Thursday, January 24, 2013

ASKARI AFA AKIELEKEA KUTULIZA GHASIA

Na John Gagarini, Pwani

ASKARI wa Jeshi la Polisi mkoani Pwani Pc Dominik amefariki dunia baada ya gari alilokuwa akisafiria kupinduka baada ya tairi kupasuka.

Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi mkoani humo Ulrich Matei alisema kuwa askari huyo alikufa alipokuwa na wenzake wakitokea wilayani Kibaha kwenda kutuliza ghasia zilizotokea Kibiti wilayani Rufiji.

Kamanda Matei alisema kuwa askari huyo alikufa kwenye ajali ambayo ilitokea jana majira ya kuelekea mchana walipokua wakienda kwenye kutuliza vurugu hizo.

Ajali hiyo iliyotokea ilikuwa ni ya kawaida tu lakini kwa bahati mbaya tumempoteza askari huyo ambaye alikuwa akienda kuwajibika hivyo tunasikitika kutokana na hali hiyo ambayo imeleta majonzi kwa watu wengi, alisema Matei

Awali kabla ya ajali hiyo watu wanaodhaniwa kuwa ni vibaka wamechoma nyumba za polisi na kuharibu mali zao baada ya kuvamia kituo cha polisi kilichopo Kibiti wilayani Rufiji mkoani Pwani kwa madai kuwa polisi walimwua mtuhumiwa.

Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoani Pwani Ulrich Matei alisema kuwa tukio hilo lilitokea jana hali iliyofanya vikosi vya jeshi hilo kwenda huko kutuliza ghasia zilizoibuka.

Kamanda Matei alisema kuwa watu hao walivamia kituo na kutaka kukichoma moto ambapo polisi waliwadhibiti watu hao ndipo walipochoma na kuharibu nyumba za polisi kwa hasira.

Idadi kamili ya nyumba zilizoharibiwa au kuchomwa moto bado haijafahamika rasmi lakini zinakaribia nne hivi na bado tunaendelea kufuatilia kujua idadi kamili za mali zilizoharibiwa na watu hao, alisema Matei.

Alisema mtu aliyekufa alikamatwa na alifia hospitali lakini hakuuwawa na polisi kama baadhi ya madai ya watu ambao waliamua kufanya fujo hizo ambazo zimesababisha hasara ambayo gharama bado haijafahamika mara moja.

Inashangaza kuona watu wanafanya uharibifu ambao hauna maana kwani hata kama mtu huyo aliuwawa na polisi ndiyo sababu ya kufanya fujo kwani huwezi ukaharibu mahakama kwa au kituo cha polisi kwani kinahusiana nini na mtu kuuwawa aliuliza kamanda Matei.

Aidha alisema kuwa tayari watu kadhaa wamekamatwa kuhusiana na tukio hilo na kusema kuwa elimu inatakiwa kutolewa kwa wakazi wa eneo hilo la Rufiji kutokana na kufanya fujo mara kwa mara hali ambayo imekuwa ikivunja amani.

mwisho.

WANAFUNZI WALIOKUTWA NA KONDOMU WAADHIBIWA

Na John Gagarini, Kibaha
HATIMAYE wanafunzi wa sekondari ya Kata ya Maili Moja wilayani Kibaha mkoani Pwani waliokamatwa na mgambo wa kata kwa tuhuma za kutoingia madarasani na kuishia vichakani na kukutwa na kondomu wameadhibi kwa kuchapwa viboko.
Wanafunzi hao walipata adhabu hiyo jana baada ya baraza la kata kuwakuta na hatia ya kujihusisha na vitendo kinyume na taratibu za shule.
Kwa mujibu wa mwenyekiti wa baraza la kata Bw Amadeus Ngombale alisema kuwa wanafunzi hao walikiri kujihusisha na vitendo hivyo kinyume cha maadili ikiwa ni pamoja na kukutwa na kondomu na simu.
“Baada ya kukiri baraza lilitoa adhabu ya viboko kutegemea na kosa la mhusika ambapo adhabu hizo za viboko walichapwa na wazazi wao ambao nao walitwa kwenye baraza hilo,” alisema Bw Ngombale.
Bw Ngombale alisema kuwa wao kama baraza walishatoa adhabu yao na wanatakiwa Jumatatu Januari 28 wanatakiwa kwenda shuleni na wazazi wao ili wapewe taratibu nyingine za shule.
“Bodi ya shule ndiyo itakayoamua hatma ya wanafunzi hao kama watapewa adhabu nyingine au kuwasamehe hilo litaamuliwa na bodi ya shule kwa lengo la kurejesha nidhamu kwa wanafunzi hao,” alisema Bw Ngombale.
Wanafunzi hao waliomba msamaha na kukiri kuwa hawatarudia tena kwani walifanya vitendo hivyo kwa kuiga tu mambo ya ujana.
Wanafunzi hao walikamakamatwa juzi na mgambo wa kata hiyo kwani walikuwa hawaingii madarasani na kuishia njiani huku wengine wakiwa vichakani na kukutwa na kondomu kwenye mifuko yao.

