisema kuwa wazazi wengi hawana uwezo wa kulipia
chakula kama ilivyoamuriwa ambapo kila mwanafunzi anapaswa kuchangia kiasi cha
shilingi 100,000 kwa muhula ambazo wazazi wanshindwa kulipa.
Aliongeza kuwa wanampongeza mlezi wa shule hiyo Bw Subbash
Patel kwa kuisaidia shule na watumishi wa shule ambapo aliwasaidia vifaa vya
ujenzi na baadhi wamefanikiwa kujenga nyumba zao za kuishi, Katika mahafali
hayo jumla ya wanafunzi 212 walipewa vyeti vya kuhitimu kidato cha nne ambapo
shule hiyo ina wanafunzi 1,228 na walimu 57.
Mwisho.
Thursday, September 19, 2013
MATUKIO MBALIMBALI YA PWANI
Na
Mwandishi Wetu, Kibaha
IMEBAINIKA
kuwa uwepo wa mabanda ya kuonyeshea video mitaani ambayo hayapo kisheria
kumechangia vitendo vya ubakaji na ulawiti wa watoto wadogo ambao ni wanafunzi
wa shule za msingi wilayani Kibaha mkoani Pwani.
Kwa
mujibu wa uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa habari hizi mjini Kibaha
umebaini kuwa watoto hao wamekuwa wakifanyiwa vitendo hivyo nyakati za usiku
wanapokuwa wamekwenda kuangalia video ambapo waonyeshaji wa video hizo
huonyesha picha chafu za ngono.
Mabanda
hayo ambayo mengi yamejengwa kwa mbao au mifuko ya sandarusi na kuezekwa na
makuti au nyasi na yasiyo na mvuto yamekuwa yakionyesha picha hizo maarufu kama
pilau, kachumbari na ubwabwa na majina mengine ambayo kwa mtu wa kawaida si
rahisi kujua maana yake.
Baadhi
ya wakazi ambao wamelaani uwepo wa mabanda hayo ambayo huanza kuonyesha video
majira ya asubuhi hadi usiku na kusababisha baadhi ya wanafunzi kushinda humo
huku wakiwa wameaga wanakwenda shule na kuishia humo na endapo wazazi
hawatafuatilia kuna hatari ya mwanafunzi huyo kutohudhuria darasani kabisa.
Walimwelezea
mwandishi wa habari hizi kuwa njia wanazotumia wabakaji hao ni kuwalipia
kiingilio cha kuangalia picha ambacho ni shilingi mia tano kwa filamu
ziltakazoonyeshwa kwa siku hiyo ambazo huonyeshwa kwa awamu na huchukua kila
awamu zaidi masaa matatu kisha kubadili picha zingine.
Picha
zinapokuwa zinaendelea mara hubadili na kuweka picha chafu za ngono hivyo
kuhamasisha vitendo hivyo na kwa kuwa vijana hao wanaobaka watoto wanakuwa
wamewalipia kiingilio huwachukua na kuwapakata watoto hao na wanapokuwa
wamepandwa na msisimko huanza kuwaingilia watoto hao hadi wanapomaliza haja
zao.
“Mara
wamalizapo haja zao huwapa fedha kwa ajili ya kuwataka wasiseme kwa wazazi wao
ambapo watoto hao baadaye huzoea na kujikuta kila wakati wakienda kwenye
mabanda hayo na kufanyiwa vitendo hivyo na kuzoea hali ambayo ina waathiri
kisaikolojia na kufanya maendeleo yao shuleni kushuka,” walisema wakazi hao.
Akizungumza
na mwandishi mwalimu mkuu wa shule ya msingi Lulanzi wilayani Kibaha mkoani
Pwani Anna Bilali alisema kuwa wanafunzi wengi wameathiriwa na hali hiyo ambapo
mbali ya kwenda kwenye mabanda hayo mara wasipokwenda shule huandika kazi
walizofanya wenzao kisha kujisahishia ili kuwadanganya wazazi wao.
“Wanafunzi
wa namna hii wamekuwa wakijisahishia madaftari yao lakini sisi tunagundua kwani
usahishaji wao ni tofauti na wa walimu na tunapowaambia baadhi ya wazazi
wamekuwa wakiwatetea watoto wao hali inayosababisha ugumu wa kuwadhibiti kwani
baadhi ya wanafunzi hukaa kwenye mabanda hayo hadi saa tatu usiku bila hata
kuulizwa walikokuwa,” alisema Bilali.
Alisema
pia baadhi yao humiliki simu ambazo wanakwenda nazo shuleni na kuangalia picha
hizo na kujikuta muda mwingi wakiutumia kwa kuangalia picha hizo kupitia simu
ambazo huwa wanazificha na inakuwa vigumu kuwagundua hadi wenzao watoe taarifa.
Aidha
alisema kuwa kuna watu wamekuwa wakiwaonyesha picha hizo kupitia simu kisha
huwatoza kiasi kidogo cha fedha kwa ajili ya kupata huduma hiyo hali amabayo
inaendelea kuongeza kusambaa kwa vitendo viovu.
Kwa
upande wake mkuu wa mkoa wa Pwani Mwantumu Mahiza alisema kuwa udhibiti wa
mitandao kama hiyo ya uonyeshaji wa picha za ngono ni viongozi wa mtaa na
vijiji kwa kuwachukulia hatua kwani hayako kisheria hivyo hayana sababu ya
kuwepo ili kuondoa tatizo hilo.
Hivi
karibuni wanafunzi wanne wa shule ya msingi Lulanzi walikamatwa na polisi
wilayani Kibaha kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi mwenzao wa darasa la pili
mwenye umri wa miaka tisa na kumsababishia maumivu makali na kulazwa hospitali
ya Tumbi ambapo aliruhusiwa kutoka wiki iliyopita baada ya kupata matibabu.
Mwisho.
Na Mwandishi Wetu,
Kibaha
MKUU wa mkoa wa
Pwani Mwantumu Mahiza amewashukia maofisa ugani na kusema kuwa hatasita
kuwaondoa kwa kushindwa kutekeleza wajibu wao na kudai maslahi na vitendea kazi
huku uwajibikaji wao ukiwa chini hali inayowafanya washindwe kuwaletea
mabadiliko wakulima.
Mahiza aliaysema
hayo jana mjini Kibaha alipokuwa akizungumza na madiwani, wenyeviti, watendaji
na wataalamu wa mitaa na kata kwenye mji wa Kibaha, wakati mkutano wa kujadili
changamoto na mafanikio kupitia mpango wa matokeo makubwa kwa sasa.
Alisema kuwa
maofisa ugani wengi mkoani Pwani wamakuwa hawawajibiki na kukaa tu huku
wakifikiri wamekwenda kutalii ndani ya mkoa huo huku wakulima wakiwa hawana
msaada wowote licha ya kulima bila ya kupatiwa stadi za kilimo bora.
“Mimi mwenyewe
nimelima mashamba ya mazao mbalimbali lakini hakuna ofisa ugani hata mmoja
ambaye aliweza kunitembelea kunipa ushauri wa kitaalamu sembuse mkulima wa
kawaida ni jambo la kushangaza sana hakuna anayejishughulisha hali hii
haikubaliki hata kidogo tutawaondoa wale watakaoshindwa kutimiza wajibu wao,”
alisema Mahiza.
“Kama kuna ofisa
ugani ambaye alimtembelea mkulima na kumpa ushauri wa kitaalamu asimame hakuna
hata mmoja aliyefanya hivyo je mnafanya nini kama hamuwezi kazi ni vema
mkaondoka mkafanye kazi sehemu nyingine lakini hapa kwangu sitakubali watu
wasiowajibika,” alisema Mahiza.
Aidha alisema
anashangazwa na maofisa hao kushindwa kuwa na eneo kwa ajili ya hata kulima
bustani ya mchicha ili kuonyesha mfano ambapo kiongozi anapaswa kuwa mfano kwa
wale anaowaongoza si kukaa tu.
“Sasa hivi mnaomba
usafiri wa kwenda wapi wakati uwajibikaji ni mdogo mtapewa pikipiki mtadai
mafuta baadaye mtadai gari kisha dereva lakini utendaji kazi hauonekani itakuwa
haisaidii mnapaswa kuwajibika ndipo mdai haki kwani huwezi kudai haki wakati
hauwajibiki,” alisema Mahiza.
Aliongeza kuwa
maofisa hao hakuna hata mmoja mwenye daftari la kujua idadi ya wakulima au
mpango kazi wa mwaka mzima kujua atafanya nini sasa ataweza vipi kutekeleza
majukumu yake bila ya kujua masuala mazima ya wakulima.
“Kutokuwa makini
kunasababisha kupikwa kwa takwimu sisi tunachotaka hali halisi na si
kutengeneza pia mkumbuke mwaka juzi tuliwaomba mipango kazi ya kata zenu
mlituletea lakini cha kushangaza hamjatekeleza hata jambo moja,” alisema
Mahiza.
Aliwataka
watendaji wa sekta mbalimbali kuwajibika kwa nafasi zao na si kukaa tu pia
watembee wasikae ofisini badala yake wawatembelee wananchi kujua mahitaji yao
na kuachana na tabia ya kutengeneza takwimu mezani bali wajionee hali halisi.
Mwisho.
Na Mwandishi Wetu,
Kibaha
KIJANA aitwaye
Ibrahimu Jumapili (30)mkazi wa Kongowe wilayani Kibaha mkoani Pwani amekufa kwa
kujinyonga kwa kutumia kanga kwenye mti wa mkorosho.
Kwa mujibu wa
mwenyekiti wa mtaa wa Bamba wilayani Kibaha Amry Mavala alisema kuwa marehemu
hakuweza kuacha ujumbe wowote wa sababu ya kuchukua maamuzi hayo ya
kujiua.
Mavala alisema
kuwa tukio hilo lilitokea Septemba 17 mwaka huu majira ya saa 6:30 mchana
kwenye mtaa wa Bamba kata ya Kongowe wilayani humo.
“Marehemu alikuwa
akijishughulisha na kazi ya ufayatuaji matofali na kabla ya kifo chake alikuwa
akilalamika kuwa kuna watu walikuwa wakitaka kumtoa kafara,” alisema Mavala.
Alisema kuwa
kutokana na hali hiyo marehemu alisema kuwa anamwachia Mungu na itambidi arudi
nyumbani kwao mkoani Singida ili ajinusuru na hali hiyo.
Kwa upande wake
kaimu kamanda wa polisi mkoani Pwani Juma Ali alisema kuwa mwili wa marehemu
ulikutwa ukininginia kwenye mkorosho kwenye shamba la Mzee Rafael.
Ali alisema kuwa
chanzo cha kifo chake hakijaweza kufahamika na mwili wa marehemu uko kwenye
hospitali ya Tumbi kwa ajili ya uchunguzi wa daktari na taratibu za mazishi.
Wakati huo huo
mwili wa mtu asiyefahamika umeokwotwa huko kwenye mtaa wa Kwa Mathiasi wilayani
Kibaha ukiwa umeharibika vibaya ambapo ulikutwa na jeraha shingoni na mtu mmoja
anashikiliwa kuhusiana na tukio hilo, na mwili huo ulizikwa hapo hapo baada ya
kushindwa kuhamishwa.
Mwisho.
Na Mwandishi Wetu,
Kibaha
WATU sita
wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Pwani wakiwemo wawili wanaodai
kuwa ni askari polisi kwa tuhuma za kukutwa na nguo zinazosadikiwa kuwa ni za
magendo kutokea nchini Kenya.
Akizungumza na
waandishi wa habari ofisini kwake jana kaimu kamanda wa polisi mkoani humo Juma
Ali alisema kuwa watuhumiwa walikamatwa na gari lililokuwa limebeba nguo za
kike na kiume.
