Wednesday, March 18, 2015

RIDHIWANI AENDELEA NA ZIARA JIMBONI CHALINZE

Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete kwenye kijiji cha Mkange wakati wa ziara yake kutembelea shughuli za maendeleo, kushoto ni katibu wa CCM wilaya ya Bagamoyo na kulia mwenyekiti wa Kijiji hicho Said Mgaya. 

Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani akiweka udongo kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya cha Kijiji cha Mkange wakati wa ziara yake kutembelea jimbo hilo kuona shughuli za maendeleo. 

Katibu wa chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Bagamoyo Kombo Kamote akizungumza na wajumbe wa halmashauri ya Kijiji cha Matipwili juu ya uwajibijaki kwa wananchi wakati wa ziara ya Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete jimboni humo. 

 Baadhi ya Wazee wa Kijiji cha Matipwili wakimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete hayupo pichani alipokuwa akiwahutubia wakazi hao kwenye mkutano wa hadhara wakati wa ziara ya kutembelea shughuli za maendeleo jimboni humo.

Baadhi ya akina mama wakimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete hayupo pichani  alipokuwa akiwahutubia wakazi wa Kijiji cha Matipwili wakati wa ziara yake ya kutembelea shughuli za maendeleo kwenye jimbo hilo.

 Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya Matipwli wakimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete alipotembelea shule hiyo wakati wa ziara yake jimbo humo kuangalia shughuli za maendeleo

Mzee Halfana Mgobanya wa kijiji cha Gongo akichota maji ya mvua kwa ajili ya matumizi ya nyumbani kijiji hicho ni moja ya vijiji vya jimbo hilo vinavyokabiliwa na tatizo la uhaba wa maji.

 Baadhi ya akinamama wa kijiji cha Mkange wakiwa wanachota maji huku kukiwa na foleni kubwa ya madumu ya maji eneo hilo nalo linakabilia na tatizo la maji ambayo yamekuwa yakitoka mara chache.


 Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete akifyetua tofali wakati akiwa kwenye ziara ya kukagua shughuli za maendeleo kwenye jimbo hilo

No comments:

Post a Comment