Mwisho.

Wednesday, January 23, 2013

WANAFUNZI WADAKWA

Na John Gagarini, Kibaha
WANAFUNZI 12 wa shule ya Sekondari ya  Kata ya Maili Moja wilayani Kibaha mkoani Pwani wamekamatwa na mgambo wa kata hiyo wakiwa vichakani huku wengine wakikutwa na kondomu kwenye mifuko yao.
Tukio hilo lilitokea juzi mjini Kibaha baada ya mgambo hao kuendesha opereshani kuwakamata wanafunzi ambao hawaingii madarasani na kuishia njiani.
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi ya Kata ya Maili Moja mara baada ya kukamatwa wanafunzi hao, diwani wa kata Bw Andrew Lugano alisema kuwa zoezi hilo ni endelevu kwani baadhi wanafunzi wamekuwa hawafiki shuleni.
“Baada ya kuona kuwa wanafunzi wamekithiri kwa utoro shule ileta suala hili ngazi ya kata na sisi tliamua kuchukua hatua kuwatuma mgambo kuwasaka wanafunzi ambao hawaingii madarasani tulifanikiwa kuwakamata wanafunzi hao ambao ni wa kidato cha tatu na nne,” alisema Bw Lugano.
“Tuliwapekua ambapo tuliwakuta na baaadhi ya vitu ikiwemo ni pamoja na simu na kondomu jambo ambalo ni kinyume cha taratibu za shule na kesho baraza la kata litakaa pamoja na wazazi wao ambao tumewaandikia barua ili waje na ndipo maamuzi yatatolewa dhidi yao,” alisema Bw Lugano. 
Aidha alisema kuwa kata itahakiksha wanafunzi wa shule hiyo wanazingatia maadili ya shule na kuachana na vitendo ambavyo ni kinyume na maadili na wataendeleza operesheni hiyo ili kusafisha shule hiyo ili itoe matokeo mazuri.
Kwa upande wake mwalimu mkuu wa shule hiyo Flora Chibululu alisema kuwa shule yao imekuwa ikidhibiti wanafunzi ambao hawafiki shuleni lakini imekuwa ngumu kwani licha ya kutoa adhabu lakini bado wanafunzi hao hawabadiliki.
Bi Chibululu alisema kuwa wamekuwa wakitoa adhabu zikiwemo za kuwataka wakae nyumbani kwa muda Fulani lakini bado vitendo hivyo bado vinaendelea hali iliyosababisha kuomba kusaidiwa na kata hiyo ambayo iliwapa mgambo kufanya hivyo.
Aliwataka wazazi kutoa ushirikiano kwa shule ili wanafunzi waweze kupata elimu bora kwani vitendo hivyo vinasababisha elimu kushuka kutokana na wanafunzi kutojituma na kufanya matokeo kuwa mabaya.
Mwisho.   
Na John Gagarini, Kibaha
TIMU ya soka Lisborn ya Kongowe wilayani Kibaha imeifunga timu ya Veteran kwa magoli 3-0 kwenye mchezo wa kuwania ngombe wa Mbepo Cup.
Mchezo huo ulipigwa jana kwenye uwanja wa Mwendapole wilayani Kibaha mkoani Pwani ulikuwa mkali na wa kuvutia na kuwakusanya mashabiki wengi akiwemo Diwani wa Kata ya Kibaha Said Nangurukuta na Meya wa Mji wa Kibaha Adhudadi Mkomambo.
Washindi walipata mabao hayo kupitia kwa mshambuliaji wao mahiri Kulwa Mwanda akishirikiana na Jesse Joseph Magoli.
Kulwa alifunga magoli hayo kwenye dakika za 22,64 na 72, michuano hiyo itaendelea Januari 26 mwaka huu kwa mchezo baina ya Mwanalugali na Cargo.
Kutokana na matokeo hayo timu za Nyumbu, Kigogo na Palasupalasu zimefanikiwa kuingia hatua ya robo fainali.
Akiongelea mashindano hayo diwani wa kata ya Kibaha Nangurukuta alisema kuwa mashindano hayo yamefanikiwa kukusanya vipaji vya vijana kwenye kata hiyo na zingine na wilaya ya Kibaha.
Nangurukuta aliwataka wakazi wa eneo hilo kujitokeza kwa wingi ili kuwahamasisha vijana wao kushiriki michezo na kukuza vipaji vyao kwani mbali ya kuboresha afya pia ni ajira kwao.
Mwisho.

