Monday, February 11, 2013

NYUMBA YA MKT YATEKETEA WATOTO WANUSURIA

Na John Gagarini, Kibaha
NYUMBA ya mwenyekiti wa mtaa waPicha ya Ndege wilayani Kibaha mkoani Pwani imeungua moto ambapo watoto wawili wadogo waliokuwa wamelala wamenusurika kufa baada ya kuamka muda mchache kabla ya tukio la moto.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mwenyekiti huyo Bw Godfrey Mwaipopo alisema kuwa moto huo ulitokea majira ya saa 9 alasiri ambapo kulikuwa hakuna mtu na nyumba ikiwa imefungwa kabla ya majirani kujitokeza na kuzima moto huo.
Bw Mwaipopo alisema kuwa watoto hao Ibrahim Hausi (2) mjukuu wake na Olebu Lugano mwaka mmoja na nusu ambaye ni mtoto wa shemeji yake walikuwa wamelala kama kawaida kwani mara baada ya kula ni kawaida kutakiwa kulala walilala ambapo kwa bahati nzuri waliamka na kwenda kucheza.
“Tunamshukuru Mungu kwani wakati moto huo unatokea watoto wale walisha amka na kwenda kucheza kwani kulikuwa hakuna mtu mzima mimi nilikuwa kwenye kikao Halmashauri ya Mji na mke wangu alikwenda kwenye masuala ya mikopo lakini ghafla nilipigiwa simu na jirani na kuambiwa kuwa nyumba yangu inawaka moto,” alisema Bw Mwaipopo.
Alisema alipofika alikuta majirani wakiwa wamejaa na kufanya jitihada baada ya kuvunja milango na kuanza kuzima moto huo ambao ulianzia kwenye swichi ya umeme, na kuzima moto huo ambao ulianza kusambaa kwa kasi.
“Kwa kweli hakuna mtu aliyejeruhiwa na moto huo licha ya vitu kadhaa kuungua ikiwemo vyeti, nguo makochi na kitanda na cha kushangaza ni kwamba eneo hili lina tatizo la maji lakini maji yalipatikana kwani kila mtu alichukua akiba na kuja kuuzima moto pia walitumia mchanga,” alisema Bw Mwaipopo.  
Aidha alisema kuwa gari la zima moto lilifika lakini walikuta moto umeshazimwa na lilichelewa kutokana na miundombinu kutoruhusu kupita hivyo walitumia muda mwingi kutafuta njia ya kupita.
Aliwashukuru sana wananchi wa mtaa huo kwa kujitokeza kwa wingi kwa kutoa msaada wa kuzima moto huo vinginevyo nyumba hiyo ingeteketea yote na kusingeweza kuokolewa kitu.
Mwisho.
Na John Gagarini, Kibaha
ASKARI wa usalama barabarani mkoani Pwani wametakiwa kuongeza juhudi katika kuzuia ajali za magari barabarani ambapo kwa mwaka jana mkoa huo uliongoza kwa kupunguza ajali hapa nchini.
Hayo yalisemwa mwishoni mwa wiki mjini Kibaha na aliyewahi kuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani Ernest Mangu wakati wa sherehe ya kumwaga ambapo amehamishiwa mkoa wa Mwanza na kumkaribisha kamanda mpya Ulrich Matei.
Kamanda Mangu alisema kuwa kwa kipindi cha mwaka mmoja na miezi mitano aliyokaa kwenye mkoa huo kwa kushirikiana na askari wengine walifanikiwa kupunguza ajali ambapo mkoa uliongoza na kuwa wakwanza.
“Mkoa wa Pwani ulikuwa ni moja ya mikoa iliyokuwa ikiongoza kwa kuwa na ajali nyingi za magari hasa ikizingatiwa kuwa mkoa huo ndiyo lango kuu la kuingilia Jiji la Dar es Salaam kutoka mikoani na nje ya nchi,” alisema Kamanda Mangu.
Alisema kuwa kikubwa kilichosababisha mkoa kufanikiwa kupunguza ajali za magari ni kutokana na ushirikiano baina ya askari wa usalama barabarani na wadau wengine ikiwemo kamati ya usalama barabarani ya mkoa.
“Nawaomba mumpe ushirikiano kamanda mpya ili muendeleze rekodi ambayo mliiweka mwaka jana kwa kufanya kazi nzuri ya kuzuia ajali barabarani ambazo zimekatisha maisha ya watu na wengine kuwa na ulemavu,” alisema Kamanda Mangu.
Kwa upande wake kamanda Matei alisema kuwa kwa kushirikiana na wenzake watafuata nyayo za mwenzake ili kuhakikisha mkoa unakuwa mbele kupambana na ajali.
“Mbali ya kuongoza kwa kupunguza ajali pia mkoa ulifanikiwa kuongoza kwa kukusanya fedha kutokana na makosa mbalimbali ya barabarani na kuushinda hata mkoa kama Mwanza amabo ni Jiji,” alisema Kamanda Matei.
Kamanda Matei alisema kuwa anaomba ushirikiano toka kwa wananchi wa mkoa huo ili waweze kukabiliana na maovu mbalimbali kwenye mkoa huo, sherehe hiyo ilihudhuriwa na viongozi waandamizi wa jeshi hilo.
Mwisho.

