Friday, February 1, 2013

KINYOZI ADAKWA KWA KUISHI NA MWANAFUNZI



Na Mwandishi Wetu, Kibaha

SAKATA la kutafuta wanafunzi watoro katika shule ya Sekondari ya Bundikani Kata ya Maili Moja wilayani Kibaha limeibua mapya baada ya mwanafunzi wa kidato cha pili kukutwa kwa kwa mwanaume ambaye ni kinyozi baada ya kushindwa kwenda shule kwa muda wa siku tatu.
Mwanafunzi huyo ambaye ni miongoni mwa wanafunzi waliofeli mtihani wa kidato cha pili mwaka jana na kutakiwa kurudia kidato cha pili mwaka huu, alikutwa kwa kijana huyo Martin Joseph (16) mkazi wa Maili Moja shuleni jirani na shule hiyo.
Tukio hilo lilitokea juzi baada ya kijana huyo kukamatwa na mgambo wa kata ambao wamepewa kazi ya kuwakamata wanafunzi watoro wa shule hiyo ambapo hivi karibuni baadhi ya wanafunzi walikamatwa porini huku wengine wakiwa na kondomu na kupewa adhabu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuchapwa viboko na wazazi wao kwenye baraza la kata hiyo.
Kijana huyo alifikishwa kwenye baraza la usuluhishi la kata ya Maili Moja  linaloongozwa na mwenyekiti Bw Amadeus Ngombale, aliskiri kukaa na mwanafunzi huyo kwa kipindi hicho licha ya kuwa mwanafunzi huyo kutokwenda shule tangu ilipofunguliwa mwanzoni mwa mwezi huu.
“Mimi sikujua kama ni mwanafunzi kwani hakuniambia anasoma shule na nilikaa naye kwa siku tatu ila nilishangaa kuona mgambo wamekuja ofini kwangu na kunikamata kwa madai kuwa ni kwanini nimekaa na mwanafunzi na kumsababisha asiende shule,” alisema Joseph.
Kwa upande wake mwalimu mkuu wa shule hiyo Flora Chibululu alisema kuwa mwanafunzi huyo ni moja kata ya wanafunzi wlaiofeli mwaka jana kidato cha pili na kutakiwa kurudia kidato hicho lakini walishangaa ni kwanini haendi shule.
“Huyu mwanafunzi ni miongoni mwa wale wanaorudia kidato cha pili mwaka huu na baada ya kukutwa kwa mwanaume tulimpa barua aje na mlezi wake ambaye ni bibi yake ambaye ndiye anayeishi naye,” alisema Chibululu.
Aidha alisema kuwa mwanafunzi huyo alisema kuwa anaishi na bibi yake kwa sababu baba yake hamtunzi kutokana na tabia zake ambazo zimekuwa ni kero.
Kijana huyo kutokana na kukubali tuhuma hizo alipelekwa polisi kwa ajili ya kufikishwa mahakamani kutokana na tukio hilo ambalo ni moja ya changamoto kubwa kwa wanafunzi wa kike kwenye wilaya ya Kibaha na mkoa wa Pwani
Mwisho.

 