Ali alisema kuwa
tukio hilo lilitokea jana majira ya saa 9 alfajiri eneo la Vigwaza wilayani
Bagamoyo kwenye kizuizi wakati askari wakiwa doria kwenye barabara ya Dar es Salaam
Chalinze.
Alisema kuwa
watuhumiwa wawili ambao ndiyo walikuwa kwenye gari aina ya Fuso lenye namba za
usajili T 303 BAY lenye mzigo huo lilikuwa likiendeshwa na Omary Salehe (66)
mkazi wa Arusha na utingo Fuwad Salimu (46) mkazi wa Moshi.
“Wakati gari hiyo
ikiwa inaendelea na safari yake ilikuwa ikifukuzwa kwa kasi ilipofika Mbwewe na
gari nyingine aina ya NOAH yenye namba za usajili T 641 CCH ikiwa na watu wanne
wakiwemo watu hao wawili ambao bado hawajathibitishwa kama ni polisi kutokea
mkoani Tanga au la huku mwingine akiwa askari mstaafu na mtu mwingine,” alisema
Ali.
Aidha alisema kuwa
wanaendelea na uchunguzi juu ya kujua thamani ya mzigo huo na kuwatambua watu
hao kama ni askari kweli au la ili hatua sahihi ziweze kuchukuliwa ambapo
magari hayo bado yanashikiliwa na watuhumiwa wanahojiwa kupata ukweli.
Mwisho.
Na Mwandishi Wetu,
Kibaha
MTU mmoja mkazi wa
Kongowe Joseph John (17) anashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za
kumlawiti mwanafunzi (jina tunalo).wa shule ya Msingi Kongowe mwenye umri wa
miaka 11.
Akizungumza na
waandishi wa habari shangazi wa mtoto huyo Rukia Bora alisema kuwa alimgundua
mtoto huyo kuingiliwa baada ya kulalamika kuwa anasikia maumivu shemu za haja
kubwa.
Bora alisema kuwa
alimgundua mtoto huyo wa mdogo wake wa kiume kuingiliwa Septemba 12 mwaka huu.
Alisema kuwa baada
ya kumhojia alimwelekeza alipokuwa akifanyiwa mchezo huo kwa muda sasa ambapo
ni karibu miezi mitatu iliyopita tangu kuanza kufanyiwa hivyo na mtuhumiwa na
watu wengine ambao walikimbia na bado wanatafutwa.
“Huyu mtoto
anaishi na bibi yake lakini kwa kuwa mimi na bibi yake tuko jirani hapa Kongowe
Kati wakati mwingine anakuja kwangu hivyo tunamlea kwa pamoja ambapo baba yake
yuko Jijini Dar es Salaam na mke we waliasha achana lakini kutokana na tabia za
mtoto za utundu udhibiti wake ulikuwa mgumu,” alisema Bora.
Aidha alisema kuwa
baada ya kumhoji alikataa kusema ikabidi wampeleke polisi na baada ya kubanwa
ilibidi aseme ukweli na kueleza kila kitu.
“Alisema kuwa
chumba (Ghetto) alichokuwa akifanyiwa mchezo huo wanaishi vijana watupu ambao
wanajihusisha na uimbaji kwenye shghuli mbalimbali za sherehe, ambapo walikuwa
wakimwingilia kwa nyakati tofauti muda wa usiku na kumwambia asiseme kwa mtu
yoyote,” alisema Bora.
Alibainisha kuwa
chanzo cha yeye kujua hilo ni baadhi ya majirani kuona kuwa mtoto huyo kuwa
karibu na mtuhumiwa hali ilyowatia shaka majirani.
“Baada ya kugundua
nilimfuata mtuhumiwa na kumkamata na kumpeleka polisi hata hivyo watuhumiwa
wengien wawili walikimbia ambapo jana watoto wawili ambao nao walikuwa
wakimfanyia hivyo walipelekwa polisi kuhojiwa na kinachosubiriwa ni mtoto huyo
kwenda kuwatambua,” alisema Bora.
