Na
John Gagarini, Kibaha
JAMII
nchini imetakiwa kutoa misaada kwa watu wenye uhitaji katika kipindi cha
sikukuu badala ya kuzitumia kwa anasa.
Hayo
yalisemwa na Bi Mwajuma Yasini wakati akishukuru kupewa misaada iliyotolewa
kwenye sikukuu ya Krismasi kwenye hopsitali ya wilaya ya Kibaha Tumbi.
Bi
Yasini alisema kuwa baadhi ya watu wamekuwa wakitumia vibaya fedha kwenye
sikukuu kama hizo kwa kufanya vitendo vya
kifahari huku watu wenye uhitaji wakiwa hawana msaada.
“Ni
vema Watanzania wangetumia sikuu kwa kutoa misaada kwa watu wenye mahitaji
wakiwemo watoto waishio kwenye mazingira magumu, yatima na wagonjwa,” alisema.
Aidha
alisema kuwa ibaada ya kweli ni kuwakumbuka watu wenye uhitaji ambapo wao kama wagonjwa kwao imekuwa faraja katika sikukuu hii ya Krismasi.
Kwa
upande wake mwandishi wa habari na Diwani Viti Maalumu Kibaha Mjini (CCM) Bi
Selina Wilson ambaye ndiye aliyetoa misaada hiyo alisema kuwa alitoa ikiwa ni kama ibaada kwa watu wenye mahitaji.
“Niliona
niungane na wagonjwa kwa kuwapatia zawadi za Krismasi ili nao wajione kuwa
jamii ina wajali na iko pamoja katika hali zote ikiwa ugonjwa na furaha,”
alisema Bi Wilson.
Naye
muuguzi wa zamu wa hospitali ya Tumbi Bi Ndenisaria Ntuah alisema wagonjwa nao
wanahitaji kufarijiwa kwa kupewa misaada mbalimbali.
Misaada
hiyo ilitolewa kwenye wodi za watoto, wazazi na wanawake na wanaume wenye
magonjwa ya kawaida, misaada iliyotolewa ni sabuni, mafuta ya kujipaka, juisi
na biskuti
Mwisho.