Wednesday, December 24, 2014

PWANIYAONGEZA UFAULU DARASA LA SABA

Na John Gagarini, Kibaha
MKOA wa Pwani umeongeza ufaulu kwa wanafunzi waliofanya mtihani wa darasa la saba ambapo jumla wanafunzi 13,242 wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kwenye shule mbalimbali za sekondari.
Akitangaza matokeo hayo mjini Kibaha katibu tawala wa mkoa huo Mgeni Baruani na kusema kuwa wanafunzi wote waliofaulu wamepata nafasi ya kujiunga na shule za sekondari.
Mgeni alisema kuwa Idadi hiyo ni kati ya wanafunzi 23,562 waliofanya mtihani wa darasa la saba mwaka huu, ambapo idadi ya waliofaulu wasichana walikuwa ni 6,851 na wavulana ni 6,391 huku idadi ya wanafunzi wasichana ikionekana kuwa juu.
“Kwa mwaka huu mkoa umeweza kuongeza kiwango cha ufaulu kwa asilimia 56.2 kutoka asilimia 54 ya mwaka 2013 hivyo kushika nafasi ya 13 kitaifa na kuwa moja ya mikoa iliyofanya vizuri,” alisema Mgeni.
Aidha alisema kuwa kupatikana kwa nafasi kwa wanafunzi hao kumetokana na mpango madhubuti uliowekwa na sekretarieti ya mkoa kwa kushirikiana na halmashauri mpango wa kuongeza vyumba vya madarasa katika shule zote za sekondari.
“Shule mpya zimejengwa ambazo zilisaidia kuondoa tatizo la wanafunzi kukosa nafasi katika shule za serikali na tunawaomba wazazi na walezi ambao watoto wao wameichaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza, kutoa ushirikiano kwa kuhakikisha wanawaandikisha watoto hao na kuhudhuria shuleni pasipo visingizio mbalimbali hali inayosababisha kuwakosesha haki yao ya msingi kielimu,” alisema Mgeni.
Kwa upande wake ofisa elimu mkoa wa Pwani Yusuph Kipengele alisema changamoto kubwa inayojitokeza kwa sasa ni baadhi ya wanafunzi wanaosoma shule za binafsi kutokwenda kuripoti katika shule wanazopangiwa.
“Wanafunzi hao wanaosoma shule za binafsi unakuta wanapata nafasi za juu lakini wanaokwenda kuripoti shule za sekondari wanzochaguliwa ni wachache labda wakipangiwa shule za sekondari za  Kibaha zinazomilikiwa na shirika la elimu Kibaha hivyo kuipa shida sana idara yetu”alisema Kipengele.
Kipengele alieleza kuwa wanafunzi hao wasioripoti katika shule za sekondari wanazopangiwa wanawanyima nafasi wanafunzi wengine ambao wangepata fursa ya kwenda kwenye shule hizo.
Mwisho