Alisema kwa sasa
mtoto huyo anaendelea kupatiwa matibabu kwenye hospitali ya Tumbi.
Kwa upande
wake kaimu kamanda wa polisi mkoani Pwani Juma Ali alisema kuwa mbali ya
mtuhumiwa huyo watuhumiwa wengine walikimbia na wanaendelewa kutafutwa.
Ali alisema
kwa sasa kinachosubiriwa ni gwaride la utambulisho wa watuhumiwa wawili wadogo
ambao ni wanafunzi ili nao waunganishwe na mtuhumiwa wa kwanza.
Mwisho.
Wednesday, September 18, 2013
AFA KWA KUJINYONGA AKIDAI KUTAKA KUTOLEWA KAFARA
Na John Gagarini, Kibaha
KIJANA aitwaye Ibrahimu Jumapili (30)mkazi wa Kongowe
wilayani Kibaha mkoani Pwani amekufa kwa kujinyonga kwa kutumia kanga kwenye
mti wa mkorosho.
Kwa mujibu wa mwenyekiti wa mtaa wa Bamba wilayani Kibaha
Amry Mavala alisema kuwa marehemu hakuweza kuacha ujumbe wowote wa sababu ya
kuchukua maamuzi hayo ya kujiua.
Mavala alisema kuwa tukio hilo lilitokea Septemba 17 mwaka
huu majira ya saa 6:30 mchana kwenye mtaa wa Bamba kata ya Kongowe wilayani
humo.
“Marehemu alikuwa akijishughulisha na kazi ya ufayatuaji
matofali na kabla ya kifo chake alikuwa akilalamika kuwa kuna watu walikuwa
wakitaka kumtoa kafara,” alisema Mavala.
Alisema kuwa kutokana na hali hiyo marehemu alisema kuwa
anamwachia Mungu na itambidi arudi nyumbani kwao mkoani Singida ili ajinusuru
na hali hiyo.
Kwa upande wake kaimu kamanda wa polisi mkoani Pwani Juma Ali
alisema kuwa mwili wa marehemu ulikutwa ukininginia kwenye mkorosho kwenye
shamba la Mzee Rafael.
Ali alisema kuwa chanzo cha kifo chake hakijaweza kufahamika
na mwili wa marehemu uko kwenye hospitali ya Tumbi kwa ajili ya uchunguzi wa
daktari na taratibu za mazishi.
Wakati huo huo mwili wa mtu asiyefahamika umeokwotwa huko
kwenye mtaa wa Kwa Mathiasi wilayani Kibaha ukiwa umeharibika vibaya ambapo
ulikutwa na jeraha shingoni na mtu mmoja anashikiliwa kuhusiana na tukio hilo,
na mwili huo ulizikwa hapo hapo baada ya kushindwa kuhamishwa.
Mwisho.
Na John Gagarini, Kibaha
WATU sita wanashikiliwa
na jeshi la polisi mkoani Pwani wakiwemo wawili wanaodai kuwa ni askari polisi kwa
tuhuma za kukutwa na nguo zinazosadikiwa kuwa ni za magendo kutokea nchini
Kenya.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana kaimu
kamanda wa polisi mkoani humo Juma Ali alisema kuwa watuhumiwa walikamatwa na
gari lililokuwa limebeba nguo za kike na kiume.
Ali alisema kuwa tukio hilo lilitokea jana majira ya saa 9
alfajiri eneo la Vigwaza wilayani Bagamoyo kwenye kizuizi wakati askari wakiwa
doria kwenye barabara ya Dar es Salaam Chalinze.
Alisema kuwa watuhumiwa wawili ambao ndiyo walikuwa kwenye
gari aina ya Fuso lenye namba za usajili T 303 BAY lenye mzigo huo lilikuwa likiendeshwa
na Omary Salehe (66) mkazi wa Arusha na utingo Fuwad Salimu (46) mkazi wa Moshi.
