Wednesday, June 7, 2023

SERIKALI YATOA MAAMUZI UENDESHAJI MAGOFU YA KAOLE BAGAMOYO

KUNENGE akiwa Bagamoyo alimuagiza Kamishna Msaidizi wa Ardhi kufuta hati ya upimaji   eneo la Mji Mkongwe uliofanyika ndani   ya eneo la hifadhi kwa kuwa zilitolewa ndani ya GN namba 1983  na kutatua mgogoro wa ardhi eneo la magofu ya Kaole na familia ya Omary Sherdel.

Alimtaka kamishna msaidizi wa ardhi wa mkoa kukamilisha ufuatiliajj kwenye mamlaka husika juu ya sheria namba 64 na 10 na maboresho ya mwaka 1976.

"Kumekuwa na uvamizi kwenye magofu na malikale na watu hawafuati utaratibu ambapo kumekuwa na mgogoro wa magofu ya Kaole na kuna marekebisho ya sheria namba 10 ya mwaka 1964 na maboresho namba 20 ya mwaka 1979 na kanuni zake kuweka ulazima wa majengo yote yenye zaidi ya miaka 100 yawe chini ya umiliki wa serikali badala ya mtu binafsi,"alisema Kunenge.

Aliongeza kuwa TFS ikusanye mapato ya mali kale kwenye mahoteli au nyumba za kulala wageni na marekebisho ya Gn namba 49 ya mwakab1973 baada ya kumega eneo la hekari 24.7 lililotolewa kwa wananchi.

KITONGOJI CHA KAJANJO KIJIJI CHA SAADANI CHATENGEWA HEKARI 50

Katika hatua nyingine akiwa Kijiji cha Saadani  Kunenge ameagiza leseni ya kampuni ya Sea Salt kupunguza eneo la hekari 50 kati ya 2,000 zinazomilikiwa na kampuni hiyo litagawiwa kwa ajili ya wananchi wa Kitongoji cha Kajanjo.

Alisema eneo hilo la hekari 50 wamepewa wakazi wa kitongoji hicho ambapo kimevunjwa ambapo kuna kaya 17 ambazo zilikuwa hapo na kuongezeka na kufika 120 pia makambi ya muda 72 ambayo wanajihusisha na uvunaji mikoko waondoke kwenye hifadhi ya mikoko.

"Hifadhi ya Saadani SANAPA ilipe kiasi cha shilingi milioni 287 kwa ajili ya mashamba na maendelezo kwa kaya 17 pia kamishna msaidizi wa ardhi abadilishe hati ya eneo la Sea Salt kwa kupunguziwa hekari 50 na mmiliki huyo alinde mipaka yake na watu wasiingie tena kwenye eneo hilo,"alisema Kunenge.

Alimtaka Kamshna Msaidizi wa Ardhi kufuta hati ya mmiliki wa sasa wa East Africa Resort kwa kuwa zipo ndani ya hifadhi na haijaendelezwa na kumtaka Mkurugenzi wa Halmshauri ya Chalinze kufuta kitongoji cha Kajanjo na kuhakisha wananchi wanahamishiwa kwenye hekari hizo 50.

WALIOVAMIA RAZABA WATAKIWA KUONDOKA


KUFUATIA wananchi zaidi ya 5,000 kuvamia eneo la Ranchi ya Zanzibar Bagamoyo (RAZABA) kwenye Kata ya Makurunge Halmashauri ya Bagamoyo serikali imewataka wananchi hao kuondoka na kuikabidhi Wakala wa Usimamizi wa Misitu Tanzania (TFS) kulisimamia eneo hilo.

Hayo yalisemwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge wakati wa ziara yake kwenye maeneo  ya Saadani, (RAZABA) na Mji Mkongwe Bagamoyo na kutoa matamko ya utekelezaji wa maamuzi ya Baraza la Mawaziri kuhusu Migogoro ya matumizi ya Ardhi Mkoani  Pwani.

Kunenge alisema kuwa maamuzi ya kuwaondoa wananchi hao yametokana na serikali baada ys kushughulikia migogoro ya ardhi ambapo Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aliunda timu ya Mawaziri nane wa kisekta iliyoshirikiana na timu ya wataalam  na kufika katika maeneno mbalimbali likiwemo la RAZABA na kutoa mapendekezo ambayo yaliridhiwa na baraza la Mawaziri kwa utekelezaji.

"Shamba hilo lilikuwa ranchi ya Mifugo ambayo ilitolewa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  kwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, eneo hili lilikuwa na ukubwa wa hekari 28,097 ambazo ziligawanywa katika shamba namba 364,365/1 na 365/2 Makurunge,"alisema Kunenge.