BEI ZA BIDHAA ZA VYAKULA HAZIJAPANDA X-MASS

Na John Gagarini, Kibaha
HUKU leo ikiwa ni sikukukuu ya kumbukumbu ya kuzaliwa Yesu Kristo X-MASS ikiwa inaadhimishwa duniani kote wakazi wa wilaya ya Kibaha mkoani Pwani wanasherehekea kwa furaha kutokana na bei za bidhaa za vyakula zikiwa hazijapanda kama inavyokuwa miaka ya nyuma.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa bei za bidhaa za vyakula hazijapanda kama miaka ya nyuma kwani nyingi ziko vilevile hali amabyo imefurahiwa na wananchi wengi.
Akizungumza na gazeti hili mjini Kibaha mkazi wa Maili Moja Kibena Mtoro alisema kuwa wanasherehekea sikukuu hii huku bei za bidhaa za vyakula zikiwa ni za kawaida.
“Miaka ya nyuma beiza bidhaa za vyakula zilikuwa zinapanda mara dufu lakini mwaka huu tunamshukuru Mungu kwani bei ni zilezile,” alisema Mtoro.
Mtoro alisema kipindi cha nyuma baadhi ya watu wenye kipato cha chini walikuwa hawaifurahii sikukuu kutokana na bei kuwa juu.
“Kutokana na hali ya kiuchumi kuwa mabaya na bei kuwa za kawaida ni dhahiri tunasherehekea sikuku hii kwa furaha kwani kila mtu anamudu kununua chakula,” alisema Mtoro.
Kwa upande wake katibu wa soko kuu la wilaya ya Kibaha Maili Moja, Muhsin Abdu alisema kuwa kwa mwaka huu bei hazijapanda kabisa.
Abdu alisema kuwa bei ya ndizi pekee ndiyo iliyopanda ambapo mkungu umepanda bei kutoka shilingi 20, 000 hadi 35,000 kwa mkungu pamoja na tanagawizi toka shilingi 3,000 kwa kilo hadi 4,500.
“Bei haijapanda kwa sababu mojawapo ni wakulima wengi kuleta bidhaa toka mashambani na kuja kuziuza mjini tofauti na kipindi cha nyuma ambapo wafanyabiashara walikuwa wakileta bidhaa na kuuza kwa bei kubwa,” alisema Muhsin.
Alisema kuwa wafanyabiashara ndiyo walikuwa wakipandisha bei kwa kuficha bidhaa ili wauze kwa bei kubwa wakitoa visingizio mbalimbali.
“Kipindi kile bei zilikuwa juu na zinakuwa adimu lakini safari hii vyakula vingi na bado vinakuja kwa wingi hata sisi tunafurahia hali kwani bei zikiwa juu hata uuzaji unakuwa mgumu,” alisema Abdu.
Mwisho.

BIDHAA ZA VYAKULA HAZIJAPANDA X-MASS 2014

POLISI KUWEKA ULINZI MKALI SIKUKUU ZA X-MASS NA MWAKA MPAYA

Na John Gagarini, Kibaha
JESHI la Polisi mkoani Pwani limewataka wananchi kutumia vikundi vya ulinzi shirikishi ili kukabiliana na uhalifu katika kipindi hichi cha sikukuu za X-Mass na mwaka mpya.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mjini Kibaha, kamanda wa Polisi mkoani hapa Ulrich Matei alisema kuwa wamejipanga vyema kudhibiti vitendo viovu kwa kushirikiana na wananchi.
Matei alisema kuwa katika kukabiliana na matukio ya uhalifu kipindi cha sikukuu kwa kutumia ulinzi shirikishi, ulinzi jirani na mgambo.
“Tutashirikiana na wananchi katika ulinzi ili washerehekee kwa amani na utulivu na tutakaowabaini wanaofanya matukio ya uhalifu,” alisema Matei.
Alisema kuwa katika ulinzi jirani wananchi wanatakiwa kuacha tabia ya kuondoka nyumbani bila ya kuacha mtu au hata kama wanatoka wawajulishe majirani zao.
“Baadhi ya vitendo viovu vinavyofanyika ni pamoja na uchomaji matairi ni kinyume cha sheria na hairuhusiwi kufanya hivyo,” alisema Matei.
Aidha alisema kuwa wazazi wanapaswa kutowaacha watoto wao kwenda kwenye maeneo ya starehe peke yao kwani ni hatari.
Aliwataka madereva kuhakikisha wanaendesha magari wakiwa hawajalewa ili kuepukana na ajali pia watawapima ulevi madereva hao kwani vifaa vya kupimia sasa wanavyo vya kutosha.
Mwisho.