“Wakati gari hiyo ikiwa inaendelea na safari yake ilikuwa
ikifukuzwa kwa kasi ilipofika Mbwewe na gari nyingine aina ya NOAH yenye namba
za usajili T 641 CCH ikiwa na watu wanne wakiwemo watu hao wawili ambao bado
hawajathibitishwa kama ni polisi kutokea mkoani Tanga au la huku mwingine akiwa
askari mstaafu na mtu mwingine,” alisema Ali.
Aidha alisema kuwa wanaendelea na uchunguzi juu ya kujua
thamani ya mzigo huo na kuwatambua watu hao kama ni askari kweli au la ili
hatua sahihi ziweze kuchukuliwa ambapo magari hayo bado yanashikiliwa na
watuhumiwa wanahojiwa kupata ukweli.
Mwisho.
Na John Gagarini, Kibaha
MTU mmoja mkazi wa Kongowe Joseph John (17) anashikiliwa na
jeshi la polisi kwa tuhuma za kumlawiti mwanafunzi (jina tunalo).wa shule ya
Msingi Kongowe mwenye umri wa miaka 11.
Akizungumza na waandishi wa habari shangazi wa mtoto huyo
Rukia Bora alisema kuwa alimgundua mtoto huyo kuingiliwa baada ya kulalamika
kuwa anasikia maumivu shemu za haja kubwa.
Bora alisema kuwa alimgundua mtoto huyo wa mdogo wake wa
kiume kuingiliwa Septemba 12 mwaka huu.
Alisema kuwa baada ya kumhojia alimwelekeza alipokuwa
akifanyiwa mchezo huo kwa muda sasa ambapo ni karibu miezi mitatu iliyopita
tangu kuanza kufanyiwa hivyo na mtuhumiwa na watu wengine ambao walikimbia na bado
wanatafutwa.
“Huyu mtoto anaishi na bibi yake lakini kwa kuwa mimi na bibi
yake tuko jirani hapa Kongowe Kati wakati mwingine anakuja kwangu hivyo
tunamlea kwa pamoja ambapo baba yake yuko Jijini Dar es Salaam na mke we
waliasha achana lakini kutokana na tabia za mtoto za utundu udhibiti wake
ulikuwa mgumu,” alisema Bora.
Aidha alisema kuwa baada ya kumhoji alikataa kusema ikabidi
wampeleke polisi na baada ya kubanwa ilibidi aseme ukweli na kueleza kila kitu.
“Alisema kuwa chumba (Ghetto) alichokuwa akifanyiwa mchezo
huo wanaishi vijana watupu ambao wanajihusisha na uimbaji kwenye shghuli
mbalimbali za sherehe, ambapo walikuwa wakimwingilia kwa nyakati tofauti muda
wa usiku na kumwambia asiseme kwa mtu yoyote,” alisema Bora.
Alibainisha kuwa chanzo cha yeye kujua hilo ni baadhi ya
majirani kuona kuwa mtoto huyo kuwa karibu na mtuhumiwa hali ilyowatia shaka
majirani.
“Baada ya kugundua nilimfuata mtuhumiwa na kumkamata na
kumpeleka polisi hata hivyo watuhumiwa wengien wawili walikimbia ambapo jana
watoto wawili ambao nao walikuwa wakimfanyia hivyo walipelekwa polisi kuhojiwa
na kinachosubiriwa ni mtoto huyo kwenda kuwatambua,” alisema Bora.
Alisema kwa sasa mtoto huyo anaendelea kupatiwa matibabu
kwenye hospitali ya Tumbi.
Kwa upande wake kaimu
kamanda wa polisi mkoani Pwani Juma Ali alisema kuwa mbali ya mtuhumiwa huyo
watuhumiwa wengine walikimbia na wanaendelewa kutafutwa.
Ali alisema kwa sasa
kinachosubiriwa ni gwaride la utambulisho wa watuhumiwa wawili wadogo ambao ni
wanafunzi ili nao waunganishwe na mtuhumiwa wa kwanza.
Mwisho.