Monday, January 21, 2013

WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU (TFS) WILAYANI BAGAMOYO NA MIKAKATI YA KUNUSURU MIKOKO KUMALIZWA

Na John Gagarini

KATIKA kuhakikisha misitu inalindwa hivi karibuni serikali ilianzisha Wakala wa Huduma za Misitu kwenye wilaya zote hapa nchini ili kuboresha usimamizi.
Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) imechukua baadhi ya majukumu kutoka idara ya misitu.
TFS imepewa jukumu la kutunza misitu ya hifadhi ya Taifa (Misitu ya Asili na Mashamba ya Miti), Hifadhi za nyuki na mazao yatokanayo na nyuki.
 Majukumu ambayo TFS imeyachukua ni pamoja na kuanzisha na kusimamia hifadhi za misitu ya asili na hifadhi za nyuki zinazomilikiwa na serikali kuu, kuanzisha na kusimamia mashamba ya miti na mashamba ya nyuki yanayomilikiwa na serikali kuu.
Majukumu mengeine ni kusimamia rasilimali za misitu na nyuki katika misitu ya wazi, kusimamia utekelezaji wa sheria na kanuni katika maeneo yanayoihusu, kuendeleza watumishi, ukusanyaji wa maduhuli ya serikali kutokana na mazao ya misitu na nyuki, kutunza mali na rasilimali na kutafuta masoko ya mazo na huduma ya misitu na nyuki.
TFS imegawanyika kwenye kanda mbalimbali ambapo moja ya Kanda ni ile ya Mashariki ambapo misitu ya serikali kuu wilayani Bagamoyo inaangukia kwenye kanda hiyo.
Meneja wa TFS wilayani humo Bw Charles Mwamfute anaelezea changamoto zinazokabili wilaya hiyo katika misitu ambapo ina eneo la misitu ya hifadhi lenye ukubwa wa hekta 3,883 huku misitu ya hifadhi ya Mikoko ikiwa na ukubwa wa Hekta 5,636.  
Bw Mwamfute akizungumzia hifadhi ya Mikoko ambayo iko pembezoni mwa Bahari ya Hindi kuanzia Kusini mwa Mto Mpiji hadi Kasakazini mwa mto Mlingani ambapo upande wa Mashariki ni Bahari ya Hindi na Magharibi ni bamvua (yanapoishia maji ya Bahari baada ya kujaa) kubwa la maji chumvi ya Bahari.
Alisema misitu ya hifadhi ya Mikoko ni muhimu katika uhifadhi wa viumbe hai wa baharini ikiwemo mazalia ya samaki na kuzuia mmomonyoko wa  kingo za bahari na utunzaji wa mazingira kwa ujumla.
 Alisema kuwa ndani ya eneo hilo kuna Visiwa vyenye miti isiyo ya Mikoko na maeneo hayo maji ya bamvua hayafiki ambapo misitu imezungukwa na Vijiji tisa na maeneo hayo huvamivamiwa mara kwa mara kwa kuwa si mikoko.
“Maeneo mengi yenye Mikoko yameharibiwa sana ambapo kwenye majangwa ya chumvi yana migogoro mingi ambapo wanaotumia maeno hayo hawafuati taratibu ndani ya hifadhi pia hawana hata hati miliki na kuweka Bikoni kinyume na matumizi ya hifadhi ambpo hujiongezea maeneo na kuharibu Mikoko,” alisema Bw Mwamfute.
Alisema baadhi ya athari zilizotokana na kuvunwa miti ya Mikoko ni pamoja na kukosekana mazalio ya samaki jambo ambalo linafanya samaki washindwe kuzaliana na kusababisha kitoweo hicho kuwa adimu.
Alisema baadhi ya maeneo ya hifadhi za Mikoko imekatwa na watu hao, kuchimba chumvi, kuanzisha mabwawa ya kuvua samaki huku wengine wakiifyeka misitu hiyo kwa ajili ya kuona mandhari ya bahari ikiwa baadhi ya wamiliki wa hoteli na watu binafsi.
Aliendelea kusema athari za kufyekwa misitu hiyo ya mikoko kumeanza kuonekana kwani maji yamekuwa yakifika hadi kwenye hoteli na nyumba hizo ambazo zinaonekana kuliwa na maji ya bahari kwa zilizojengwa pembeni ya Bahari.
Alisema kuwa zaidi ya hekta 70 za hifadhi ya misitu ya Mikoko imeharibiwa na watu hao wengine wakiwa ni wawekezaji ambapo katika kukabiliana na uharibifu huo wameshaanza kuchukua hatua kwa kuwapeleka mahakamani waharibifu hao pia kuanza kupanda upya miti hiyo muhimu kwa viumbe hai ambapo moja ya adhabu watakazo zipata watu hao ni pamoja na kupanda miti ya Mikoko na kuwajibika endapo miti hiyo itakatwa.
“Pia tumeanzisha kamati za utunzaji wa misitu hiyo kwenye vijiji ambavyo vinazunguka hifadhi hizo ambapo hutuletea taarifa za waharibifu hao ambao wengine huharibu misitu hiyo nyakati za usiku na kufanya ufuatiliaji kuwa mgumu,” alisema Bw Mwamfute.
Hata hivyo alibanisha changamoto kubwa inayowakabili ni idara ya ardhi kuwapatia watu ardhi kwenye maeneo ya hifadhi jambo ambalo limekuwa likisababisha uharibifu kuendelea kwani watu hao wanabainisha kuwa wanapewa maeneo hayo kihalali.
Aliongeza kuwa ramani za hifadhi hizo ziliwekwa tangu enzi za mkoloni miaka ya 50 kabla hata nchi haijapata uhuru ambapo wakoloni waliilinda misitu hiyo bila ya kuiharibu kinyume na ilivyo sasa ambapo watu wanaiharibu bila ya kuangalia athari zinazoweza kujitokeza.
“Changamoto kubwa tuliyonayo ni ushirikiano mdogo na baadhi ya taasisi ikiwemo ardhi kwenye halmashauri kwani sheria ya misitu inasema mwisho wa hifadhi ya Mikoko ni pale Bamvua linapoishia lakini watu wa ardhi wanagawa ardhi ndani ya eneo hilo ambalo liko ndani ya hifadhi,” alisema Bw Mwamfute.
Alisema changamoto nyingine ni kuwa na watumishi wachache ambapo ni watumishi wawili tu ndiyo wanaofuatilia eneo hilo lenye ukubwa wa zaidi ya hekta 5,000 ya hifadhi ya Misitu ya Mikoko.
Aidha Bw Mwamfute alisema kuwa kutokana na wakala kupewa majukumu ya kusimamia msitu watatumia sheria kuwadhibiti watu wanaoharibu misitu hiyo kwa kuwachukulia hatua kali za kisheria.
Kwa upande wake ofisa misitu wa wilaya ya Bagamoyo Bw Joseph Msaki alisema kuwa kikubwa kinachotakiwa ni watu kupewa mafunzo juu ya utunzaji wa misitu hiyo.
“Kitu kingine tutahakikisha tunapata ramani ya eneo la hifadhi ili kuondoa utata uliopo na kisha kuunda kamati mpya za mazingira za kila kijiji kisha kuweka sheria ndogo ndogo na kuwa na ushirikiano na sekta zingine,”  alisema Bw Msaki.
 Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya ya Mikoko katika Kijiji cha Kiharaka Bw Msafiri Kiponda alisema kuwa baaadhi ya wawekezaji wamefanya uharibifu mkubwa wa kukata mikoko wakidai kuwa wamepewa vibali na watu wa ardhi.
Bw Kiponda alisema kuwa kutokana na mitkoko kufyekwa na wawekezaji hao mazalio ya samaki hakuna hali inayowafanya wakose samaki hivyo kukosa miradi ya uhifadhi wa viumbe hai na hawatoi asilimia yoyote kwenye Kijiji kama sheria inavyowataka.
Kutokana na uharibifu mkubwa wa hifadhi ya Misitu ya mikoko na ile mingine kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Bagamoyo ikongozwa na mkuu wa wilaya hiyo Bw Ahmed Kipozi ilitembelea misitu hiyo na kujionea hali mbaya ya misitu.
Mkuu wa wilaya hiyo alitaka apewe majina ya watu waliojenga kwenye hifadhi ya misitu ya Mikoko kwani wamesababisha uharibifu mkubwa ambo hautaweza kuvumiliwa kwani athari za kuharibu misitu hiyo ni kubwa ikilinganishwa na faida itakayopatikana ni kwa watu wachache huku wengi wakiathirika kwa kuharibiwa mazingira.
Bw Kipozi alisema kuwa mbali ya kupewa majina ya watu waliojenga na kuharibu mikoko pia apewe majina ya maofisa wa ardhi toka halmashauri ambao waliwapatia watu ardhi kwenye maeneo ya hifadhi ya Mikoko na kusababisha uharibifu huo mkubwa kwa wilaya ya Bagamoyo.
Aliwataka watendaji wa halmashauri kushirikiana na wakala hao ili kuepusha kuvunwa misitu hiyo ya Mikoko kwani kugawa maeneo hayo ya hifadhi ni kuchangia kuendeleza uharibifu ndani ya hifadhi hiyo.
Mwisho.

MIKOKO KUTOWEKA BAGAMOYO