Alisema kufuatia maagizo hayo aliwataka wananchi waliovamia eneo hilo la RAZABA kuondoka kwa sababu ni mali ya serikali na kuanzia sasa eneo hilo litakuwa chini ya usimamizi wa Wakala wa Usimamizi wa Misitu Tanzania (TFS).

Tuesday, June 6, 2023

SERIKALI YATATUA MIGOGORO SUGU YA ARDHI MKOANI PWANI

SERIKALI imewaagiza wananchi zaidi ya 5,000 waliyovamia na kuishi  katika Ranchi ya Zanzibar Bagamoyo (RAZABA) kuondoka na kuikabidhi Wakala wa Usimamizi wa Misitu Tanzania (TFS) kulisimamia eneo hilo.

Agizo hilo limetolewa leo Juni 6, 2023 na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge wakati wa Ziara yake  eneo la Saadani na (RAZABA) na Mji Mkongwe Bagamoyo ya kutoa matamko ya Utekelezaji wa Maamuzi ya Baraza la Mawaziri kuhusu Migogoro ya Matumizi ya Ardhi Mkoani  Pwani.

Kunenge amesema maamuzi ya kuwaondoa wananchi hao yametokana na serikali kushughulikia migogoro ya ardhi ambapo Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aliunda timu ya Mawaziri wanane wa kisekta iliyoshirikiana na timu ya wataalam  na kufika katika maeneno mbalimbali likiwemo la RAZABA na kutoa mapendekezo ambayo yaliridhiwa na baraza la Mawaziri kwa utekelezaji.

"Shamba hilo lilikuwa ranchi ya Mifugo ambayo ilitolewa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  kwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, eneo hili lilikuwa na ukubwa wa hekari 28,097 ambazo ziligawanywa katika shamba namba 364,365/1 na 365/2 Makurunge,"amesema Kunenge.

“Naagiza wananchi wa eneo hili la RAZABA kuondoka mara moja kwa sababu ni mali ya serikali na kuanzia sasa lipo chini ya usimamizi wa Wakala wa Usimamizi wa Misitu Tanzania TFS,” amesema Kunenge.

Katika hatua nyingine akiwa Kijiji cha Saadani  Kunenge ameagiza leseni ya kampuni ya Sea Salt kupunguza eneo la hekari 50 kati ya 2,000 zinazomilikiwa na kampuni hiyo  ambalo litagawiwa kwa ajili ya wananchi wa Kitongoji cha Kajanjo.

Amemtaka Kamshna Msaidizi wa Ardhi kufuta hati ya mmiliki wa sasa wa East Africa Resort kwa kuwa zipo ndani ya hifadhi na hakijaendelezwa.

Aidha amemtaka Mkurugenzi wa Halmshauri ya Chalinze kufuta kitongoji cha Kajanjo na kuhakisha Wananchi wanahamishiwa kwenye hekari hizo 50.

Pia amemuagiza Kamishna Msaidizi wa Ardhi, kufuta hati ya upimaji   eneo la Mji Mkongwe, uliofanyika ndani   ya eneo la hifadhi kwa kuwa zilitolewa ndani ya GN namba 1983  na kutatua mgogoro wa ardhi eneo la magofu ya Kaole na Familia ya Omary Sherdel.


Sunday, June 4, 2023

WAFANYABIASHARA HALMASHAURI YA WILAYA YA KIBAHA WATAKIWA KUUNGANA


WAFANYABIASHARA wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani wametakiwa kuungana ili waweze kupata fursa mbalimbali za kiuchumi zilizopo kwenye Wilaya hiyo.

Hayo yalisemwa Mlandizi Wilayani Kibaha na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania (JWT) Mkoa wa Pwani Abdala Ndauka wakati wa mkutano na wafanyabiashara wa Mlandizi.

Ndauka alisema kuwa serikali au wadau wanashindwa kuwafikia wafanyabiashara kutokana na kutokuwa na umoja lakini wakijiunga kwenye umoja ni rahisi kunufaika.

"Serikali haifanyi kazi na mtu mmoja bali inawapa fursa watu kutokana na makundi hivyo ili wafanyabiashara wa Halmashauri hiyo wanufaike na fursa hizo lazima waungane,"alisema Ndauka.

Alisema kuwa Jumuiya ya wafanyabiashara Halmashauri hiyo ilikuwepo lakini ilivunjika hivyo wafanyabiashara walikosa fursa nyingi lakini nia waliyoionesha ya kurudi itawasaidia sana.

"Mnapoungana mnakuwa na sauti moja hivyo ni rahisi kusikilizwa tofauti na mfanyabiashara anapolalamika peke yake pia inasaidia kupata haki zao na kupunguza vitendo vya rushwa na serikali kupata mapato,"alisema Ndauka.

