Pongezi hizo zilitolewa na Katibu wa Taasisi ya Kumbukumbu ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Mkoa wa Pwani ndugu Omary Punzi wakati wa mafunzo ya Ijue Kesho yako kwa wanawake wa mkoa wa Pwani yaliyofanyika Mlandizi Wilayani Kibaha.
Punzi alipata nafasi ya kuwashukuru na kuwaambia wanawake kuwa Mwalimu Nyerere alijenga misingi ya Uzalendo, kujituma na kujitoa kwa hali na mali katika nchi na misingi ambapo misingi hiyo ilitokana na nguvu ya Mwanamke katika kuleta maendeleo.
Alisema Mwalimu Nyerere katika Uongozi wake alijitahidi sana kuwainua wanawake mfano mzuri ni Bibi TITI MOHAMMED ambaye alikuwa karibu sana na Mwalimu katika kupigania Uhuru wa Taifa na hakuna Taifa lolote linaloendelea ikiwa Mwanamke atawekwa nyuma.
"Ushauri wangu serikali inatakiwa kuwekeza nguvu kubwa ya kuhakikisha mwanamke anapatiwa mahitaji yote ya msingi endelevu ya kumwezesha katika kumuinua kiuchumi,"alisema Punzi.
Kwa upande wake mgeni rasmi Mkali Kanusu mwenyekiti wa CCM Kibaha Vijijini ambaye alimwakilisha Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM NEC Hamoud Jumaa, aliwapongeza waandaji na wawezeshaji kwa mada zilizokuwa zinatolewa ni nzuri na mahiri kwa wakati tulionao kwa Serikali ya Mheshimiwa Daktari Samia Suluhu Hassani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kanusu alishauri matukio kama hayo yafanyike mara mbili kwsa mwaka kwani itasaidia kuwakumbusha watu maadili ya Watanzania na kama chama wamelipokea na kuhakikisha wanaunga mkono juhudi za maendeleo kwa wanawake wa Kibaha na Tanzania kwa ujumla.
Naye Mwakilishi wa Taasisi ya IJUE KESHO YAKO Ndugu Martha Kyoka alisema lengo kuu la Taasisi hiyo ni kuhakikisha wanamjengea uwezo mwanamke kujitambua na kutekeleza malengo katika maisha na jamii kwa ujumla ambapo takribani wanawake 100 walipatiwa mafunzo hayo.
Masomo waliyofundishwa ni pamoja na Afya ya Akili, malezi ya mume na mtoto nyumbani, nafasi ya kujitambua, Uwekezaji, Maono na Mikopo na Ujasiriamali.
No comments:
Post a Comment