Sunday, February 10, 2013

MIPAKA YALETA KIZAAZAA

Na Mwandishi Wetu, Kibaha
SAKATA la kugombea mipaka kwa wakazi wawili wa Mtaa wa Visiga Kati wilayani Kibaha mkoani Pwani limechukua sura mpya baada ya mlalamikiwa kuwasweka walalamikaji rumande licha ya licha ya baraza la ardhi la mtaa huo kutoa maamuzi.
Maamuzi ya baraza hilo yalitoa maamuzi kuwa mlalamikiwa Bw Salum Mnjovu asogeze mpaka huo ambao ulileta mzozo baina yake na jirani yake Bw Henrik Simbanyamba.
Hata  hivyo baada ya maamuzi hayo Bw Simbanyamba alilalamika kuwa yeye na Bw Ally Mnola na Bi Ashura Mohamed walikamatwa na polisi baada ya Bw Mnjovu kwenda polisi kulalamika kuwa wameharibu mali zake.
Alisema kuwa anashangaa kukamatwa kwani shauri lilisha amuliwa na baraza na hata kama ana malalamiko ilipaswa aende mahakama ya juu kwenda kutoa mamalamiko yake.
Alisema walikamatwa na askari wa kituo cha polisi Visiga na kushikiliwa kwa muda kabla ya kuachiwa nakuwa nje kwa dhamana hadi Jumanne ambapo suala hilo litaendelea.
“Tunachotaka sheria zifuatwe kwani sisi majirani zake tuna kosa gani hadi tunakamatwa kwani kama ni maamuzi yalitolewa na baraza likaweka mipaka halali,” alisema Bw Simbanyamba.
Bw Mnjovu alitakiwa arekebishe mpaka lakini alipingana na maamuzi hayo kwa kusema kuwa yeye alipouziwa na Bw Seko Mbaruku alionyeshwa tofauti na anashangaa kwanini asogeze mpaka ambapo alilalamika kuwa ameweka kisima cha chini hivyo itabidi kibomolewe.
“Mimi sikubaliani na maamuzi yaliyotolewa kwani wakati nanunua eneo hili kwa thamani ya shilingi milioni 5 toka kwa Bw Mbaruku nilionyeshwa mipaka mbele ya uongozi wa mtaa akiwemo mwenyekiti Bw Hemed Mpaki na ofisa Mtendaji wa mtaa Bw Benedict Maganga nashangaa leo kuambiwa kuwa mpaka umekosewa,” alisema Bw Mnjovu.
Alisema kuwa anashangaa kuona maamuzi yanatolewa huku viongozi wa mtaa hawapo ambao ndiyo walikuwepo wakati wa mauziano na mipaka ilipokuwa inaonyeshwa walikuwepo.
“Sijaridhika na maamuzi nitakwenda mbele ili niweze kupata haki yangu kwani naona haki haijatendeka kwa upande wangu niko hapa miaka miwili iliyopita hakukuwa na maneno, pia mawe niliyoweka niliweka kwenye mpaka wangu na sikuingia kwenye eneo la mtu,” alisema Bw Mnjovu.
Naye mlalamikaji Bw Simbanyamba alisema kuwa alishangaa kuona jirani yake akingoa michungwa ambayo ndiyo iliyokuwa mipaka kasha kuweka mawe ndani ya eneo lake jambo ambalo lilimfanya aende kwenye baraza kutafuta haki yake.
“Miezi miwili iliyopita tuliona anaweka mawe na tulivyojaribu kumwambia kuwa mipaka hiyo ni ya asili hivyo asiitoe lakini alingoa michungwa na mnazi kisha kusogeza mpaka,” alisema Bw Simbanyamba.
Kaimu mwenyekiti wa baraza hilo Bi Mwanahawa Husein alisema kuwa baraza hilo limefuata sheria na halijamuonea mtu kwani lenyewe linatenda haki na kama mlalamikiwa anaona kaonewa anaruhusiwa kukata rufaa ndani ya siku 45.
Kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa huo Bw Hemed Mpaki alisema kuwa mipaka ilikuwa ni michungwa ambapo wakati wa mauziano mlalamikaji Bw Simbanyamba hakuwepo.
“Muuzaji Bw Mbaruku alimwelekeza vibaya mipaka na suala la kupanda mawe ilibidi majirani wote wawepo ili kuondoa migogoro jambo ambalo majirani hawakushierikishwa,” alisema Bw Mpaki.
 Mwisho.
 
Friday, February 8, 2013

SAKATA KUGOMBEA MPAKA LACHUKUA SURA MPYA

WANAOCHUKUA SHERIA MKONONI WAONYWA

Na  John Gagarini, Kibaha
SERIKALI imewaonya wananchi wanaojichukulia sheria mkononi kwa kuwaua watuhumiwa badala yake wawapeleke kwenye vyombo husika ili wachukuliwe hatua za kisheria.
Hayo yalisemwa na kamanda wa polisi mkoani Pwani Ulrich Matei ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya siku ya sheria (Law Day) na kusema kuwa watu wengi wamepoteza maisha katika mkoa huo kutokana na watu kujichukulia sheria mkononi.
Kamanda Matei alisema kuwa vyombo vya kutoa haki vipo hivyo wananchi wa mkoa huo hawapaswi kuwaua watuhumiwa kwani wengine wanakuwa hawana hatia.
“Watu wengi wameuawa na watu wanaoojiita kuwa wana hasira kali na kuwafanyia vitendo vya kinyama watuhumiwa wa wizi wa pikipiki, kuku na vitu vidogovidogo,serikali haitakuwa tayari kuona vitendo hivyo vinaendelea,” alisema Kamanda Matei.
Alisema kuwa watu hao wanaojiita wenye hasira kali mbali ya kuua watuhumiwa wameharibu miundombinu mbalimbali ya watu na serikali jambo ambalo ni kinyume cha sheria.
“Tabia hii kwa sasa imeshamiri na kushika mizizi kwa sasa kwenye mkoa wa Pwani jambo hili ni kinyume cha sheria na haki za binaadamu kwani hata katiba inalinda haki ya mtu kuishi,” alisema Kamanda Matei.
Aidha alivitaka vyombo vya kutoa haki kutochelewesha kutoa maamuzi ili kuondoa dhana kuwa haki haitendeki na kufikia watu kujichukulia sheria mkononi.
Mwisho.

