Sunday, November 1, 2015
johngagariniblog: RIDHIWANI KIKWETE AWASHUKURU WANACHALINZE KUMCHAGU...
johngagariniblog: RIDHIWANI KIKWETE AWASHUKURU WANACHALINZE KUMCHAGU...: Na John Gagarini, Chalinze MBUNGE Mteule wa Jimbo la Chalinze wilayani Bagamoyo mkoani Pwani Ridhiwani Kikwete amesema kuwa hana chuki kw...
Friday, October 30, 2015
RIDHIWANI KIKWETE AWASHUKURU WANACHALINZE KUMCHAGUA TENA
Na John Gagarini, Chalinze
MBUNGE Mteule wa Jimbo la Chalinze wilayani Bagamoyo mkoani Pwani Ridhiwani Kikwete amesema kuwa hana chuki kwa wale ambao hawakumpigia kura kwenye uchaguzi uliofanyika Oktoba 25 mwaka huu kwani hizo ni changamoto za uchaguzi.
Aliyasema hayo jana kwenye uwanja wa Miembe Saba Chalinze wilayani Bagamoyo wakati wa mkutano wa hadhara wa kuwashukuru Wanachalinze kwa kumchagua kuwa mbunge kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika Jumapili.
Ridhiwani alisema kuwa licha ya baadhi ya maeneo kutompigia kura za kumchagua kuwa mbunge lakini atawatumikia wananchi wote bila ya kujali kama walimpigia kura au la kwani kila mtu ana haki ya kumpigia kura mgombea yoyote anayempenda.
“Nawashukuru wananchi wote walionipigia kura na hata wale ambao hawakunipigia kura kwani hiyo ndiyo demokrasia nitahakikisha nawahudumia wananchi wote bila ya kuwabagua nitahakikisha napeleka maendeleo kwa watu wote wa jimbo hili,” alisema Ridhiwani.
Alisema kuwa kutopigiwa kura kwa wingi siyo sababu ya kuwagawa wananchi kwani hizo ni changamoto za uchaguzi ambao unakuwa na mambo yake ambapo baadhi ya maeneo walipiga kura kwa kuzingatia ukabila.
“Sitakuwa na chuki wala hasira kwa wale ambao hawakunipigia kura nitashirikiana nao katika suala la maendeleo ili kuhakikisha jimbo letu linakuw ana maendendeleo na wananchi wanaboresha maisha yao ili yasonge mbele,” alisema Ridhiwani.
Aidha alisema kuwa atahakikisha Mji wa Chalinze ambao umekuwa Halmashauri ya Mji Mdogo unajengwa kwa kuwekewa huduma muhimu ili wananchi waweze kuboresha biahara zao hasa ikizingatiwa kuwa mji huo ni wa kibiashara.
“Moja ya mambo nitakayo yafanya ni kufanya Chalinze kuwa makao makuu ya Halmashauri hiyo na baadaye kuwa wilaya kwani mchakato unaendelea na tunaamini baada ya muda tutapewa wilaya hivyo tutaweza kujitegemea na kujiimarisha kiuchumi,” alisema Ridhiwani.
Alibainisha kuwa wananchi wasiwe na wasi wasi kwani kukichagua Chama Cha Mapanduzi CCM ni kuchagua maendeleo hivyo wasubiri kuona jinsi serikali mpya itakavyofanya kazi kwani kwao ni kazi tu.
Kwa upande wake mwenyekiti wa CCM Chalinze Nasa Karama alisema kuwa mbunge huyo ameonyesha uwezo mkubwa kwani kwa kipindi alichochaguliwa cha mwaka mmoja na miezi mitatu ameweza kufanya mambo makubwa ambapo alitumia ziadi ya shilingi bilioni moja na zaidi kwa ajali ya miradi ya maendeleo.
Mwisho.
Ridhiwani Kikwete |
Sunday, October 25, 2015
RAIS DK JAKAYA KIKWETE ASHIRIKI ZOEZI LA KUPIGA KURA MSOGA
Rais Dk Jakaya Kikwete akihojiwa na waandishi wa habara mara baada ya kupiga kura kwenye kituo cha Kijiji cha Msoga |
Rais Dk Jakaya Kikwete kushoto akisubiri kupewa karatasi kwa ajili ya kwenda kupiga kura |
Rais Dk Jakaya Kikwete akiwa amepanga foleni kabla ya kwenda kupiga kura hata hivyo alisimama kwa muda mfupi kabla ya kutimiza zoezi hilo |
Rais Dk Jakaya Kikwete akisalimiana na mkuu wa mkoa wa Pwani Evaristi Ndikilo alipowasili kwenye kituo cha kupigia kura kwenye Kijiji cha Msoga |
Baadhi ya akinamama wakiwa wanasubiri kupiga kura kwenye kituo cha Kijiji cha Msoga |
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kupitia CCM Ridhiwani Kikwete akichukuliwa maelezo kabla ya kupiga kura |
Ridhiwani Kikwete akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kupiga kura kwenye Kituo cha Kijiji cha Msoga |
Thursday, October 22, 2015
johngagariniblog: DK MAGUFULI KUUFANYA MJI WA CHALINZE KUWA WA KISAS...