Tuesday, December 23, 2014

AMWUA MWANAE KWA KUMNYONGA ADAKWA NA HEROIN

Na John Gagarini, Kibaha
ESTER Endrew (23) mkulima mkazi wa Tabata Jijini Dar es Salaam anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Pwani kwa tuhuma za kumwua mwanae Marko Elibariki (2) kwa kumnyonga kwa kutumia mikono.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mjini Kibaha, kamanda wa polisi mkoani hapa Ulrich Matei alisema kuwa tukio hilo linahusishwa na wivu wa kimapenzi.
Kamanda Matei alisema kuwa tukio hilo lilitokea saa 2 asubuhi eneo la Wipas mtaa wa mkoani B kata ya Tumbi wilayani Kibaha.
“Mtuhumiwa baada ya kutekeleza tukio hilo naye alijichoma tumboni kwa kisu hali iliyosababisha apate majeraha,” alisema Kamanda Matei.
Alisema kuwa mtuhumiwa huyo baada ya tukio baadhi ya majirani waligundua kutokana na kulalamika huku damu zikimtoka.
“Alijijeruhi tumboni kwa kisu akitaka kujiua lakini hata hivyo licha ya kujichoma hakufa na kuanza kupiga kelele ndipo majirani walipotoa taarifa polisi na mtuhumiwa kuja kuchukuliwa ambapo ilibainika kuwa alikuwa akimlaumu mumewe kuwa na mke mwingine,” alisema Kamanda Matei.
Aidha alisema mtuhumiwa amelazwa kwenye hospitali ya Rufaa ya mkoa ya Tumbi kwa matibabu huku akiwa chini ya ulinzi.
Mwisho.
Na John Gagarini, Kibaha
SHAMBA Malela (20) mkazi wa Nianjema wilayani Bagamoyo mkoani Pwani anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kupatikana na kete 136 za dawa aina ya Heroin.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoani Pwani Ulrich Matei alisema kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa na polisi waliokuwa doria.
Kamanda Matei alisema kuwa tukio hilo lilitokea Desemba 22 mwaka huu majira ya saa 7:45 mchana huko Nianjema kata ya Magomeni wilaya ya Bagamoyo.
“Mtuhumiwa baada ya kutiliwa mashaka alikwenda kupekuliwa nyumbani kwake na kukutwa na dawa hizo ambazo zinadhaniwa kuwa ni za Heroin ambapo hata hivyo thamanai yake haikuweza kufahamika mara moja.
Alisema kuwa jeshi hilo linafanya doria kwenye maeneo mbalimbali ya wilaya za mkoa huo ili kukabiliana na matukio mbalimbali ya uhalifu.
Mwisho.

Sunday, December 21, 2014

Saturday, December 20, 2014

RIDHIWANI AKARIBISHWA KIJIJINI MSOGA KWA SHEREHE ZA JADI

Na John Gagarini, Chalinze

MBUNGE wa Jimbo la Chalinze Wilayani Bagamoyo mkoani Pwani  Ridhiwani Kikwete juzi alifanyiwa sherehe za jadi za kabila la Kikwere kama kiongozi baada ya kuchaguliwa kuwa mbunge.

Sherehe hizo za jadi ambazo zilifanyika kijijini kwao Msoga ziliambatana na kukabidhiwa vitu mbalimbali vya kijadi kwa ajili ya matumizi ya nyumbani.

Baadhi ya vitu alivyoakabidhiwa na mzee wa kabila hilo Zaidi Rufunga ni pamoja na fimbo kama kiongozi, kitanda cha kamba, msuli, kigoda na kinu pamoja na vitu mbalimbali.

Sherehe hizo za kijadi ziliamabatana na ngoma ya Kikwere na ulaji wa chakula kiitwacho Bambiko ambacho hutumiwa na kabila hilo. 

 Mzee Zaidi Rufunga kulia akimkabidhi vyungu mbunge wa Jimbo la Chalinze wilayani Bagamoyo mkoani Pwani Ridhiwani Kikwete wakati wa sherehe za jadi za kumkaribisha nyumbani zilizofanyika juzi kijiji cha Msoga. 

 Mbunge wa Jimbo la Chalinze wilayani Bagamoyo mkoani Pwani  akielekezwa jambo na mzee Zaidi Rufunga  kabla ya kula chakula cha jadi cha kabila la Wakwere kiitwacho Bambiko baada ya kukaribishwa nyumbani na kufanyiwa sherehe za jadi za kikabila zilizofanyika kwenye Kijiji cha Msoga.

Baadhi ya akina mama wakila chakula mcha jadi cha kabila la Kikwere kiitwacho Bambiko mara baada ya kumkaribisha nyumbani Mbunge wa Jimbo la Chalinze wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani

 Baadhi ya akina mama wakila chakula mcha jadi cha kabila la Kikwere kiitwacho Bambiko mara baada ya kumkaribisha nyumbani Mbunge wa Jimbo la Chalinze wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani

Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete kushoto na katikati diwani wa kata ya Msoga Mohamed Mzimba na baadhi ya wageni wakila chakula cha jadi kiitwacho Bambiko mara baada ya sherehe za jadi za kumkaribisha nyumbani kwenye Kijiji cha Msoga .