Wednesday, February 6, 2013

WATAKA MAJAJI WAFANYIWE USAILI

Na John Gagarini, Kibaha
SEIKALI imeshauriwa kubadili mfumo wa upatikanaji wa majaji kwa kufanyiwa usaili badala ya kuteuliwa ili kuleta utawala bora wa kisheria.
Hayo yalisemwa jana mjini Kibaha na mwakilishi wa mawakili mkoani Pwani, Saiwelo Kumwenda, wakati wa maadhimisho ya siku ya sheria nchini kwenye mkoa huo zilizofanyika kwenye viwanja vya mahakama.
Alisema kuwa ili kuimarisha utawala wa sheria ni vema waajiriwe kwa kwa kufanyiwa usaili rasmi na chombo kisicho na mfungamano wa kiutawala na serikali.
“Ni vema majaji wakaomba kazi na kufanyiwa usaili na wale watakaofuzu vigezo vinavyotakiwa ndiyo watakaopata nafasi hiyo tofauti na sasa ambapo huteuliwa na Raisi,” alisema Bw Kumwenda.
Alisema kuwa mfumo wa kuteua si mzuri katika mfumo wa kutaka kuimarisha utawala wa sheria ili kuepuka malalamiko na manunguniko.
Aidha alitaka viongozi wan chi kusaidia kulinda uhuru wa mahakama ili nchi iendelee kufuata utawala wa sheria na mfumo mzima wa demokrasia.
Pia kuchukua hatua ya kinidhamu kwa watumishi wale ambao wanaonekana au watathibitika kuwa kazi zao za kutafsiri sheria, kusikiliza mashauri na kuyatolea maamuzi hawaijui vizuri wala hawazielewi.
Kwa upande wake hakimu mkazi mfawidhi wilaya ya Kibaha mkoani Pwani Bi Bahati Ndesarua alisema kuwa utawala wa sheria una umuhimu kwa kugawa madaraka kwa kuzingatia taratibu.
Bi Ndesarua alisema kuwa utawala wa sheria unasaidia kukua kwa uchumi na watu kupata haki zao bila ya kumwonea mtu kutokana na uwezo wake.
Aliwataka wananchi kushiriki katiba zoezi la uboreshaji wa katiba mpya ili kutoa mchango wao wa mawazo na kuifanya iweze kuwa na manufaa kwa kila mtu.
Naye mgeni rasmi kamanda wa polisi mkoani Pwani Bw Ulrich Matei alisema kuwa wananchi waachane na tabia ya kuvunja sheria kwa kuwapiga na kuwaua watuhumiwa.
Bw Matei alsiema kuwa ni vema wananchi hao wakawapeleka kwenye vyombo vya sheria ili haki iweze kutendeka na si kutumia mabavu kwa kuwaua.
Mwisho.

Friday, February 1, 2013

MWANAFUNZI ATOWEKA NYUMBANI BAADA YA KUFELI KIDATO CHA PILI

Na John Gagarini, Kibaha
MWANAFUNZI ambaye ni miongoni mwa wanafunzi waliofeli kidato cha pili mwaka jana kwenye shule ya sekondari ya Tumbi wilayani Kibaha mkoani Pwani Shaban Kihemele (16) ametoroka nyumbani kwa madai kuwa wanafunzi wenzake kumzomea kuwa amerudia darasa.
Akizungumza na waandishi wa habari hizi mjini Kibaha mzazi wa mtoto huyo Bw Shaban Kihemele alisema kuwa mwanae huyo huyo alitoroka Januari 24 mwaka huu na hadi leo hajaonekana licha ya jitihada za kumtafuta kushindwa kufua dafu.
Bw Kihemele alisema kuwa mwanae aliondoka nyumbani majira ya saa 4 asubuhi huku akiwa amevalia kaptura nyeusi ya Jeans iliyokatwa tisheti ya rangi ya zambarau yenye ufito mweupe kifuani na ndala nyekundu.
“Chanzo cha yeye kutoroka siku ya Januari 23 alimwambia mama yake kuwa kutokana na kufeli mtihani wa kidato cha pili ni vema wamwamishe shule kuliko kuendelea kusoma hapo kwani wanafunzi wanaomfahamu wanamzomea lakini mama yake alimwambia asubiri mimi nirudi kwani sikuwepo nilikuwa Bagamoyo kikazi,” alisema bw Kihemele.
Alisema mama yake alimjibu kuwa asubiri hadi nirudi lakini kesho yake alirudi kutoka shuleni na kubadilisha nguo huku majirani wakimwuliza kuwa ni kwanini amewahi kurudi na anakwenda wapi akawaambia yuko hapa hapa pia baba yake hajalipa ada hivyo amerudishwa.
“Alichukua fedha kiasi cha shilingi 20,000 kati ya shilingi 50,000 zilizokuwepo kasha akachukua na shuka kisha kuondoka kusikojulikana na inawezekana aliotoroka kutokana na kuona kuwa ni fedheha kurudia darasa na madai kuwa wenzake wanamzomea jambo ambalo linatushangaza,” alisema Bw Kihemele.
Aidha alisema siku ya kwanza walimsubiri hakutokea na ilipofika usiku walikwenda kutoa taarifa kituo cha polisi cha Maili Moja KMM/RB/108/2013 juu ya kutoonekana mtoto wao, walikwenda nyumbani kwao Bagamoyo lakini hawajaweza kufanikiwa kumwona pia waliwasiliana na ndugu zao wote lakini imeshindikana.
Mwisho.