johngagariniblog: DK MAGUFULI KUUFANYA MJI WA CHALINZE KUWA WA KISAS...: Na John Gagarini, Chalinze MGOMBEA Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk John Magufuli emesema kuwa endapo atachaguliwa kuwa R...
DK MAGUFULI KUUFANYA MJI WA CHALINZE KUWA WA KISASA
Na John Gagarini, Chalinze
MGOMBEA Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk John
Magufuli emesema kuwa endapo atachaguliwa kuwa Rais atahakikisha mji wa
Chalinze wilayani Bagamoyo mkoani Pwani unakuwa moja ya miji ya kisasa na wa
uwekezaji ambapo utakuwa na barabara za juu Fly Over.
Aidha ujenzi huo ambao utakuwa wa barabara sita hadi jijini
Dar es Salaam utagharimu kiasi cha shilingi trilioni 2.3 na Chalinze itakuwa
kiunganishi cha njia hizo kwenda mikoa ya Kasakazini na mikoa ya Kati ambapo
tayari wataalamu wa upembuzi wa ujenzio huo wamelipwa kiaisi cha shilingi billion
7.7.
Aliyasema hayo kwenye mkutano wa kampeni kwenye Jimbo la
Chalinze mkoani humo ambapo alisema kuwa atahakikisha mji huo unakuwa wa kisasa
na huduma zote muhimu zinapatikana hapo na kuwa mji mbadala wa Dar es Salaam.
Dk Magufuli ambaye ni Waziri wa Ujenzi na Miundombinu alisema
kuwa mji huo utakuwa kituo kikubwa cha uwekezaji hapa nchini kwani faida
nyingine iliyopo ni kugunduliwa gesi eneo la Ruvu hivyo kufanya uchumi wa mji
huo kuwa juu na wananchi wataboresha maisha yao na kuwa na maisha bora.
“Msiuze kiholela maeneo yenu kwani baadhi ya watu wanauza
maeneo kwa bei ndogo lakini watakao nunua watakuja kuuza kwa bei kubwa hivyo
huu ni moja ya miji itakayokuwa ya kisasa hapa nchini na sasa maisha bora
yanakuja na sitawaangusha naomba mnipigie kura nyingi za kutosha ili niweze
kuwa Rais,” alisema Dk Magufuli.
Alisema kuwa kuhusu changamoto ya maji kwenye mji huo alisema
kuwa atahakikisha suala hilo linakwisha ambapo aliipongeza awamu ya tatu na nne
ambazo zimejitahidi angalau maji yanapatikana kwani mji huo ulikuwa na tatizo
kubwa la maji.
Katika hatua nyingine amesema anashangazwa na baadhi ya
wanasiasa kusema kuwa fedha zilizokuwa zijenge bandari ya Tanga zimepelekwa
Bagamoyo kisa ni wilaya anayotoka Rais Dk Jakaya Kikwete.
“Kauli kama hizo ni za uchonganishi kwani kila eneo
limetengewa fedha zake kwa ajili ya ujenzi wa Bandari kuanzia Tanga, Mtwara na
Mwanza kote kutajengwa bandari hizo na Bagamoyo ni uwekezaji wa watu binafsi
hivyo hakuna sababu ya kuwachonganisha watu kwa maneno ya uongo,” alisema Dk
Magufuli.
Alibainisha kuwa hizo ni hoja hafifu na hazina msingi wowote
zaidi ya kuleta uchonganishi kwani wanapaswa kutangaza sera zao na si kuongopa
hali ambayo inajenga chuki baina ya wananchi wa eneo fulani na eneo jingine.
Alisisitiza kuwa endapo atapata
ridhaa ya kuongoza atahakikisha ushuru mdogomdogo unaondolewa ili kuwaondolea
kero wananchi ambao wanataka kujiongezea kipato kutokana na shughuli zao za
ujasiriamali.
Kwa upande wake mgombea Ubunge wa
Jimbo hilo la Chalinze Ridhiwani Kikwete alimshukuru Dk Magufuli kwa mipango
hiyo na kusema kuwa changamoto iliyopo ni ujenzi wa kituo cha afya kikub wa ili
kukabiliana na uwingi wa wagonjwa pamoja na majeruhi kwenye kituo cha afya chya
Chalinze.
Ridhiwani alisema kuwa changamoto
nyingine ni maji ambayo licha ya kupatikana bado kuna baadhi ya maeneo hayapati
maji hasa kwenye makmao makuu ya vitongoji ambapo kwa makao makuu ya vijiji
yote yanapata maji kwa asilimia 94 ambapo Dk Magufuli alisema atashughulikia
changamoto hizo endapo atachaguliwa kuwa Rais.
Mwisho
Mgombea Ubunge Jimbo la Chalinze CCM Ridhiwani Kikwete kulia akisalimiana na moja ya wanachama waliojitokeza kwenye mkutano wa kampeni wa Dk John Magufuli kwenye uwanja wa Miembe Saba Chalinze |
Ridhiwani Kikwete akisalimiana na mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Josia Jackson |
Add caption |
Ridhiwani Kikwete na Dk John Magufuli wakiteta kabla ya kuanza mkutano wa kampeni uliofanyika uwanja wa Miembe Saba Chalinze |
Ridhiwani Kikwete katikati akiteta jambo na mgombea Urais CCM Dk John Magufuli kushoto ni Amoud Jumaa mgombea ubunge Jimbo la Kibaha Vijijini |
Dk Magufuli katikati wakitetea na Ridhiwani Kikwete kushoto na mjumbe wa kampeni Taifa CCM Abdala Bulembo |
Abdala Bulembo akiwaonyesha wananchi wa Chalinze hawapo pichani namna ya kuwapigia kura wagombea wa CCM ngazi ya Urais |
Ridhiwnai Kikwete akizungumza kwenye mkutano huo wa kampeni |
Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM Dk John Magufuli akiongea |
Baadhi ya wagombea udiwani wa CCM kwenye Majimbo ya Chalinze na Bagamoyo wakitambulishwa kwenye mkutano huo wa kampeni |
Dk John Magufuli akifurahi jambo na Ridhiwani Kikwete wakifurahia jambo wakati wa mkutano wa kampeni |
Baadhi ya wanachama wa CCM wakiwa wamejazana kwenye uwanja wa Miembe Saba Chalinze kumsikiliza mgombea Urais wa chama hicho Dk John Magufuli |
Sehemu ya umati wa wanachama na wananchi wa Chalinze wakiwa wanawasikiliza wagombea mbalimbali wa CCM |
Wanachama wa CCM wakiwa wamefurika uwanja wa Miembe Saba Chalinze |
Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM Dk John Magufuli kulia na Ridhiwani Kikwete kushoto wakiombewa duwa mara baada ya mkutano wa kampeni kwenye uwanja wa Miembe Saba Chalinze |
Monday, October 19, 2015
WANAFUNZI HATARINI KUOZWA
Na John Gagarini, Chalinze
WANAFUNZI wawili wa kidato cha tatu waliokuwa wakisoma shule ya sekondari Msata wilayani Bagamoyo mkoani Pwani ambao mwanzoni mwa mwaka jana walilamikiwa na wanafunzi wenzao kuwa wanajihusisha na vitendo vya ushirikina shuleni hapo hali iliyosababisha washindwe kuendelea na masomo wako katika hatari ya kukatishwa masomo kufuatia taarifa kuwa mmoja kaozeshwa kwa mwanaume na mwingine yuko kwenye mipango ya kuolewa.
Wanafunzi hao ambao wanatoka kijiji cha Mkoko kata ya Msata wilayani humo wanadaiwa kuwa wako kwenye hatua hizo baada ya wazazi wao na walezi kushindwa kuwafanyia uhamisho kwenda shule nyingine baada ya wanafunzi wenzao kuwakataa kutokana na madai hayo ya ushirikina.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi moja ya wakazi wa kijiji hicho ambaye hakutaka kutajwa jina lake kutajwa alisema kuwa mwanafunzi wa kwanza (17) anaishi na mwanaume baada ya baba yake kumwoza.
Alisema kuwa baba wa mwanafunzi huyo Damian Joseph alifikia hatua hiyo baada ya mwanae kugoma kuendelea kusoma kwenye shule hiyo na kutaka ahamishiwe shule nyingine kutokana na wenzake kumtuhumu kuwa ni mshirikina.
