Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa kamati ya ukatili wa kijinsia mkoa wa Dodoma Grace Ringo wakati wa mafunzo ya utoaji wa elimu katika chuo Mipango chini ya uongozi wa Binti Makini kuhusu kupinga unyanyasaji kwa wanawake.
Amesema yapo mambo ambayo mwanamke wanakutana nayo kama Ulawiti, kupigwa , pamoja na kukosa haki ambazo zinamfanya mwanamke akashidwa kujiamini katika nafasi yake na kupelekea anguko la uchumi katika jamii hata familia hivyo niwaombe Mabinti ambao mmepata elimu leo muhakikishe mnasaidia jamii
Kwa upande wake Mjumbe wa kamati ya ukatili wa kijinsia Mkoa wa Dodoma Irene Sanga amewasihi Mabinti kutumia mitandao kwa ajiri ya kuwaingizia kipato na sio kutumia mitandao kwa kufanya mambo maovu huku akiwasisitiza wawe na nidhamu Katika jamii ya leo
"Wapo Mabinti ambao wanatumia mitandao kwa kuangalia vitu visivyofaha na kupelekea Vijana kualibika kwa kuiga mambo ambayo kwa nafasi na umri bado na kulazimisha kufanya vitu kama rushwa za ngono," amesema Sanga.
Naye Mjumbe wa kamati ya kupinga ukatili chini ya ofisi ya Mkoa wa Dodoma Rhoda Denis amewataka wasichana kuzingatia kujithamini na kujitambua Ili kujikomboa katika maisha ya jamii ya leo.
"Wapo wanawake wanapigwa na waume zao sababu kukosa kujitambua ila kama utajua thamani yako utaweza kufika sehem ambayo utaweza kupata msaada," amesema Rhoda
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Binti Makini Chuo Cha Mipango Dodoma Swaumu Rajabu amewahimiza wanawake kujitokeza kugombania nafasi mbalimbali za uongozi kwani wanawake tunanafasi kubwa sana katika jamii leo hivyo tuwe mstari wa mbele kuwasihi na wengine unaowaona wanaweza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika nchi yetu .
Aidha amesema kuwa chuo Cha mipango kinaenda kufanyika uchaguzi wa viongozi wa serikali ya wanafunzi ikiwemo nafasi mbalimbali kama Rais wa chuo Cha mipango, wabunge pamoja nafasi nyingine hivyo amewaomba Binti Makini wote wenye sifa wajitokeze wakagombee nafasi hizo.
Ikumbukwe kuwa kamati ya Kupinga Ukatili wa kijinsia iliyochini ya wanawake na Samia inaendelea kufanya mafunzo ya utoaji wa elimu kwa wanawake na wanaume ili kuhakikisha elimu hii inawafikia wengi ili kutengeneza Taifa lenye nguvu kazi na lenye Maadili ikiwa na kauli mbiu IPELEKE DODOMA DUNIANI NA DUNIA ILETE DODOMA