Aidha alisema kuwa na wafanyabiashara hao hawapaswi kuchanganya siasa na biashara kwani inasababisha mgawanyiko baina yao na siasa wawaachie wanasiasa.

Kwa upande wake mratibu wa mkutano huo Majuto Ngozi alisema kuwa wanamshukuru mwenyekiti wa kutoa elimu kwa wafanyabiashara juu ya umuhimu wa kuungana.

Ngozi alisema wataendelea na mchakato ili kuunda Jumuiya yao kwa kutoa elimu kwa wafanyabiashara wengi zaidi ili kuwa na utaratibu mzuri na kufanya uchaguzi wa viongozi ili kupata uongozi imara.

Naye moja ya wafanyabiashara Fihiri Msangi ambaye ni moja ya wanachana wa Jumuiya hiyo  alisema kuwa amepata manufaa makubwa ikiwa ni pamoja na kupata fursa ya kutembelea maeneo mbalimbali ya kibiashara.

Msangi alisema kuwa ameweza kupata pasi ya kusafiria kupitia Jumuiya hivyo kuwa na urahisi wa kwenda nje ya nchi kwa ajili ya kutafuta fursa nje ya nchi.

Katika mkutano huo wafanyabiashara hao walikubaliana kuunda Jumuiya hiyo lakini wapewe elimu juu ya faida za Jumuiya ili wapate uelewa wa pamoja ambapo waliomba wapewe katiba ili waone miongozo ya Jumuiya hiyo.

Friday, June 2, 2023

AHUKUMIWA KUNYONGWA HADI KUFA KWA KUUA WATOTO WAKE WATATU KWA KUWANYWESHA SUMU

MKULIMA na mkazi wa Ditere Wilaya ya Kipolisi Chalinze Mkoani Pwani Salehe Masokola amehukumiwa kunyongwa hadi kufa baada ya kupatikana na hatia ya kuwaua watoto wake watatu kwa kuwanywesha sumu.

Watoto hao watatu waliouwawa kwa kunyweshwa sumu ni Sheila Masokola (8), Nurdin Masokola (6) na Sabrati Masokola miezi (6).

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani (ACP) Muhudhwari Msuya alisema kuwa mshitakiwa huyo alitenda kosa hilo Novemba 26 mwaka 2018 baada ya kutoelewana na mke wake.

Msuya alisema kuwa baada ya kutengana mkewe aliondoka na watoto ambapo aliwafuata watoto wake kwa mama yao na kurudi nao nyumbani kwake ambapo alitekeleza mauaji hayo baada ya mkewe kugoma kurudi nyumbani ili waendelee kuishi.

Alisema kuwa baada ya kutekeleza mauaji hayo alikamatwa na kesi kufunguliwa kwenye kituo cha polisi Chalinze ambapo upelelezi ulifanyika na kupatikana na hatia na kuhukumiwa hadi kufa hukumu na Jaji wa Mahakama Kuu Elizabeth Mkwizu.

Thursday, June 1, 2023

KONGAMANO KUWAKUTANISHA WALIMU WANAWAKE NA UJASURIAMALI

 

WALIMU wanawake 300 kutoka Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani wanatarajia kukutana kwenye Kongamano la ujasiriamali ambalo litafanyika mwezi Agosti mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari Mjini Kibaha Mwenyekiti wa CWT kitengo cha wanawake Rose Nyambweta alisema kuwa wameamua kuandaa kongamano hilo ili walimu hao wajifunze masuala ya ujasiriamali.


Nyambweta alisema kuwa kwenye kongamano hilo kutakuwa na vitu mbalimbali ambavyo walimu hao watafundishwa masomo ya ujasiriamali na masuala ya fedha ikiwa ni pamoja na kujiwekea akiba na ukopaji wa fedha usio na madhara.

"Kongamano hilo litakuwa na wataalamu wa mafunzo hayo ya ujasiriamali ikiwemo wa kutengeneza batiki, sabuni za vipande, vikoi na sabuni za maji ni vitu vya kijasiriamali ili wauze waongeze kipato chao,"alisema Nyambweta.

Kwa upande wake Katibu wa CWT Wilaya ya Kibaha Kitengo cha Wanawake Florence Ambonisye alisema kuwa kutokana na walimu kuwa na mahitaji makubwa wamejikuta wakiingia kwenye mikopo umiza maarufu kama kausha damu na mingineyo lakini ujadiriamali unaweza ukawaondoa kwenye mikopo hiyo inayowaumiza.

Naye Katibu wa CWT Wilaya ya Kibaha John Kigongo ambaye pia ni mjumbe alisema kuwa mara baada ya mafunzo hayo walimu hao wanawake wataunda vikundi vya ujasiriamali ambavyo vitawezeshwa ili vifanye uzalishaji.