Baba wa mwanafunzi huyo Joseph alipoulizwa juu ya suala hilo alikanusha na kusema kuwa hajamwoza mwanaye na hana mpango wa kumwozesha kwa kuwa bado ni mwanafunzi ila tatizo lilikuwa ni uhamisho na kufiwa na mkewe.
Akielezea juu ya tatizo la mwanae alisema kuwa mwanawe alikuwa ni mnyonge na kukata tamaa ya kusoma kutokana na wanafunzi wenzake kumtuhumu kuwa ni mchaawi na anawaloga wanafunzi wenzake yeye na mwenzake ambao wanatoka Kijiji kimoja hivyo walishindwa kwenda shule na yeye alikataa kurudi shuleni vinginevyo ahamishiwe shule nyingine.
Joseph alisema kuwa jambo lililomfanya ashindwe kumhamisha mwanae ni kutokana na msiba wa mkewe uliomfanya achanganyikiwe hivyo kusimamisha taratibu za kumhamisha shule hata hivyo amesema kuwa atahakikisha mwanae anawekwenda shule.
Kwa upande wa mwanafunzi (17) ambaye alidaiwa yuko kwenye mchakato wa kutolewa mahari na mwanaume kaka wa mwanafunzi huyo Ramadhan Ndege alikanusha taarifa hizo na kusema kuwa mdogo wake yuko kwa bibi yake mzaa mama ambapo kwa sasa anazaidi ya miezi sita hajaenda shule kutokana na kuwa na matatizo ya mapepo.
Ndege alisema kuwa si kweli kuwa mdogo wake yuko kwenye mpango wa kuozeshwa ila yuko kwa bibi yake akipatiwa matibabu ambapo akienda shule hali inakuwa mbaya kutokana na mapepo kumsumbua.
“Changamoto nyingine ni kukosa fedha kwa ajili ya kumfanyia uhamisho kiasi cha shilingi 250,000 ambazo ni gharama zote kuanzia ufuatiliaji pamoja na sare, vitabu na vifaa vinavyotakiwa kwenye shule anayokwenda ya Changarikwa ambayo ni jirani na kijiji hicho,” alisema Ndege.
Alisema kuwa tatizo kubwa linalowasumbua ni ukosefu wa fedha kwani kipato chao ni kidogo na hawawezi kupata fedha hizo kwa mara moja na msaada ni mdogo kwani wazazi wao walishafariki nakuomba kama kuna wafadhili wanaoweza kuwasaidia wajitokeze ili kuwasaidia kumpeleka shule ndugu yao.
Kwa upande wake mwenyekiti wa Kijiji hicho Hamis Buzoza alisema kuwa mambo hayo yalikuwa yakifanywa kifamilia zaidi lakini masuala hayo hayajapelekwa ofisini kwake ila aliwataka wazazi wa familia hizo kutofanya hivyo kwani hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Mwisho.
WAFUGAJI WALIOINGIA KINYEMELA BAGAMOYO KUONDOLEWA
Na John
Gagarini, Chalinze
WILAYA
ya Bagamoyo imesema kuwa itawaondoa wafugaji wote walioingia kinyemela kwenye wilaya
hiyo ili kuepusha migogoro ya wakulima na wafugaji.
Hayo yalisemwa
na mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Hemed Mwanga, wakati akizungumza na wakazi wa
Kijiji cha Kihangaiko wilayani humo.
Mwanga
alisema kuwa kuna baadhi ya wafugaji wameingia kinyemela kwenye wilaya hiyo
jambo ambalo ni kinyume cha taratibu.
“Tuna
taarifa tunazo kuwa kuna baadhi ya wafugaji wanaingia kinyume cha taratibu hali
ambayo inaweza kusababisha vurugu baina ya wakulima na wafugaji,” alisema
Mwanga.
Alisema
kuwa wafugaji wote walioingia kwa njia za panya wataondolewa kwani kila mahali
kuna taratibu zake na kama walikuwa wanataka kuingia walipaswa kufuata
taratibu.
“Wafugaji
walioingia kinyume cha utaratibu wataondolewa na tumepata taarifa kuwa baadhi
ya mgambo wamekuwa wakihusika kuwaingiza wafugaji hao kinyume cha utaratibu
pale Mto Wami,” alisema Mwanga.
Aidha alisema
kuwa wale wote wanaohusika kuwaingiza wafugaji hao kinyume cha utaratibu
watashughulikiwa kwani wanataka kutoletea matatizo.
Mwisho.
Subscribe to:
Posts (Atom)