Wednesday, January 30, 2013



Na John Gagarini, Kibaha
MWANAFUNZI ambaye ni miongoni mwa wanafunzi waliofeli kidato cha pili mwaka jana kwenye shule ya sekondari ya Tumbi wilayani Kibaha mkoani Pwani Shaban Kihemele (16) ametoroka nyumbani kwa madai kuwa wanafunzi wenzake kumzomea kuwa amerudia darasa.
Akizungumza na waandishi wa habari hizi mjini Kibaha mzazi wa mtoto huyo Bw Shaban Kihemele alisema kuwa mwanae huyo huyo alitoroka Januari 24 mwaka huu na hadi leo hajaonekana licha ya jitihada za kumtafuta kushindwa kufua dafu.
Bw Kihemele alisema kuwa mwanae aliondoka nyumbani majira ya saa 4 asubuhi huku akiwa amevalia kaptura nyeusi ya Jeans iliyokatwa tisheti ya rangi ya zambarau yenye ufito mweupe kifuani na ndala nyekundu.
“Chanzo cha yeye kutoroka siku ya Januari 23 alimwambia mama yake kuwa kutokana na kufeli mtihani wa kidato cha pili ni vema wamwamishe shule kuliko kuendelea kusoma hapo kwani wanafunzi wanaomfahamu wanamzomea lakini mama yake alimwambia asubiri mimi nirudi kwani sikuwepo nilikuwa Bagamoyo kikazi,” alisema bw Kihemele.
Alisema mama yake alimjibu kuwa asubiri hadi nirudi lakini kesho yake alirudi kutoka shuleni na kubadilisha nguo huku majirani wakimwuliza kuwa ni kwanini amewahi kurudi na anakwenda wapi akawaambia yuko hapa hapa pia baba yake hajalipa ada hivyo amerudishwa.
“Alichukua fedha kiasi cha shilingi 20,000 kati ya shilingi 50,000 zilizokuwepo kasha akachukua na shuka kisha kuondoka kusikojulikana na inawezekana aliotoroka kutokana na kuona kuwa ni fedheha kurudia darasa na madai kuwa wenzake wanamzomea jambo ambalo linatushangaza,” alisema Bw Kihemele.
Aidha alisema siku ya kwanza walimsubiri hakutokea na ilipofika usiku walikwenda kutoa taarifa kituo cha polisi cha Maili Moja KMM/RB/108/2013 juu ya kutoonekana mtoto wao, walikwenda nyumbani kwao Bagamoyo lakini hawajaweza kufanikiwa kumwona pia waliwasiliana na ndugu zao wote lakini imeshindikana.
Mwisho.

HABARI ZA PWANI




Na John Gagarini, Mkuranga
IMEELEZWA kuwa kuishi mbali na vituo vyao vya kazi kwa baadhi ya maofisa
ugani kwenye vijiji wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani kumechangia kudumaza
shughuli za kilimo wilayani humo.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mafunzo kwenye kijiji cha
Msufini kata ya Mbezi, mratibu wa mradi wa Wajibu wa Jamii Katika Usimamizi
wa Rasilimali za Umma za Sekta ya Kilimo wilaya hiyo (POCUSO), Bw Said
Gwaja alisema kuwa maofisa hao wamekuwa hawafiki kwenye vijiji
walivyopangiwa.

Bw Gwaja alisema kuwa kutokana na kuishi mbali na vituo vyao vya kazi
wamekuwa wakiishia ofisini na kushindwa kwenda kwenye maoeneo waliyopangiwa
hasa yale ya vijijini.

“Ni vema wangekaa kwenye maeneo yao ya kazi ili iwe rahisi kwao kutoa
huduma kwa wakulima ambao wanakosa fursa nyingi kutokana na kutofahamishwa
namna ya kuweza kuzipata,” alisema Bw Gwaja.

Alisema kuwa fursa ambazo wakulima walipaswa kuzijua zinashindwa kuwafikia
kwani wanazipata wakati muda wa kilimo unakuwa umepita hivyo kushindwa kupata pembejeo za ruzuku kwa wakati muafaka.
Aidha alisema kuwa endapo wangekuwa wanafanya kazi kwenye maeneo waliyopangiwa hususani vijijini ingekuwa raisi kwao kujua chanagamoto zinazo wakabili wakulima hivyo ingekuwa rahisi kuwasaidia kuliko ilivyosasa.
Aliwataka wakulima kujitokeza kwenye mafunzo yanayoandaliwa na shirika lake ili waweze kujua namna ya kufuatilia matumizi ya rasilimali za wananchi zikiwemo zile za kilimo ambazo nyingine zinawalenga wao moja kwa moja.
Mwisho.
Na Mwandishi Wetu, Mkuranga
WANANCHI wametaka katiba mpya iwe na kipengele cha wafanyakazi wa serikali kufanya kazi kwa mkataba wa miaka 10 ili aweze kuwajibishwa endapo utendaji kazi wake hautaridhisha.
Hayo yalisemwa jana Mkuranga na Bw Mohamed Abdul wakati wa Mdahalo wa Katiba kwa wakazi wa Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani uliandaliwa na Mtandao wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali wilayani Mkuranga (MKUNGONET).
Alisema kuwa baadhi ya wafanyakazi wa serikali wamekuwa hawatekelezi vema majukumu yao hali inayofanya washindwe kuwaletea maenedeleo wananchi ambao wanaamini kuwa elimu walizonazo hawazitumii kikamilifu.
“Tungetaka katiba iwe na kipengele cha wafanyakazi wa serikali kuwa na mkataba wa miaka 10 ili akifanya vema aongezewe mkataba na kama akifanya vibaya asiongezewe mkataba wa kazi,” alisema Bw Abdul.
Alisema kuwa endapo kutakuwa na mikataba ya muda wa kufanya kazi kutaleta uwajibikaji sehemu za kazi tofauti na ilivyo sasa baadhi ya wafanyakazi kutowajibika kwa kuamini kuwa hawawezi kuondolewa kazini hata kama wameboronga.
Aidha alisema kuwa pia sifa za wataalamu  mbalimbali ziwekwe kwenye mbao za matangazo ili wananchi waweze kujua uwezo wa wataalamu hao.
“Hii itasaidia kuwawajibisha wataalamu hao ambao wataonekana uwezo wao ni mdogo kwani baadhi hawana uwezo,” alisema Bw Abdul.
Kwa upande wake mratibu wa MKUNGONET Bw Mohamed Katundu alisema kuwa lengo la mdahalo huo ni kuwaelekeza namna ya kutoa maoni yao juu ya marekebisho ya katiba mpya.
Bw Katundu alisema kuwa mdahalo huo uliofadhiliwa na The Foundation for Civil Society ulihudhuriwa na madiwani, wataalamu toka wilayani, mashirika mbalimbali yasiyo ya kiserikali na wananchi.
Mwisho.   
Na John Gagarini, Kibaha
MWANAFUNZI ambaye ni miongoni mwa wanafunzi waliofeli kidato cha pili mwaka jana kwenye shule ya sekondari ya Tumbi wilayani Kibaha mkoani Pwani Shaban Kihemele (16) ametoroka nyumbani kwa madai kuwa wanafunzi wenzake kumzomea kuwa amerudia darasa.
Akizungumza na waandishi wa habari hizi mjini Kibaha mzazi wa mtoto huyo Bw Shaban Kihemele alisema kuwa mwanae huyo huyo alitoroka Januari 24 mwaka huu na hadi leo hajaonekana licha ya jitihada za kumtafuta kushindwa kufua dafu.
Bw Kihemele alisema kuwa mwanae aliondoka nyumbani majira ya saa 4 asubuhi huku akiwa amevalia kaptura nyeusi ya Jeans iliyokatwa tisheti ya rangi ya zambarau yenye ufito mweupe kifuani na ndala nyekundu.
“Chanzo cha yeye kutoroka siku ya Januari 23 alimwambia mama yake kuwa kutokana na kufeli mtihani wa kidato cha pili ni vema wamwamishe shule kuliko kuendelea kusoma hapo kwani wanafunzi wanaomfahamu wanamzomea lakini mama yake alimwambia asubiri mimi nirudi kwani sikuwepo nilikuwa Bagamoyo kikazi,” alisema bw Kihemele.
Alisema mama yake alimjibu kuwa asubiri hadi nirudi lakini kesho yake alirudi kutoka shuleni na kubadilisha nguo huku majirani wakimwuliza kuwa ni kwanini amewahi kurudi na anakwenda wapi akawaambia yuko hapa hapa pia baba yake hajalipa ada hivyo amerudishwa.
“Alichukua fedha kiasi cha shilingi 20,000 kati ya shilingi 50,000 zilizokuwepo kasha akachukua na shuka kisha kuondoka kusikojulikana na inawezekana aliotoroka kutokana na kuona kuwa ni fedheha kurudia darasa na madai kuwa wenzake wanamzomea jambo ambalo linatushangaza,” alisema Bw Kihemele.
Aidha alisema siku ya kwanza walimsubiri hakutokea na ilipofika usiku walikwenda kutoa taarifa kituo cha polisi cha Maili Moja KMM/RB/108/2013 juu ya kutoonekana mtoto wao, walikwenda nyumbani kwao Bagamoyo lakini hawajaweza kufanikiwa kumwona pia waliwasiliana na ndugu zao wote lakini imeshindikana.
Mwisho.
Na John Gagarini, Kibaha
