WAKALA wa Barabara Tanzania (TANROADS) imetoa ufafanuzi juu ya taarifa inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii ya lori la mizigo lililokamatwa kwenye mizani ya Vigwaza kuwa taratibu za kulikamata lori hilo ulifuatwa.
Thursday, March 20, 2025
TANROADS YATOA UFAFANUZI LORI LILILOZIDISHA UZITO MIZANI YA VIGWAZA.
TCRA KUSHIRIKIANA NA TBN KUSADIA KUZALISHA MAUDHUI YENYE TIJA
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeahidi kufanyakazi na Mtandao wa Wana Blogu Tanzania (TBN) pamoja na vyama vingine vya waandishi wa habari ambavyo vinawakilisha mahitaji na matakwa ya wanachama wao.
Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 19 Machi 2025 Jijini Dar es Salaam na Meneja wa Huduma za Utangazaji wa TCRA, Mhandisi Andrew Kisaka, alipokutana na ujumbe wa TBN ofisini kwake, katika kikao cha kujadiliana changamoto mbalimbali zinazowakabili Bloga nchini.
“Sisi huwa tunapenda kufanya kazi na vyama ambavyo vinawakilisha mahitaji na matakwa ya wanachama wao, badala ya kufanyakazi na mwaandishi mmoja mmoja…tunafurahi sana kufanyakazi na waandishi kupitia vyama vyao,” amesema Mhandisi Kisaka.
Mhandisi Kisaka amesema kuwa TCRA imefurahi kukutana na TBN kwa kuwa wanafahamu kuwa Bloga wanasehemu kubwa sana kwenye maudhui ya ndani, na hata kwenye usajili wa TCRA Bloga wanachukua nafasi kubwa sana katika maudhui ya mtandaoni.
“Kwa hiyo TBN mtakuwa silaha moja wapo nzuri sana yakutuwezesha sisi kama Mamlaka ya Mawasiliano nchini, tunao simamia utangazaji pamoja na maudhui ya mtandaoni kuwa karibu na nyinyi na kuhakikisha maudhui ya mtandaoni yanaleta tija na maendeleo kwa wananchi,” amesema Mhandisi Kisaka.
Friday, March 14, 2025
RAIS MSTAAFU DK KIKWETE AFANYA ZIARA NCHINI JAPAN KUIMARISHA USHIRIKIANO KATI YA BODI YA SHIRIKA LA ELIMU LA KIMATAIFA (GPE) NA JAPAN
Rais mstaafu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akiwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Elimu la Kimataifa (GPE), yupo Tokyo nchini Japan kwa ziara maalum yenye lengo la kuimarisha ushirikiano kati ya GPE na serikali ya Japan katika kutatua changamoto za elimu ya msingi katika nchi zinazoendelea.
Katika siku yake ya kwanza Tokyo, Dkt. Kikwete amefanya mazungumzo na Waziri wa Fedha wa Japan, Mhe. Shin-ichi Yokohama, pamoja na Naibu wake, Mhe. Atsushi Mimura.
Mazungumzo hayo yalijikita katika ushirikiano wa kifedha ili kusaidia miradi ya elimu inayosimamiwa na GPE, ikiwemo upatikanaji wa rasilimali kwa ajili ya kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa watoto wa nchi zinazoendelea.
Baada ya mazungumzo hayo, Rais Mstaafu Kikwete alikutana na Bw. Akihiko Tanaka, Rais wa Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Japan (JICA).
Shirika hili limekuwa na mchango mkubwa katika miradi ya maendeleo barani Afrika, na mazungumzo yalihusu namna JICA inaweza kusaidia jitihada za GPE katika kukuza elimu bora.
Dkt. Kikwete pia alikutana na Bw. Yohei Sasakawa, Mwenyekiti wa Taasisi ya Nippon. Bw. Sasakawa, mwenye umri wa miaka 86, ni mtu mashuhuri wa kusaidia miradi ya kijamii duniani.
Katika mazungumzo yao, waligusia nafasi ya sekta binafsi katika kusaidia elimu, hasa kupitia taasisi zisizo za kiserikali. Vilevile, Bw. Sasakawa alishangaza dunia baada ya kufanikisha kupanda Mlima Kilimanjaro tarehe 12 Februari 2024, kama sehemu ya maadhimisho ya miaka 85 ya kuzaliwa kwake – hatua inayothibitisha kuwa umri si kikwazo kwa ndoto kubwa.
Katika siku zinazofuata, Rais Mstaafu Kikwete anatarajiwa kukutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan, Mhe. T. Miyaji, pamoja na wabunge wa Bunge la Japan, ambapo ajenda kuu itakuwa nafasi ya elimu na teknolojia katika maendeleo ya jamii.
Pia, atashiriki mijadala maalum kuhusu elimu na teknolojia, kufanya mahojiano na vyombo vya habari, pamoja na kukutana na Mhe. Tetsuro Yano, Rais wa Taasisi ya AFRECO, ambayo inahusika na kukuza ushirikiano kati ya Japan na Afrika.
Ziara hii ni sehemu ya juhudi endelevu za Dkt. Kikwete katika kuboresha mifumo ya elimu duniani, hasa katika nchi zinazoendelea.
Japan ni mshirika muhimu wa maendeleo ya elimu barani Afrika, na ushirikiano huu unaweza kuwa na mchango mkubwa katika kuhakikisha watoto wengi zaidi wanapata fursa ya elimu bora.
Thursday, March 13, 2025
KIWANDA CHA KEDS CHATOA MSAADA KWA WANAWAKE
KIWANDA cha kuzalisha sabuni cha Keds Tanzania Company Ltd cha Kibaha Mkoani Pwani kimetoa misaada ya sabuni kwa wanawake wa Mtaa wa Lulanzi ambao uko jirani na kiwanda hicho ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya sherehe ya siku ya wanawake Duniani.
KEDS KUENDELEA KUZALISHA BIDHAA BORA
KIWANDA cha Keds Tanzania Company Ltd kimesema kitaendelea kuzalisha bidhaa zenye ubora na bei nafuu kulingana na hali ya soko.