Thursday, September 12, 2013
NAGU ANZISHENI UZALISHAJI SUKARI
Na John Gagarini, Bagamoyo
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji Mary
Nagu ameitaka kampuni ya Eco Energy ya wilayani Bagamoyo mkoani Pwani kuendelea
na mchakato wa kufungua kiwanda cha kuzalishia sukari ili kukabiliana na
upungufu wa bidhaa hiyo hapa nchini.
Aliyasema hayo juzi alipotembelea kampuni hiyo ili kuona
maendeleo ya mradi wa kilimo cha miwa kwenye kijiji cha Razaba wilayani humo na
kusema kuwa mara kiwanda hicho kitakapoanzishwa kitasaidia kukabiliana na
upungufu huo.
Nagu alisema kuwa kiasi kikubwa cha sukari inayotumika
inatoka nje ya nchi hali ambayo inayaosababisha bei ya bidhaa hiyo kuwa juu
ambapo uzalishaji ungeanza ungekuwa mkombozi kwa Watanzania.
“Tunajua mnakabiliwa na changamoto nyingi lakini ni vema
mkaanza kutekeleza mradi huu ili kukabiliana na changamoto ya upungufu wa
sukari ambapo uzalishaji huo utaambatana na mazo mengine ikiwemo umeme, mafuta
ya mitambo ya Ethanol na mbolea,” alisema Nagu.
Aidha alisema kuwa serikali itahakikisha inaweka mazingira
mazuri kwa wawekezaji ili waweze kutekeleza miradi yao ambayo pia ina faida
kubwa kwa wananchi kama ilivyo kwa mradi huo ambao utainufaisha nchi ambayo inamiliki
asilimia 25 kutokana na ardhi.
“Kwa sasa kuna watu wawili wamefungua kesi kupinga wawekezaji
hao kutokana na kuchukua ardhi kwa ajili ya mradi huu licha ya taratibu za
malipo kufanyika hivyo isiwe sababu ya wao kuchelewa kuanza kutekeleza mradi,”
aliongeza nagu.
Kwa upande wake makamu mwenyekiti wa kampuni hiyo Jonathan
Nkandala alisema kuwa mbali ya kuzalisha sukari tani 150,000 kwa mwaka pia mradi
huo pia utazalisha megawati 25 za umeme, mafuta na mbolea ambapo eneo la mradi
lina ukubwa wa hekta 22,000 huku eneo la miwa lkiwa na ukubw awa hekta 8,000.
Nkandala alisema kuwa umeme utakaozalishwa megawati 14 hadi 15 zitatumika kwenye gridi ya taifa huku
nyingine zikibaki kwenye mradi huo kwa ajili ya kuendeshea mashine na mitambo
mbalimbali ambapo hadi sasa umeshatumia dola milioni 50 na hadi kukamilika
kwake utagharimu kiasi cha shilingi dola milioni 500 na ulianza mwaka 2007 na
unatarajiwa kukamilika 2016.
Mwisho.
Sunday, September 8, 2013
MWANAFUNZI ABAKWA NA WENZAKE
Na John Gagarini, Kibaha
MATUKIO ya uvunjifu wa maadili
kwenye shule mbalimbali hap nchini yameendelea kuharibika baada ya wanafunzi
wanne wa shule ya Msingi Lulanzi wilayani Kibaha mkoani Pwani kutuhumiwa kubaka
mwanafunzi wa darasa la pili (9) na kumsababishia maumivu yalipelekea kulazwa
hospitali ya Tumbi kwa matibabu.
Akizungumza na mwandishi wa
habari hizi jana babu wa mtoto huyo (jina tunalo), Jacob Mrope alisema tukio
hilo lilitokea Septemba 2 majira ya saa 6 mchana, ambapo mjukuu wake ambaye ni yatima, alikuwa
akitoka shuleni huku akiwa na wenzake wawili wakike walikimbizwa na watuhumiwa
hao ambapo yeye alishindwa kukimbia kutokana na kuuumia mguu na kujikuta akikumbana
na dhahma hiyo.
