SHULE ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere imeingia makubaliano ya ushirikiano na Chuo Kikuu cha Renmin katika nyanja mbalimbali zikiwemo za mafunzo utafiti na kubadilishana wataalamu.
Wakisaini makubaliano hayo kati ya Mkuu wa Shule ya Mwalimu Nyerere Profesa Marcellina Chijoriga na kiongozi mkuu wa Chama Tawala Cha China Cha (CPC) kwenye Renmin Zhang Donggang katika Shule hiyo iliyopo Kibaha Mkoani Pwani walifurahishwa na ushirikiano huo.
Chijoriga alisema kuwa makubaliano hayo yatakuwa ni kwa ajili ya kubadilishana wataalamu ambapo wao watakuja huku na wa Tanzania watakwenda kwao ikiwa ni sehemu ya kubadilishana uzoefu.
“Chuo hicho ni kikubwa sana na cha muda mrefu na kiko vizuri kwenye masuala ya utafiti wa uandishi wa vitabu na katika masuala ya uandishi wa vitabu ambapo ushirikiano huo utakuwa na manufaa makubwa sana kwa pande zote mbili,”alisema Chijoriga.
Alisema kuwa chuo hicho cha Renmin kinauwezo mkubwa wa kuwajengea uwezo viongozi wa chama na serikali kwani kiko vizuri sana katika ufundishaji masuala hayo na watatumia uzoefu ili kujifunza kupitia kwao kwani kimeanza muda mrefu.
“Faida hiyo ni kwa vyama sita vya ukombozi Kusini mwa Afrika ambapo China ni msaidizi mzuri kwani wamesaidia ujenzi wa shule hiyo ambavyo ni CCM, FRELIMO, SWAPO, ANC na ZANU-PF ambapo CPC .
Aidha alisema kuwa chuo hicho kilichopo Beijeng China kilianza ushirikiano mwaka jana ambapo uongozi wa Shule walikwenda na katibu mkuu wa CCM wakati ule Chongolo na sasa imeanza safari mpya na kina uzoefu mkubwa nani cha zamani sana.
“Tunashukuru sana kwani wametuonyesha ushirikiano mkubwa na makubaliano ya kutengeneza ushirikiano huu ni sasa safari mpya imeanz na leo waametupa vitabu tunawashukuru kwani maktaba yetu sasa itakuwa na vitabu vingi na wasomaji wataweza kujifunza masuala mbalimbali ya nchi ya China,”alisema Chijoriga.
Naye alisema Dk Evaristo Haule Naibu Mkuu wa Chuo Mipango Fedha na Utawala Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere alisema kuwa China imefanikiwa na tumeona namna gani kutumia njia ili kuona wao wamefanyaje na kufikia hatua kubwa kiasi hicho kwenye maendeleo na CPC inavyotoa dira kuongoza nchi yao wanataka twende pamoja katika miradi yao mikubwa ya kidunia.
Haule alisema kuwa ili kwenda pamoja hivi karibuni Rais Dk Samia Suluhu Hassan alienda China kwenye mkutano wa ushirikiano kati ya China na nchi za Afrika wao wana dira na kufanya kazi kwa bidii na kuwa na nidhamu ya kazi na watu wawe na uzalendo wa nchi watu wanaangalia changamoto badala ya kuangalia fursa zilizopo.
Naye Dk Theresia Dominick kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam alisema kuwa Watanzania wanatakiwa kujifunza kwa kuwa nadhifu na wanaangalia masuala ya ulaji na wawe watu wa kujishusha na kuachana na matumizi yasiyo ya lazima na wasiwe na tamaa.
Dominick alisema kuwa badhi ya wafanyabiashara Watanzania wamekuwa wakienda China hivyo wanapaswa kujifunza tabia za Wachina za kufanya kazi kwa bidii na kuwa na nidhamu ya jambo wanalolifanya ni mfano wa kuigwa.
Naye kiongozi huyo Zhang Donggang alisema kuwa ushirikiano uliopo baina ya China na Tanzania nan chi nyingine ni katika masuala mbalimbali ya kimaendeleo ambapo wao wanaangalia sana maslahi ya wananchi.
Donggang alisema kuwa nchi za Afrika na China zinapaswa kushikana mkono katika kuhakikisha zinapiga hatua katika masuala ya kimaendeleoili kudumisha umoja uliopo kwani umoja uliopo umeleta mafanikio makubwa.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment