Na John Gagarini, Kibaha
WATU wawili wamefariki dunia na wengine 11
kujeruhiwa mkoani Pwani kufuatia ajali iliyohusisha mabasi madogo mawili ya
abiria kugongana uso kwa uso huko Kiparanganda wilayani Mkuranga.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya
habari mjini Kibaha na Kamanda wa Polisi mkoani humo Bonaventura Mushongi
alisema kuwa watu hao walifariki papo hapo.
Mushongi alisema kuwa ajali hiyo ilitokea Septemba
21 mwaka huu majira ya saa 10:30 jioni T363 DCV likiendeshwa na Zidadu Mohamed (25)
mkazi wa Dar es Salaam akielekea Kimazinchana liligongana na T363DHD yote aina
ya Toyota Hiace likiendeshwa na Miraji Mlonga (22) akielekea Dar es Salaam.
Aliwataja waliokufa kuwa ni Zuhura Haji (21) na
Neema Julius (25) wote wakazi wa Kimazinchana wilaya ya Mkuranga ambapo miili
yao imehifadhiwa kwenye Hopsitali ya Wilaya ya Mkuranga kusubiri ndugu kwa
ajili ya mazishi.
Aidha aliwataja watu waliojeruhiwa kuwa ni Majeruhi
ni Mariamu Aloyce (46) wa Kimazinchana Mariamu Sultan (60) mkzai wa Chanika,
Yusufu Maziku (33) mkazi wa Kimazinchana,Kulwa Abdala (30) makzi wa
Mbagala,Ibrahim Hamis (3) mkazi wa Mbagala na Fatma Abdul (25) mkazi wa
Chanika.
Wengine ni Salum Mohamed (54) mkazi wa Mwalusembe,
Litus Mwarami (26) mkazi wa Kimazinchana Kidawa Abdala (30) mkazi wa Mbagala,
Issa Hemed (2) mkazi wa Kimazinchana na Greyson Ernest (23) mkazi wa
Kimazinchana.
“Tuna washikilia madereva wote waili kutokana na
kusababisha ajali hiyo na watafikishwa mahakamani mara upelelezi wa kesi hiyo
utakapokamilika ili kujibu tuhuma hizo zinazowakabili,” alisema Mushongi.
Kwenye tukio lingine mkazi wa Kwa Mathias Hamis
Tenende (38) aliuwawa kwa kupigwa kisha kuchomwa moto na wananchi wenye hasira
kali kwa madai ya kutaka kuiba pikipiki eneo la Umwelani.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment