Na John Gagarini, Kibaha
HUKU
kiwango cha maambukizi ya ugonjwa wa
UKIWMI wilayani Kibaha Mkoani Pwani kikiwa kimepanda kutoka
asilimia 7 mwaka jana hadi hadi kufikia asilimia 9.7 mwaka huu wakazi wa kata ya Kikongo imetakiwa kuepukana
unyanyapaa ili kupunguza maambukizi mapya.
Taarifa
zinaonyesha kuwa idadi ya waliopata ushauri na kupima kwa kipindi
cha mwezi Januari hadi Desemaba mwaka huku waliopima ni
6,850 kati yao waliokutwa na maambukizi ya VVU ni 665 wanaume 214 na
wanawake 451.
Akizungumza
na wananchi wa kata hiyo wakati wa mafunzo ya kutoa elimu kwa wananchi juu ya
mapambano dhidi ya ugonjwa huo iliyoandaliwa na asasi ya kuwaletea maendeleo
vijana ya Mlandizi Kibaha (YEN), diwani wa kata hiyo Bi Fatuma Ngozi alisema
kuwa moja ya vitu vinavyochangia maambukizi mapya kuendelea ni kutokana na
unyanyapaa ambao unaendelea ndani ya jamii.
Bi Ngozi alisema kuwa unyanyanyapaa unasababisha watu
walioathirika kushindwa kujibainisha hivyo kuendelea kueneza ugonjwa huo
kutokana na kuwa wasiri.
“Jamii inapaswa kuepukana na unyanayapaa ili kuondoa usiri
uliopo kwani endapo wangeweka wazi hali zao ili jamii itambue na kuwasaidia,”
alisema Bi Ngozi.
Alisema kuwa takwimu zinaonyesha maambukizi kuongezeka licha
ya elimu kutolewa kila wakati lakini bado tatizo hilo linaendelea kuwa sugu.
“Kuna sababu nyingi ambazo zimekuwa chanzo cha maambukizi
mapya ya ugonjwa huo lakini mojawapo ni unyanyapaa unaoendelea ndani ya jmii,”
alisema Bi Ngozi.
Kwa upande wake mkurugenzi wa Naye mkurugenzi wa mtandao wa
kuwapatia uwezo vijana (YEN) wa Mlandizi wilyani Kibaha ambao ndiyo walioandaa
tamasha hilo Bw Issa Lukolo alisema kuwa lengo mafunzo hayo ni kuwakumbusha
watu kujikinga na UKIMWI na kuepukana na njia zinazochangia maambukizi mapya.
Lukolo alisema kuwa jamii inapaswa kuepukana na vitendo
ambavyo vimekuwa chanzo cha maambukizi ya ugonjwa huo ambao umekuwa ukimaliza
nguvu kubwa na kusababisha jamii kutumia muda mwingi kuuguza wagonjwa.
Mwisho.
Na John Gagarini, Kibaha
WAZAZI nchini
wameaswa kuhakikisha wanashirikiana na kusimamia malezi ya watoto wao badala ya
kuwaachi wasichana wa kazi hali ambayo inachangia kwa kiwango kikubwa mmmonyoko
wa maadili.
Hayo yalisemwa na Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Pwani Kamishina Msaidizi Mwandamizi Ulrich Matei katika hotuba
iliyosomwa kwa niaba yake na Mkuu wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) Mkoa wa
Pwani Mrakibu Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SSP) Atumani Mwambalaswa wakati wa
mahafali ya sita katika shule ya awali ya Memory Day Care Centre iliyopo
Kibaha Mkoa wa Pwani.
Akizungumza na wazazi pamoja na
walezi wa wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo, Kamanda Mwambalasa alieleza
kuwa ni jukumu la kila familia kuhakikisha kuwa, inajiwekea malengo na mikakati
ya kuhakikisha haizalishi wahalifu bali inazalisha watu wema na waadilifu.
“Kila mmoja katika familia yake
kukataa kuwa na mhalifu na hivyo iwapo sote tukiunganisha nguvu katika mradi
mpya wa Jeshi la Polisi uliozinduliwa hivi karibu na Mkuu wa Jeshi la Polisi
Nchini IGP Said Mwema wa Familia yetu haina Mhalifu basi uhalifu utapungua na
jamii yetu kuwa salama,”. Alisema Kamanda Matei
Kwa upande wake Mkuu wa Dawati la
Jinsi na watoto Mkoa wa Pwani Mrakibu wa Polisi Yusta Milinga, (SP) aliwaomba
wananchi kuendelea kujitokeza kwenye madawati yaliyopo kwenye Mkoa na
kuwafichua wale wote ambao wamekuwa wakifanya vitendo hivyo ili sheria ziweze
kuchukuliwa dhidi yao na amewataka wazazi na walezi kutokubali kuyamaliza
matukio ya ukatili wa jinsi majumbani mwao.
Naye Mkurugenzi wa Kituo hicho Bi
Margareth Njimba alisema kuwa kutokana na kutambua umuhimu wa malezi ya mtoto
na usalama wao katika makuzi, shule yao wameamua kuanzisha tawi la kupambana na
vitendo vya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia katika shule hiyo kwa
kushirikiana na wazazi wa wanafunzi hao pamoja na dawati linalohusika na
maswala ya kupambana na vitendo vya ukatili ndani ya Jeshi la Polisi Mkoa wa
Pwani.
Mahafali hayo ya sita katika shule
hiyo yalienda sambamba na uzinduzi wa tawi hilo uliofanywa na Mkuu wa Kikosi
cha Kutuliza Ghasia (FFU) Mkoa wa Pwani ambapo tawi hilo litakalokuwa na jukumu
la ulinzi na usalama wa Mtoto ili kumfanya awe na makuzi yaliyona maadili
jamii.
Mwisho