DIWANI wa kata ya Picha ya Ndege wilayani Kibaha mkoani Pwani Bw Bosco Mfundo kupitia chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) juzi alitolewa nje kwenye kikao cha baraza la Madiwani wa halmashauri ya Mji wa Kibaha baada ya kusema kuwa meya wa mji huo Bw Adhudadi Mkomambo ni mwizi.
Sakata la diwani huyo maarufu kama Obama kutolewa nje lilikuja wakati wa kikao cha madiwani kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo uliopo Kibaha.
Chanzo cha diwani huyo kutolewa nje ni kukataa kupokea taarifa ya halmashauri na kusema kuna wizi umefanyika kwenye taarifa ya fedha na mwenyekiti ni mwizi jambo ambalo lilimfanya meya huyo kumtaka diwani huyo atoke nje kwa muda kabla ya kurejea na kuendelea na kikao.
“Nilikataa taarifa ya mwenyekiti wa halmashauri kwa sababu kuna wizi umefanywa na halmashauri ya mji wa Kibahakiasi cha shilingi milioni 533 zinaoneka zimeibwa ni wazi taarifa hii ni kuanzia mwezi Oktoba hadi Desemba lakini inaleta matumizi ambayo yalishaletwa kwenye taarifa ya robo ya mwaka uliopita,” alisema Bw Mfundo.
Alisema kuwa kitendo cha wao kutohoji taarifa na kuikubali na kuridhia wizi uliofanyika hadi mwenyekiti anamtoa nje ni wazi naye ni shemu ya wizi huo.
“Mimi ni mwakilishi wa wananchi hivyo siwezi kuridhia kuona fedha za walipa kodi zinachotwa na kutumika kinyume cha taratibu sikotayari,” alisema bw Mfundo.
Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashauri hiyo Bw Mkomambo alisema kuwa alimtoa kwenye kikao kwa kufuata kanuni za baraza kwa kutoa lugha mbaya.
“Lugha aliyotumia ilikuwa inahatarisha kikao kishindwe kuendelea na ni jambo ambalo ni kinyume kwani ni utovu wa nidhamu kutumia lugha mabya kwenye kikao kama hicho ambacho ni cha kisheria,” alisema Bw Mkomambo.
Bw Mkomambo alisema kuwa anashangaa diwani huyo kumwita kuwa yeye ni mwizi kwani kama kaiba kaiba nini hasa ikizingatiwa kuwa taarifa hiyo ya fedha ilipitiwa chama chetu na chama chake kabla ya kuletwa kwenye baraza na kama kulikuwa na hoja si wangeileta kwa maandishi juu ya hilo.
“Nawasii madiwani kufuata kanuni na taratibu na kuacha jazba hata kama kuna jambo lazima lifuate taratibu na si kuwa na jazba kwani wanapaswa kutetea maslahi ya wananchi ili kuwaletea maendeleo,” alisema Bw Mkomambo.
Mwisho.
Na John Gagarini, Kibaha
MKUU wa Mkoa wa Pwani amesema kuwa kupatikana kwa greda la kuchongea barabara kwa Halmashauri ya Mji wa Kibaha kuwe changamoto ya kukabiliana na miundombinu mibovu ya barabara za mji huo.
Aliyasema hayo kwenye uzinduzi wa greda hiloa na gari la kuzolea uchafu ambapo taarifa yake ilisomwa na mkuu wa wilaya ya Kibaha Bi Halima Kihemba na kusema kuwa kwa sasa hakuna haja ya kusema kuwa kuna kiporo cha mradi wa barabara.
Alisema kuwa miradi mingi ya barabara ilikuwa inakwama kwa sababu ya kuwa na bajeti ndogo ya kuwalipa wakandarasi kwa ajili ya kufanya kazi hiyo lakini kwa sasa watakuwa wameondokana na kujenga barabara kwa gaharama kubwa.
“Tunawapongeza kwa kununua greda hili ambalo lina thamani ya shilingi milioni 528 zikiwa ni fedha za mapato yenu ya ndani, sasa mtaondokana na kuweka viporo vya miradi ya barabara kwani sasa hivi mtakuwa mkiweka mafuta tu na kutengeneza barabara zenu wenyewe,” alisema Bi Mahiza.
Bi Mahiza alisema kuwa mbali ya kutengeneza barabara hizo wao wenyewe kwa gharama nafuu pia wataweza kulikodisha kwa wakandarasi mbalimbali ndani na nje ya mkoa hali itakayosababisha kujiongezea mapato ya halmashauri.
Aidha alisema kuwa mbali ya kununua greda hilo changaamoto nyingine inayowakabili ni namna ya kulitunza hivyo wanapaswa kuwa makini ili liweze kuleta manufaa kwa halmashauri na wananchi ambao sasa wataondokana na kero ya barabara.
Akizungumzia gari la kuzolea uchafu ambalo limetolewa kama msaada na kutoka Gotland Sweden alisema litasaidia kuboresha mazingira ya mji huo kwani gari walilokuwa nalo mwanzo lilikuwa dogo hivyo kushindwa kumudu uchafu uliopo.
Aliwataka wananchi kulitumia gari hilo kwa kuweka mazingira yao katika hali ya usafi kuondokana na kero hiyo ambayo ilikuwa ni kubwa kwa muda mrefu 
Kwa upande wake kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya Mji wa Kibaha Bi Lweah Lwanji alisema kuwa wamejipanga kuvitumia vyombo hivyo katika kuboresha barabara za mji na kuuweka katika usafi ili ufanane na ile ya Moshi na Arusha.
Mwisho.   


