Mkuu wa Majeshi nchini Jenerali Jacob Mkunda kupitia uratibu wa Baraza la Michezo la Majeshi ya Ulinzi Dunia (Conseil International du Sports Military) imewaleta wakufunzi na wataalum kutoa mafunzo kwa makocha ikiwa na lengo ni kuwaaendeleza maafisa wa jeshi na aksari wenye taaluma ya ukocha wa Mpira wa miguu kutokana mahusiano mazuri yaliyopo kati ya Tanzania na nchi ya Uholanzi.
Dhamira ya mkuu wa Majeshi ya Ulinzi wa Tanzania ni kupata walimu wazuri watakao saidia timu za jeshi zinazoshiriki ligi mbalimbali na Taifa.
Wakizungumza kwa wakati tofauti makocha ambao ni maafisa wa jeshi na aksari wameshukuru mkuu wa majeshi kwa kuliona hilo ambapo mbali na wakufunzi hao TFFwamekuwa wakitoa mafunzo mbalimbali lakini walimu hawa wakigeni wanavifaa hivyo wanatoa ahadi ya kufanya vizuri katika kuhakikisha timu za majeshi na Taifa zinafanya vizuri.
Mafunzo haya ni ya wiki mbili na ijumaa jioni yatafungwa rasmi hii inatokana na mahusiano mazuri ya Chama Cha Mpira wa Miguu cha Majeshi .
No comments:
Post a Comment