Mrope alisema kuwa wanafunzi
wenzake aliokuwa nao walisema kuwa baada ya watuhumiwa hao kumkamata walimziba
mdomo kisha wakaanza kumuingilia kwa zamu ambapo mwanafunzi huyo hakuweza kupata
msaada wowote hadi watuhumiwa hao kutimiza haja zao.
“Wenzake waliokuwa nao walitoa
taarifa nyumbani kwa mlezi wake ambaye ni dada yake ambapo alikwenda na kumkuta
akitokwa na damu nyingi na alipomuuliza alisema kuwa wenzake wamembaka na
kumchukua na kumpeleka shuleni na kutoa taarifa,” alisema Mrope.
Kwa upande wake dada yake Lwiza
alisema kuwa yeye alipata taarifa kupitia kwa wanafunzi hao ambao walikuwa nao
wakati wanatoka shule na kukimbizwa na watuhumiwa hao, ambapo walisema kuwa
ilibidi warudi na kumkuta mwenzao akitokwa damu na kumkokota mwenzao hadi
nyumba iliyojirani na kumjulisha.
“Alikuwa kwenye hali mbaya kwani
alikuwa akitokwa na damu nyingi na nilipomuuliza alisema kuwa amebakwa na
mtuhumiwa ambaye alimtambua na kumtaja jina mwenye umri wa miaka 10 akiwa na
wenzake watatu,” alisema Lwiza.
Lwiza alisema kuwa baada ya kuona
hali ile walimpeleka shule na uongozi wa shule ukamwelekeza kufuata taratibu za
kisheria ambapo walikwenda serikali ya mtaa kasha kwenda polisi na baadaye
hospitali ya Tumbi kwa matibabu zaidi ambapo hadi juzi mwanafunzi huyo alikuwa
bado kalazwa na hali yake inasemekena kuwa ni mbaya.
Naye mwalimu mkuu wa shule hiyo
ya Lulanzi Anna Bilali alisema kuwa wao kama uongozi wa shule hawawezi kusema
lolote kwani sula hilo liko kwenye vyombo vya sheria pamoja na kitabibu na
watakuwa tayari kusema mara taarifa zitakapokamilika.
“Ni kweli tukio hili limetokea
lakini bado haijathibitishwa kama ni kweli au la na pia lilitokea nje ya shule
na muda wa shule kwa wanafunzi wa madarasa ya chini walisharuhusiwa kurudi
nyumbani mara baada ya masomo kwisha,” alisema Bilali.
Akizungumzia tukio hilo mjumbe wa
mtaa wa Lulanzi Rasul Shaban alisema kuwa walipata taarifa hiyo na kushnagazwa
na kitendo hicho ambapo tukio hilo ni la mara ya kwanza kutokea katika shule
hiyo ambayo iko kwenye mtaa huo na pia walitoa barua za kuwadhamini wanafunzi
wanaotuhumiwa kufanya tukio hilo.
Akithibitisha kutokea kwa tukio
hilo kamanda wa polisi mkoani Pwani Ulrich Matei alisema kuwa hadi sasa
wanawashikilia wanafunzi wanne wenye umri kati ya miaka 10 na 13 kuhusiana na
tukio hilo.
“Wanafunzi hao wanatuhumiwa
kumbaka mwenzao wakati akitoka shule ambapo walimkamata na kumkimbiza kwenye
kichaka na kumziba mdomo ili asiweze kupiga kelele kisha walimshika miguu na
mikono na kumbaka kwa zamu na
kumsababishia maumivu makali ambapo amelazwa hospitali ya Tumbi kwa matibabu
zaidi na hali yake bado haijawa nzuri,” alisema Matei.
Matei alisema kuwa watuhumiwa hao
wanne wanahojiwa juu ya tukio hilo ambapo watafikishwa mahakamani mara
upelelezi utakapokamilika ikiwa ni pamoja na uchunguzi wa daktari kuhusina na
tukio hilo lakusikitisha.
Mwisho.
Subscribe to:
Posts (Atom)