Monday, January 28, 2013

WAHAMIAJI HARAMU WADAKWA



Na John Gagarini, Kibaha
JESHI la Polisi mkoani Pwani linawashikilia wahamiaji haramu watano wa nchi ya Ethiopia na Somalia kwa kuingia nchini bila ya kibali.
Kwa mujibu wa kamanda wa Polisi mkoani humo Ulrich Matei alisema kuwa raia hao walikamatwa wakati wa msako wa kukamata wahamiaji haramu.
Kamanda Matei alisema kuwa wahamiaji haramu hao walikamatwa Januari 23 mwaka huu huko Kitongoji cha Kibosha Kijiji cha Mapinga wilayani Bagamoyo.
“Wahamiaji haramu hao walikamatwa wakiwa wanasafirishwa kwenye gari namba T 371 BTL aina ya Noah,” alisema Kamanda Matei.
Alisema kuwa gari hilo lilikuwa likiendeshw ana Bw Evarist Mbilinyi (25) dereva wa Mwananyamala Jijini Dar es Salaam akisaidiwa na Omary Karim (28) fundi magari mkazi wa Magomeni Makuti wakielekea Ethiopia kupitia Bagamoyo.
Aliwataja wahamiaji hao kuwa ni Itemegen Wolde (20) mwanafunzi, Beyene Dutano (25), Aduel Ashebo (24) na Detene Bore (25) kutoka nchini Ethiopia na Abdirsa Abdilim (20) ambaye ni raia wa nchi ya Somali.
Mwisho.